Am I a loner,selfish?

Am I a loner,selfish?

Habari za Pasaka. Jana ilikuwa sikukuu hivyo nilipata mialiko. Ajabu nilikataa mialiko yote nikaamua kukaa nyumbani peke yangu siku nzima na sikuboreka hata kidogo kwasababu nishazoea na nilipanga nisitoke.

Mwaliko wa kwanza Bi Mkubwa kanipigia asubuhi,anajua nakaa mwenyewe, kaniomba niende nyumbani nikajumuike nao. Bila kujiuliza nikamjibu leo sitaweza kuja nimetoka nje ya mji wakati nimepanga kushinda nyumbani.

Baadae kanipigia binamu wangu,me, kaniomba aje nae nikamwambia leo sitakuwepo nyumbani. Wa mwisho rafiki yangu mkubwa kanipigia jioni kaniuliza kama nipo tu nyumbani anipitie tukasafishe macho maeneo fulani, huyu nilimjibu tu kuwa nipo ila leo sitoki.

Nimekaa nikajifikiria naweza kuwa mbinafsi au loner fulani bila kujijua? Maanake napenda sana kukaa mwenyewe nyumbani au naweza kwenda sehemu ya starehe peke yangu. Na kuna marafiki wananishangaa nawezaje kukaa mwenyewe siku nzima!

Girlfriend Je?🙂🙂
 
True loners do not join JF.
Thats your own view nd not a fact...

through my own experience with jf members i hav come accross physically,most of them are loners that jf is the only place they meet "people of their own kind"..

Most loners don find themselves energetic when they are sorrounded with a lot of people and also seems to prefer things which worth their intelligence ....

Nenda insta ama snapchat,huko ndo kuna attention seekers na viumbe wanaojichanganya sana na watu yaani wataigiza uhalisia unaokubalika kinyume na wao walivyo...

Kukaa pekee kuna raha ila kuzidisha ni karaha... TOO MUCH IS HARMFUL ALWAYS
 
Tuko wengi kumbe....
Nilichogundua kuna watu wengi wana hii tabia. Wengi humu wanachanganya upweke na mtu kupenda kukaa ndani. Nakaa ndani kwa kupenda na nina enjoy kila dakika, naweza kuwa naangalia tv, na browse jf au nasikiliza muziki.

Nikijisikia kukaa na watu natoka naenda walipo au nawaita home wanakuja. Ila ndio nikiamua kukaa ndani hata uwe mwaliko wa umuhimu gani, sitoki.
 
hata mimi napenda kukaa mwenyewe sana sema siku hizi nimeacha kwasababu ya rafiki yangu kila saa ananifata
 
Thats your own view nd not a fact...

through my own experience with jf members i hav come accross physically,most of them are loners that jf is the only place they meet "people of their own kind"..

Most loners don find themselves energetic when they are sorrounded with a lot of people and also seems to prefer things which worth their intelligence ....

Nenda insta ama snapchat,huko ndo kuna attention seekers na viumbe wanaojichanganya sana na watu yaani wataigiza uhalisia unaokubalika kinyume na wao walivyo...

Kukaa pekee kuna raha ila kuzidisha ni karaha... TOO MUCH IS HARMFUL ALWAYS
If you join JF, you wish to communicate with others.

Therefore, you are not a true loner.

True loners do not join JF.

Why woyld a true loner join JF?

Sent from my LGLS992 using JamiiForums mobile app
 
me nina tabia kama yako ila nahisi mimi kuna jambo lilinitokea ndugu wakawa against mimi na wakati mimi ndiyo muathirika na kumtetea muhalifu ile hali ilinifanya kutomuamini mtu yeyote kabisa na kupenda kukaa peke yangu tokea nikiwa form 2 na nina uwezo wa kuwa nyumbani nikaa ndani peke yangu na watu wapo .. nikiongea ni kujibu nililouliza na siulizi kama hakuna umuhimu sana .. na hii tabia ipo na inaumiza wengine hasa walio karibu yangu upande wa mwenzangu hawanielewi kabisa no story, no party mpaka nitake mimi ..nipo kwenye kujifunza kuamini watu polepole najua nitapona
 
Me nikiwa likizo naweza enda even a week sijatoka nje ya geti(ndani) hapo ni Kama Nina mzigo Mpya wa series kibao. Ni kuhama tuu here to there.
Hapo hata babe hakumbukwi.
I also do this when I'm off.
About going out me pia naenda. Yaani si kwamba I don't go out naenda Sana.
Ila most of the times napenda kuwa alone and of course with my babe(phone)
 
If you join JF, you wish to communicate with others.

Therefore, you are not a true loner.

True loners do not join JF.

Why woyld a true loner join JF?

Sent from my LGLS992 using JamiiForums mobile app
Thats your own perception nd don force it on the other people...

its not like every jf member is here to communicate or interact with others coz jf is one of the best informational source in Tz so, some people tend to be motivated by only that

Kwanza tupo anonymous humu yaani with fake IDs sasa kama kuna mtu anakuwa hajiassociate hadi mtandaoni ni punguwani...
 
Sio muda wote...kuna wakati najirusha vizuri tu. btw umeadimika, busara zako tumezikosa muda sasa.

Basi una bipolar disorder vinginevyo sijui kwa nini uwe concerned hadi kuuliza kama ni kawaida. Binafsi sijakuelewa maana umesema ulikataa mialiko kwa sababu uliazimia sikukuu hii utakaa nyumbani. Sasa unahisi kuamua kukaa nyumbani badala ya kwenda mialikoni ndo tatizo? Huu si uamuzi mbaya maana miili na akili zetu zinahitaji mapumziko. Cha kujiuliza ni hali hii imekuwa sehemu ya maisha yako na haiba yako siku zote au ilikuja tu baadae? Kama ilikuja baadae ni lini na unafikiri chanzo ni nini? Wewe unaionaje? Unajisikia amani na hali hiyo?

Ukiona au ukidai umeamua au unapenda kukaa peke yako nyumbani halafu ukawa busy na JF na mitandao mingine ya kijamii basi ujue una tatizo. Ina maana hamu ya kuhusiana na kuongea na watu unayo ila kuna kitu kinakufanya usihusiane na watu halisi. Ukifikia hapo jisogeze Muhimbili kwa clinical psychologists msemezane.

Halafu watu wakisema "hata mimi" "uko kama mimi" uichukulie kama taarifa kuwa hauko peke yako na si kuwa si tatizo.
 
Back
Top Bottom