Ally Hapi, Anguko lako kisiasa umelitengeneza mwenyewe!

Ally Hapi, Anguko lako kisiasa umelitengeneza mwenyewe!

Masikini alafu yule Dokta, alikuwa kainamisha kichwa chini, na pale alipokuwa akionywa anamuangalia kwa sura ya kutaka huruma ya kutoendelea kushalilishwa kwenye public..

Jaman Mungu na mm anipe unyenyekevu na subira kama alichokifanya yule dk

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Anasema nilikuwa nakutafuta sana wewe....sasa umeingia kwenye 18 zangu....
 
Wanaudhi. Kuna mawili. Kuwafanyia kama alivyofanya Jaffo ili wajifunze. AU kuhakikisha wako nyuma ya mzoefu. Kuwatimua sio jema. Mkuu wa mkoa wa Dodoma awasimamie wa Iringa na mbeya. Wa Morogoro asimamie wa Dar nk. Wanapoelekea kustaafu "wanafunzi" watakuwa wamefuzu.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Mimi kuna kitu naomba mnifafanulie mnaofaham, wakuu wa mikoa hua wanareport kwa nani? i mean majukum ya kazi zao na Je waziri wa TAMISEMI hana mamlaka ya kumwajibisha Mkuu wa Mkoa!
 
Hata methali za kawaida kabisa zinatufundisha kuwa tuwe na kiasi,ukiwa mtu wa kiburi,kulewa sifa kwa kujiona u mtu bora kuliko wengine mwishoni ni kujikuta uko shimoni na wakukutoa humo hayupo,wote ulishawadharau nao wamejiweka mbali na wewe,"analo hilo"
 
Tunafanya makosa sana kuwapa vijana( 25-30) years majukumu ya kimaamuzi.
Ni busara tuanze kuwaandaa kidogo kidogo kwa kusimamia idadi ndogo ya watu kwanza( supervision)
Changamoto atakazopata kwa idadi ndogo haitakuwa na athari kubwa wakati huo mabosi Wa juu yake watasawazisha makosa na atajifunza zaidi.
Angalia mtu kama Mongella,Mtaka, Kebwe,Hamsini, Magoiga, hawana scandal za uongozi.
Mtaka is the best RC kwanza anapenda watumishi wa umma na yuko tayari kujifunza
 
Sio mara ya kwanza Jaffi kusema hivyo!Hawa vijana vijana wanalewa madaraka!Mpaka sasa vijana wote walio katika uteuzi wa kisiasa serikalini wamefeli!
Hawana hekima ya kufanya kazi na wengine?
 
Ndio maana tunasema utaratibu wa kisheria ufuatwe kuwawajibisha!
RC ni M/kiti wa usalama wa Mkoa. Anaona kuna vitendo vinahatarisha amani, huwajibika kuchukua hatua.

Niliangalia "video clip" ya sakata la Daktari huyo bingwa, RC alimtumbua, wananchi walishangilia sana. Kinachofuata na mamlaka husika kuchukua hatua za kinidhamu au sheria.

HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA.
 
Sio mara ya kwanza Jaffi kusema hivyo!Hawa vijana vijana wanalewa madaraka!Mpaka sasa vijana wote walio katika uteuzi wa kisiasa serikalini wamefeli!

Siyo wote waliofeli, ila wengi wao kwa kweli wamefeli ....tatizo ni kuwa hawa vijana hawajui A B C za uongozi na wengi wao wametumbukizwa tu kwenye uongozi
 
mkuu ngoja nichukue nafasi hii kukuelewesha kidogo.

1. MH. Harpy Eagle alimkaripia Dr. bingwa mbele ya hadhara na kusema hamtaki tena ndani ya mkoa wake, pili alisema alikuwa anamtafuta muda mrefu so siku hiyo bahati nzuri dr. bingwa akawa ameingia kwenye 18 za harpy

maneno kama haya kwa nchi tunazoishi wengine yanatosha kabisa kumfanya Harpy ajihudhuru nyazifa zake, hii ni personal attack na amekitumia cheo cha RC kama dhamana binafsi. Ilitakiwa kufuata taratibu za kisheria. Huwezi kumwambia mtumishi wa uma ulikuwa unamtafuta muda mrefu, that means mudawote huu hukuweza kumpa maelekezo ajirekebishe ilimuende sawa.

2. MH. Harpy Eagle alisikitishwa na kitendo cha baadhi ya watoto na wazee kulipishwa wakati sera inataka watibiwe bure na hii kupelekea RC kucharuka na kumvunjia heshima Dr. mbele ya hadhara.

Hapa kuna kosa kubwa sana mh. rc kalifanya either makusudi kutafuta kick au hakujua. Referral hospital zote ukienda kutibiwa kama self (home) referral bila kupitia hospital za awari unatakiwa uchangie (coast sharing). Dr. alikuwa sahihi sema hakuweza kujitetea vyema. Nadhani kuna umuhimu wa kuheshimu taaluma na kuacha kuleta siasa katika maswala nyeti kama haya. Hospital zetu zina upungufu mkubwa sana wa budget ya kuziendeshea katika kutoa huduma bora.
Juzi hapa Zito kasema kuwa budget iliyopangwa ya wizara ya afya kwa ajili ya huduma za afya kupitia bunge fedha hizo zilipelekwa hata nusu ya budget haikufikia kiwango kilicho pitishwa.
Kwakipindi kilefu sana budget yatue inasaidiwa na donor, 2017/2018 budget hii 26% ni donor na 74% ndo serekali inatoa fedha hizo.

Tumekuwa tunawaaminisha watu watatibiwa bure huku pesa ya budget haitoshi, siasa nikitu cha hovyo sana

Analysis of the Government of Tanzania’s Budget Allocation to the Health Sector for Fiscal Year 2017/18 POLICY Brief January 2018
View attachment 913401
View attachment 913402
View attachment 913403
View attachment 913404
cost sharing ni mpaka kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano mkuu? dah hebu review upya sera za afya sio tanzania tu duniani kwa public hospital kwa sasa
 
Ungesoma na kuelewa kwanza
sawa mkuu taaluma ni muhimu kuliko kuhudumia wagonjwa tena watoto maskini kabisa ubarikiwe sana ipo siku utamwaga chozi wodini mtumishi wa umma mwenye joho jeupe anamalizia kupost selfie kwanza ndo utaelewa 😀
 
Hakuna asie wajibishwa Nchi hii ,hapa tuna lalamikia Utaratibu ulio tumika kumuwajibisha huyo Daktari.Haukuwa sahihi na ndio Sababu Waziri amesema atawaelekeza hao Jamaa Mipaka ya Majukumu yao.
si atahamia mkoa mwingine tu mkuu na kubaki na ubingwa wake na kuwachage watoto wadogo wa mkoa husika fees kama kawa shida ipo wapi
 
Back
Top Bottom