Alshabab walifanikiwa kuondoka

Alshabab walifanikiwa kuondoka

Status
Not open for further replies.
Duh kama ni kweli hali ni mbaya ila hao TBC habar hiyo wameitoa wapi?Sikumbuki kuona mwandishi wa TBc kwenye tukio jingine wale waliokuwa wanashambuliana ni wanajeshi wa kenya wenyewe kwa wenyewe au ndo mambo ya teknolojia al shabab waliwazidi maarifa?

hata tv ya citizen ya kenya wametoa hiyo habari na waneuonesha huo mtaro ni mrefu sana na wale alshabab wote walitoroka kupitia hapo ktk maiti zote walizotoa hakuna maiti ya mtekaji hata mmoja wote walitoroka.jeshi la kenya limeonyesha udhaifu mkubwa sana
 
Kilichotokea pale mall ni kama kilichotokea katika movie ya Denzel "INSIDE MAN". Hata CNN jana usiku walisema kuhusu kutoroka kwa baadhi ya hao wasomali. Inavyosemekana wengine walitoroka kwa kujichanganya na wananchi waliokuwa wakiokolewa
 
Kwa masikitiko na sintoelewa kwa nini "'truth (ukweli) ni jambo la kwaza kupotea katika hali kama hii" ??? Uongo na contradiction ndio unatawala mtandao wa habari(media) na uhakika/ukweli haumfikii raia wa kawaida au wananchi wenye ndugu zao katika matokeo ya athari? Watu wengi hawana hatia kwa nini wasijulishwe juu ya hatma ya jamaa zao, ili waanza kuchukua taratibu za maziishi na kuomboleza !!
 
vijana watz tuwe makini na hizi fukuto la kidini, huo ni uchuro kabisa. AL SHABAAB HAWAKO MBALI NAZI KAMA TUKI CHEZA MAKIKDA MAKIDA
 
Daah jamaa kweli walichomoka baadhi citizen news wameonyesha mtaro live bila chenga kdf wameustukia j4 this week those people were not mere terrorist,it is beyond what we can imagine, poleni sana wahanga wa tukio.
 
we ndio kilaza maana unafuata taarifa za vijiweni, lakini taarifa kutoka serikali ya Kenya, zinasema hakuna mjinga yeyote wa kiislamu aliyetoka baada ya majeshi ya kenya kuzingira westgate! tunapinga ugaidi kwa nguvu zote!

Hakuna asiyepinga ugaidi na wala sifikirii kama kuna binaadamu mwenye akili timamu aliyefurahia yaliyotokea Westgate. Ila kichwa chako kimejaa mavi na chuki dhidi ya Uislam.
 
serikali ya Kenya inajaribu kuficha hiyo aibu , ila wamefeli sana kuendesha huo uokoaji
 
Ndio habari inayowaumiza vichwa wana usalama wa Kenya wakisaidiwa na wale wa kutoka Nje ni kwamba baada ya kufanya lile tukio la Westgate jamaa walifanikiwa kuondoka salama salmin kwa kupitia mtaro wa maji taka ambao umeambaa mita kadhaa kutoka lilipo jengo walimofanya tukio la kufuru

Source"tbc habari sa2
1. Hili linawezekana kabisa kuwa wale jamaa walitoroka,kwani tumeshuhudia Katika mpambano ule Kenya iliingiza vikosi vingi vya Usalama ambavyo sidhani kama walikuwa wanatambuana kwani kulikuwa na Polisi, Jeshi, Raia wa kawaida wenye Silaha na inawezekana na watu wa usalama wa Taifa sasa kwa mchanganyiko huu kweli unaweza kupambana? maana pale kulitakiwa kuwe na kiongozi anayetoa amri kitu ambacho nafikiri hakikuwepo ilikuwa ni shaghalabagala. na wale jamaa waliacha wametega mabomu yaliyolipua kabisa lile jengo.

2. Kitu kingine ukitaka kujua Wakenya ni wapumbavu kwenye upande wa utoaji wa Taarifa kwani siku ya tukio kufikia saa 12 jioni walisema waliokufa ni 39 ilipofika saa 5 wakasema 62 huku Red Cross wakisema ni 69, Mpambano ukaendelea kwa siku tatu lakini vifo vya raia idadi imebaki hiyo hiyo ongezeko ni wale Askari 6 na magaidi 5. Je kuna ukweli hapa?

Kenya westgate lilivyobomoka.jpg

kenya westgate 4.jpg

Hali kama hii halafu kusiwe na ongezeko la vifo.
 
Jee, mnajuwa Insurance ya hilo jumba la maduka ni kiasi gani?
 
Jee, mnajuwa Insurance ya hilo jumba la maduka ni kiasi gani?
Insurance haikavi Terrorism... Hata riot and Strike vile vile Pole imekula kwao wajue... Burglary sawa na Natural Disaster ina cover
Wakenya wanajua sana umuhimu wa Insurance na kwa hilo wanalifahamu kwenye Policy ya Insurance lipo wazi....

Hata hapa kama Gari lako likivamiwa na waandamanaji likachomwa moto au likavunjwa vunjwa Insurance hailipi kitu.

Mwenye Jengo ataifungulia kesi Serikali kwa kulilipua jengo lake.... Tatizo ni la Waisrael so wanaweza Jenga wao wenyewe tena
 
warrant ya kumsaka white widow imetoka anatafutwa na kwa udi na uvumba
ikumbukwe ndio alikuwa leader wa wale majamaa

BBC kama uliangalia jumamosi kuna Mzungu alikuwa anasema alimuona mwarabu akiua watu then akabadilisha nguo na kutoka kama mateka

hao ni watu ambao waliowaona ni wangapi wametoka kama mateka bila ya kuonekana?

serikali imesema kuwa magaidi waliouawa ni 8 ila mashahidi wanakwambia ni zaidi ya watu 15 waliovamia wengine walikuwa kwenye parking juu wengine chini wengine ndani ya nakurmatt

propaganda zipo katika mambo kama haya lakini tunatupia logic katika kupambanua mambo kama haya mwisho kabisa mkuu

kuhusu kwa post ambayo uliyoitoa

porojo baada ya Mauaji, wale wajahedeen waliuwawa wote, hakuna mjinga wa kiislamu aliyetoka kule

ungeweza kuandika mjinga wa al shabab kulikuwa hakuna haja ya kuweka neno "Kiislamu" sio ustaarabu, sio burasa na wala sio uungwana
sawa wameua lakini hatuna mamlaka ya kuhukumu ila kama dini yako unayoiamini inakuruhusu kuhukumu badala ya kumuachia Muumba wako kuhukumu pia ni juu yako

ila ningekuwa wewe ningefumba macho then kwa dini yako nikamuomba mungu wangu msamaha

unaweza fanya hivyo hautapungukiwa na chochote ila utapata baraka tu

Muwache aongee na Wananchi hao jamaa wanajiita waislam na wanafanya Ujinga so Kuwaita wajinga ni Haki ya Msemaji kwa Wananchi.... Usimkataze wala Kumfundisha au Umeona sawa hao jamaa kufanya hicho kitendo kilicholaaniwa hadi na Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina akisema huo Uislam wao ni wa aina yao na yeye hafuati mfumo wao wa hao magaidi... ni wajinga.... usitetee kilicholaaniwa na jamii yote
 
Insurance haikavi Terrorism... Hata riot and Strike vile vile Pole imekula kwao wajue... Burglary sawa na Natural Disaster ina cover
Wakenya wanajua sana umuhimu wa Insurance na kwa hilo wanalifahamu kwenye Policy ya Insurance lipo wazi....

Hata hapa kama Gari lako likivamiwa na waandamanaji likachomwa moto au likavunjwa vunjwa Insurance hailipi kitu.

Mwenye Jengo ataifungulia kesi Serikali kwa kulilipua jengo lake.... Tatizo ni la Waisrael so wanaweza Jenga wao wenyewe tena

Mkuu uko dunia ya wapi?

walikata bima kwa kampuni ya uingereza na kuna uwezekano wakalipwa
billion 6.6 ksh
 
Muwache aongee na Wananchi hao jamaa wanajiita waislam na wanafanya Ujinga so Kuwaita wajinga ni Haki ya Msemaji kwa Wananchi.... Usimkataze wala Kumfundisha au Umeona sawa hao jamaa kufanya hicho kitendo kilicholaaniwa hadi na Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina akisema huo Uislam wao ni wa aina yao na yeye hafuati mfumo wao wa hao magaidi... ni wajinga.... usitetee kilicholaaniwa na jamii yote

sijateta chochote hapa ila mie nimesema tu sio uungwana wala ustaarabu kutumia neno "wajinga wa kiislamu"ni neno linaloonekana linalochochea na kuleta matabaka hili huwezi kuiona kama ukiwa hujakaa muda mrefu darasani

na ni kweli sikatai kitu walichokifanya ni cha kijinga lakini huwezi kuweka dini yao mbele kwani kila mtu duniani anafanya maovu wao sio watu wa kwanza kuua
wangapi wanaua watu wasio na hatia? polisi hawauwi watu wasio na hatia tukianzia hapa Tanzania?

tena polisi wa kikristo je tuwaaite Wajinga wa Kikristo?

hakuna majambazi yanayovamia watu na kuua ovyo wakiwa ni wakristo

je tuwaite "wapumbavu wa kikristo?"

tukinzingatia Tunu zetu saba sie watanzania hatuwezi kufika kugawanyika hivyo

so nasisitiza kusema sio uungwana, sio uustarabu, sio hekima, kuwaita wenzako "wajinga wa kiislamu"

unless wewe uwe una matatizo upstairs
 
Mkuu humu watu wengi hawafikiri kabisa na kama wanafikiri sina uhakika kama wanatumia ubongo,kwani kulikuwa na majibizano ya risasi na mateka walikuwa wakishikiliwa ndani,sasa mtu unawezaji kufikiri tu eti walitoka wote?Baadhi wangeweza kutoka na raia lakini si wote.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Hapo ndo panakuwepo na utata, Kenya ilisema kuna magaidi kadhaa wamewaua. Cha ajabu dunia hakuthibitishwa na mwili angalau mmoja wa magaidi.
 
Mkuu humu watu wengi hawafikiri kabisa na kama wanafikiri sina uhakika kama wanatumia ubongo,kwani kulikuwa na majibizano ya risasi na mateka walikuwa wakishikiliwa ndani,sasa mtu unawezaji kufikiri tu eti walitoka wote?Baadhi wangeweza kutoka na raia lakini si wote.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

labda magaidi waliishikisha bunduki midoli ya ndani ya mall ikawa inapambana na askari wa kenya. hahahahaha..............
 
we ndio kilaza maana unafuata taarifa za vijiweni, lakini taarifa kutoka serikali ya Kenya, zinasema hakuna mjinga yeyote wa kiislamu aliyetoka baada ya majeshi ya kenya kuzingira westgate! tunapinga ugaidi kwa nguvu zote!

yuko raia aliyethibitisha kuwa alimuona gaidi mmoja anabadili nguo na pia yeye alitoka kama mateka akatokomea nadhani hii clip umeiona KTN. Sasa huyo ni mmoja tu, je unajua ni wangapi walitoroka kwa mtindo huo? Na wale waliokamatiwa airport na michoro ya westgate?
 
hata tv ya citizen ya kenya wametoa hiyo habari na waneuonesha huo mtaro ni mrefu sana na wale alshabab wote walitoroka kupitia hapo ktk maiti zote walizotoa hakuna maiti ya mtekaji hata mmoja wote walitoroka.jeshi la kenya limeonyesha udhaifu mkubwa sana

mimi nilikuwa nawaambia watu hawa magaidi watakuwa wameturoka kupitia kwenye mitaro ya maji machafu, kweli kenya hakuna jeshi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom