Kaka unaongea kwa busara sana. Lakini naomba kukuuliza swali moja tu. Waliowahi kutumbuliwa wote tangu utawala huu uanze hawakuwa na mazuri waliyowahi kufanya? Ukipata jawabu jitafakari na unachotetea hapa.
Ahsante! Tunapomlaumu mtu ama kumtuhumu kwa hatua aliyo chukua ama aliyo taka kuichukua kwa kukiuka mipaka yake ki uongozi ni vema tukaangalia chimbuko la kitendo hicho ama maamuzi hayo lilikuwa nini.
Mfano, ukitembelea katika taasisi nyingi za serikali kuna ubwanyenye ulio kithiri na watendaji hawa wa serikali ambao ni kero kwa wananchi. Na wao sabbu wanajua kuwa hawawezi kufanywa jambo lolote kuathiri ajira zao mpaka taratibu fulani zifuatwe wanapata jeuri na kiburi kisicho weza kustamiliwa.!
Je umewahi peleka mgonjwa kwenye hosptali ya serikali..ukaona kero wanazo kutana nao wananchi wa kipato cha chini?
Kuna wakati niliwahi kaa kwenye benchi kwa zaidi ya masaa mawili nasubiri kuonana na daktari
Kumbe Dr yupo ndani anachagua bidhaa za kununua kutoka kwa shoga yake.!
Mpaka alipomaliza ndo unaingia kutibiwa ama kuandikiwa dawa, katika mazingira ya kama haya unategemea mkuu wa mkoa achukue hatua zipi.? Anapolalamikiwa na wananchi?
Kumbuka yeye ndie kiongozi mkuu wa Mkoa kwa wakati huo na watumishi wote wa serikali wako chini yake.!
Endapo Mganga mkuu wa mkoa hana jeur ya kuwawajibisha walio chini yake kwa sabbu zozote zile unataraji mkuu wa mkoa afanye nini? Kwa hatua za mwanzo? Sio kutoa onyo na kalipio la kimamlaka?
Ni vema tuwe wakweli wakati fulani japo nyuma ya hoja zetu tuna ajenda binafsi za kisiasa.!
Kwa wale ambao hatutegemea huduma za kijamii.
Mfano Shule, hosptali sio rahisi sana kuona hizo kero.