Aliyetupa Macho asiweze kuona?

Mkuu unakipenda chadema kweli, yaani mwenyekiti alipata zero form 6 unataka na katibu wake awe mtu wa elimu ya hapa na pale??
nani atakayemuongoza mwenzake......umewahi kipofu anamuongoza kipofu mwenzie?!

Kama wewe ni msomi kuliko Lema na Mbowe basi ni majanga kabisa kama siyo ubashite, maana hotuba za Mbowe na hata jinsi ambavyo Lema amawasilisha mada yake, havilingani kabisa na uwasilishaji wako.

Bila shaka wewe hutofautianai na Daudi Albert Bashite.
 
ok...na ya CHADEMA ni ipi? Viwanda si umeona cha dangote na bahresa vinavyopiga kazi? na dangote anajenga kingine cha makaa ya mawe

Wale Chadema umeshamaliza wewe hapo juu kwamba hawana dira na hawajitambui, sasa unataka nini zaidi tena Mkuu???
 
Basi kama huyo Rais wako alikuwa anategemea wananchi ndio tutajenga viwanda atasubiri sana.na wewe endelea kusubiri sisi wananchi tujenge viwanda.kenge wewe huna akili hata moja
Mh mkuu wa nchi yeye kuandaa "paratable & favourable conditions interms of socio,political, economocal dvp for the proper dvp of our industries" wala si vinginevyo mkuu.
 

Mhe. Godbless Lema, kwanza nikupe pole sana kwa kifungo cha miezi 4 bila hatia wala mashtaka. Pole sana.
Hii ndiyo Tanzania ya Magufuli, ni vurugu, ni unyama, ni udikteta, ni uhuni na ubabe uliopitiliza. Haya matukio ni mageni sana masikioni mwa watu wa Tanzania. Sielewi huyu Rais wa CCM A5 anataka Watanzania wafanye nini kwa haya mambo ya ajabu ajabu anayowafanyia Watanzania wenzake kana kwamba ni Makaburu!!

Nelson Mandela(RIP) pamoja na kufungwa na MAKABURU miaka 27 gerezani bado alikuja kuwa Rais wa SA na AKAWASAMEHE MAKABURU WOTE!!. Bado Nelson Mandela alipoanza kutawala nchi ya Afrika Kusini ALIWEZA KUWAACHIA IKULU CHAMA CHA UPINZANI KUKAIMU AKIWA ZIARANI NCHI ZA NJE!!! Je, Magufuli anaweza kufika hata 0.00001% ya UTU na UUNGWANA aliokuwa nao Marehemu Mandela???

Tanzania inapitia kipindi kigumu sana katika Historia tangu kuundwa kwake. Bahati ni kwamba Watz hawakupitia misukosuko ya vita vya kupigania Uhuru ndiyo maana hawana fujo za kijinga kutaka kujibu mapigo. Lakini Rais Magufuli lazima ajue kuwa ameshaanza kubadilisha mwelekeo na upepo kwa Watanzania. Asifikiri Watanzania ni Malaika walioshushwa kutoka Mbinguni. Watz nao ni wanadamu kama wanadamu wengine kama wa nchi za Rwanda, Burundi, Algeria, Misri, Libya, Yugoslavia n.k.
Kuna kitu Rais Magufuli anachokitafuta kwa Watanzania na iko siku inakuja atakipata. Naomba JPM ayakumbuke maneno ya Baba wa Taifa aliyoyatumia wakti wa kumng'oa mkolone bila kutumia bunduki yanayosema,'' TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA,TUMENYONYWA KIASI CHA KUTOSHA. UNYONGE WETU NDIO ULIOTUFANYA TUONEWE, TUNYONYWE NA TUPUUZWE, SASA TUNASEMA BASI ''

Magufuli ameamua kuchezea HAKI, UTU na HESHIMA za Watanzania kwa kuamua KUWAONEA, KUWAPUUZA, KUWANYONYA na KUWANYANYASA kisa tu eti wapinzani. Kwanini Magufuli ameamua kuwafanya WATANZANIA WAISHI KAMA WAKIMBIZI NDANI YA NCHI YAO????Hii ni akili ya ajabu sana kuwahi kufanywa na mtu anayejiita Rais wa JMT. Sijajua kwa akili ya Magufuli kama Wapinzani ni maadui,wahaini au magaidi wanaotaka kupindua nchi!! Nchi hii ni ya Watanzania wote bila kujali wako chama gani, wana itikadi gani, wana dini gani, wana Elimu gani au wanatoka kabila gani. Lakini kwa Utawala huu rangi zote za Ubaguzi na Ukabila zimeanza kuonekana waziwazi. Ubaguzi wa kiitikadi/kichama uko wazi(rejea speech zake kwenye Mkutano Mkuu wa CCM juzi na alipoongea na Wabunge wa CCM.Ukija kwenye Ukabila usiseme, kwa sasa kila akitumbua mtu anayemteua ni Msukuma mwenzie. Angalia swala la RC Makonda, pamoja na USHAHIDI WA WATU WA MUNGU KUWA HUYU ALIGHUSHI VYETI MAGUFULI YUKO KIMYA anajifanya kama vile haoni au hayupo. This is double standard. Inasikitisha sana. Nimalize kwa kusema tu kwamba haya yote anayotufanyia Watanzania wawe Wapinzani, wawe Wanachuo waliokosa mikopo, Wafanyakazi ambao hawajapata madai yao kama WAALIMU na MADAKTARI, Watani zangu WAHAYA na TETEMEKO LA ARDHI, Mungu wa Mbinguni anaona huu UTAWALA MWOVU NA IKO SIKU ATAUPATILIZA KATIKA JINA LA YESU KRISTO.

Mwisho ni kuwa Wana CCM tunashauri mwambieni Mwenyekiti wenu na Rais wenu kuwa VISASI HAVIJENGI VIWANDA wala UMOJA WA KITAIFA. Anachofanya kwa sasa ni KUBOMOA NCHI NA KUSAMBARATISHA UMOJA,AMANI, MSHIKAMANO NA UPENDO TULIACHIWA NA WAASISI WA TAIFA HILI. Shame on him!!!
 
Siku ukibaki peke yako ndio utaelewa maana kwa sasa bado unajifariji...
 
Kamanda hongera, busara kama hizi ulizonazo ni hazina kwa taifa.
Kamanda hata mimi sipendi kushuhudia udhalimu wa watawala nataka nifungue kesi ya kikatiba mahakamani siku moja ila sijapata mawakili tu.
Godbless J Lema
 
Kamanda nitafurahi siku moja nikikusikia ukiongea kwa undani kilichompata kamanda Ben Saanane..Tafadhali Lema fuatilia hili tumebaki kwenye giza nene,watu hatujui huyu kamanda yupo wapi..tusaidie katika hili kamanda..
 
Wakati mwingine unaweza kumsoma mtu ukashangaa mwenyewe. Mbunge ambaye ndiye mtungaji wa Sheria anaandika vitu kiushabiki kiasi hiki?

Mtu anatengeneza mazingira ili kupata huruma za watu.. huu ni Ujinga kufanywa na Mtu mfano wa Lissu. Kampeni za kipuuzi mfano huu zinakushusha. (Ingawa siuoni huo uimara wako).

HAKUNA DHAMBI MBAYA KAMA KUMSHIRIKISHA MUNGU KWENYE UONGO
 
Zoezi la kutumbukiza karatasi likifanyika kwa haki 2020 matokeo ni aibu kwa fulani! Hata huko kwenye nyumba ndogo hata ikipigwa ndiyo na hapana bado ni aibu!
Kuficha aibu kwenye nyumba ndogo ni kufanya figisu ili asipingwe, hilo limefanyika, Ikitegemewa kuwa kwenye nyumba kubwa rafu za February Zitaokoa jahazi!
 
Amevunja sheria ipi tuambie wengine hatujui mkuu
 
Wewe akili yako bado haijakaa sawa. Tuliza kichwa kwanza bwana mdogo.
 
Which is which?-TL ni mjinga au anafanya makusudi? Nafasi yake katika kesi ya Dodoma ni ipi na nafasi ya wakili wake kwenye kesi yake Dar ni ipi? Nauliza haya maswali kwa kuwa umemega kipande kidogo cha hoja nzima ya Lema ukaona alichokiandika hakina maana kwa kuwa TL ni mjinga au anafanya makusudi......Hoja niliyokuwa nazungumzia ni mantiki ya kilichoandikwa na Lema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…