Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,511
- 8,147
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Ally Hapi amewataka Wanaume kuacha kutelekeza Watoto huku akiwasisitiza Vijana kuoa .
Hapi amesema hayo akiwa Mkoani Singida May 10,2024 ambapo amesema “Nataka tuone mkakati kweli tuna tatizo kubwa la Watoto wa Mitaani na sio Singida tu ni kote Nchini, Vijana tumekuwa Mabingwa wa kufanya yale mambo, Watoto wakipatikana unajifanya upo bize hutaki kulea, meseji yangu kwa Wababa na Vijana hakuna jambo baya kama kutelekeza damu yako, mbaya sana, kuzalisha Mwanamke ukamtelekeza Mtoto ni mbaya sana”
“Wakina Baba tutunze Watoto, kila anayejua ana Mtoto wake amemtelekeza sehemu tukitoka hapa mtafute Mtoto wako mtunze usitelekeze damu yako, Mwanaume imara na shupavu hatelekezi Watoto, wewe ukiona unatelekeza Watoto ni Mwanaume suruali, baadaye Watoto wakifanikiwa mnaanza ooh tuyamalize”
“La pili Vijana tuoe, Vijana sasa hivi tunaogopa kuoa, Wakina Mama na Wadada ni wengi kuliko sisi wewe unakaa gheto unajipilikisha, ushajua kukanda maandazi na chapati, unakaanga mpaka rosti kwanini huoi?”