Hizi ni sababu kuntu (muhimu) zinazowafanya baadhi ya wanaume/vijana kukataa kuoa

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,741
Nimefanya uchunguzi mdogo(simple research) hapa kitaa ninapoishi na maeneo tofauti tofauti pamoja na kwenye social network, nikagundua sababu kuu muhimu zinazofanya baadhi ya wanaume kukataa kuoa.
Najua Kuna kikundi Cha wahuni kipo humu jamii forum kitakuja kupinga hiki ninacho kizungumza hapa.
Moderaters naomba msifute uzi huu Kama mlivyofuta ule uzi nikielezea tofauti ya mtu aliyeoa na anayenunua totoz.

(1) Jobless (ukosefu wa ajira/kazi) vijana wengi hawana kazi au shughuli maalumu ya kuingiza kipato, kijana Kama huyu ukimwambia oa wakati tumbo lake tu kula ni shida hata bando ni lakuunga unga ni ngumu sana kijana/mwanaume wa Kariba hii kuoa.

(2) Uchoyo/ubinafsi Kuna vijana/wanaume wanapenda maisha ya peke yao, kukaa peke yake anaona akioa atabanwa sana au bajeti zake/uchumi wake utayumba na wanaume wa namna hii akizalisha nje huko huwa anachukua mtoto anapeleka kwa bibi yake ili abaki peke yake tu kutokana na roho ya uchoyo aliyonayo.

(3) Kuendekeza starehe/zinaa na uasherati hapa Kuna kundi kubwa la vijana/wanaume wanaona watakapooa watabanwa starehe na Mambo yao yakulala club na kununua wanawake wapya tinder, badoo na telegram utagonga mwamba na ndipo wanaona wabaki kuwa single.

(4) Matatizo ya kibinadamu (hanithi) Kama ilivyo binadamu tuna mapungufu magonjwa/ matatizo Kama haya pia husababisha vijana/wanaume wenye tatizo Kama hili wasifikirie kabisa suala la kuoa.

(5) Kuningiliwa kinyume na maumbile (ushoga) hakuna kijana wa kiume/mwanaume anaweza kufikiria kufunga ndoa na kuwa na mpenzi wake Kama ni muumini wa kuingiliwa kinyume na maumbile(shoga) hakuna kitu Kama hicho.

(6) Matukio/hadithi za kutisha zinazotokea kwa walio kwenye ndoa
Matukio yanayotokea Kama mauaji,fumanizi ,dhurma baina ya mwanamke na mwanaume katika ndoa, hii huwatisha vijana/wanaume wanaotaka kuoa wanaposikia mtu fulani kazulumiwa na mke wake/mume wake.
Mfano mdogo kilichotokea kwa mchezaji wa mpira wa miguu ashraf hakimi dhidi ya mke wake.

(8) Kuiga kutoka kwa watu maarufu duniani Kama vile wacheza mpira wa miguu, wasanii wa nyimbo na nk.
Kuna vijana/wanaume hawaoi kwa sababu tu ya baadhi ya watu Maarufu hawajaoa. Mfano Christian Ronaldo kazaa na mpenzi wake watoto si chini ya watatu lakini hayupo kwenye ndoa, unakuta kijana/mwanaume wa kitanzania naye anamuiga CR7.

Hizo ni sababu kuntu (muhimu) ambazo NALIA NGWENA kipenzi Cha watoto wazuri wa jamii forum nimeona nizilete hapa baada yakufanya uchunguzi wangu mdogo(simple research).

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mbona hawajatoa sababu ya kuachana.
Screenshot_20230422-071920.jpg


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom