Aliyeteuliwa kuwa Waziri wa michezo Dkt. Damas Ndumbaro aliwahi kufungiwa miaka 7 kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi na TFF kwa kukiuka kanuni

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,606
17,784
Kwanza Kabisa natoa Shukrani kwa Rais Dkt Samia Hassan Suluhu Kufanya ReShuffling ya Mawaziri mbalimbali amefanya kitu ambacho Tanzania wengi walikuwa wanahitaji.

Moja ya Watu walioguswa na hii Reshuffling yumo Mheshimiwa Dr Damas Ndumbaro.

Tujikumbushe Mwaka 2014 akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba na mjumbe wa Bodi ya Ligi ya Tanzania..,Alikula chuma cha kufungiwa Miaka saba kwa kukiuka Kanuni na sheria za TFF....

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilimfungia kwa miaka saba, Dk Damas Ndumbaro kujihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa kukutwa na makosa mawili.

Kosa la kwanza Lilikuwa kutoa taarifa zisizo sahihi kiasi cha kupotosha maamuzi ya TFF kinyume cha kanuni nambari 41 kifungu kidogo cha sita cha kanuni za Ligi toleo la mwaka 2014.

Akiwa kama Wakili pia alifungiwa miaka saba kwa kosa la pili, ambalo lilikuwa ni kushawishi au kupotosha na kuzuia maamuzi ya TFF kupitia bodi ya Ligi kinyume cha kanuni ya nne kifungu kidogo cha 16 toleo la mwaka 2014.

Wakili Ndumbaro (enzi hizo) a akiwa mwanafamilia wa TFF kwa vyeo vyake vya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba na Mjumbe wa Bodi ya Ligi, alikubali kuziwakilisha klabu dhidi ya TFF.
Ambavyo anajua kufanya hivyo ni makosa kwa sababu yeye alikuwa ndani ya TFF na maana yake anajua siri za shirikisho, kwa hivyo alichotakiwa ni kukataa.

huyu huyu Ndumbaro aliyekula chuma Na TFF Kwa kufungiwa Miaka 7 leo ndo Boss wa TFF...

Hii naifananisha na nyimbo ya Alikiba Kuwa sisi kama Pipo Tutakutana Na sisi Kama pipo zitaumanaa...Siku zote usikate Tamaa mpaka uwe Boss wa Wabaya Wako

KARIBU TFF DR DAMAS NDUMBARO (WSNM)
 
Kwanza Kabisa natoa Shukrani kwa Rais Dkt Samia Hassan Suluhu Kufanya ReShuffling ya Mawaziri mbalimbali amefanya kitu ambacho Tanzania wengi walikuwa wanahitaji...
Miaka 7 kutoka 2014, maana yake adhabu yake iliisha mwaka 2021.

Si hilo tu, Unapaswa kujua kuwa TFF haiwajibiki kwa serikali. Ni taasisi inayojitegemea kimaamuzi pasipokuingiliwa na serikali.

Sioni mantiki ya uzi huu..
 
Kwanza Kabisa natoa Shukrani kwa Rais Dkt Samia Hassan Suluhu Kufanya ReShuffling ya Mawaziri mbalimbali amefanya kitu ambacho Tanzania wengi walikuwa wanahitaji.....
Miaka 7 aliyofungiwa ilifika ukomo mwaka 2021, kwa hiyo adhabu iko irrelevant.

Pili wale wababaishaji waliomfungia kujishirikisha na muchezo wenyewe walikuja kufungwa na Magufuli kwa uhujumu uchumi na wakatumikia kufungo. Kuna Jamal Malinzi na Mwesigwa.

Piga kazi Damas Ndumbaro
 
Miaka 7 kutoka 2014, maana yake adhabu yake iliisha mwaka 2021.

Si hilo tu, Unapaswa kujua kuwa TFF haiwajibiki kwa serikali. Ni taasisi inayojitegemea kimaamuzi pasipokuingiliwa na serikali.

Sioni mantiki ya uzi huu..
Haiwajibiki wa serikali ila iko chini Ya wizara ya Sanaa na Michezo
 
Kwanza Kabisa natoa Shukrani kwa Rais Dkt Samia Hassan Suluhu Kufanya ReShuffling ya Mawaziri mbalimbali amefanya kitu ambacho Tanzania wengi walikuwa wanahitaji...

Moja ya Watu walioguswa na hii Reshuffling yumo Mheshimiwa Dr Damas Ndumbaro...

Tujikumbushe Mwaka 2014 akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba na mjumbe wa Bodi ya Ligi ya Tanzania..,Alikula chuma cha kufungiwa Miaka saba kwa kukiuka Kanuni na sheria za TFF....

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilimfungia kwa miaka saba, Dk Damas Ndumbaro kujihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa kukutwa na makosa mawili.

Kosa la kwanza Lilikuwa kutoa taarifa zisizo sahihi kiasi cha kupotosha maamuzi ya TFF kinyume cha kanuni nambari 41 kifungu kidogo cha sita cha kanuni za Ligi toleo la mwaka 2014.

Akiwa kama Wakili pia alifungiwa miaka saba kwa kosa la pili, ambalo lilikuwa ni kushawishi au kupotosha na kuzuia maamuzi ya TFF kupitia bodi ya Ligi kinyume cha kanuni ya nne kifungu kidogo cha 16 toleo la mwaka 2014.

Wakili Ndumbaro (enzi hizo) a akiwa mwanafamilia wa TFF kwa vyeo vyake vya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba na Mjumbe wa Bodi ya Ligi, alikubali kuziwakilisha klabu dhidi ya TFF.
Ambavyo anajua kufanya hivyo ni makosa kwa sababu yeye alikuwa ndani ya TFF na maana yake anajua siri za shirikisho, kwa hivyo alichotakiwa ni kukataa.

Pia, Ndumbaro aliupotosha umma kwa kusema klabu 12 zilimuomba kuwawakilisha kupinga makato ya asilimia tano za fedha za udhamini wa Ligi Kuu, wakati klabu nyingine zilikana kuhusika na mpango huo, Coastal Union na Stand United.

huyu huyu Ndumbaro aliyekula chuma Na TFF Kwa kufungiwa Miaka 7 leo ndo Boss wa TFF...

Hii naifananisha na nyimbo ya Alikiba Kuwa sisi kama Pipo Tutakutana Na sisi Kama pipo zitaumanaa...

KARIBU TFF DR DAMAS NDUMBARO (WSNM)
Mungu huyu acha aitwe Mungu...

Nisikilize...

Dr.Ndumbaro "alikaangwa" na watu wa TFF....

#SiempreJMT
 
Kwanza Kabisa natoa Shukrani kwa Rais Dkt Samia Hassan Suluhu Kufanya ReShuffling ya Mawaziri mbalimbali amefanya kitu ambacho Tanzania wengi walikuwa wanahitaji...

Moja ya Watu walioguswa na hii Reshuffling yumo Mheshimiwa Dr Damas Ndumbaro...

Tujikumbushe Mwaka 2014 akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba na mjumbe wa Bodi ya Ligi ya Tanzania..,Alikula chuma cha kufungiwa Miaka saba kwa kukiuka Kanuni na sheria za TFF....

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilimfungia kwa miaka saba, Dk Damas Ndumbaro kujihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa kukutwa na makosa mawili.

Kosa la kwanza Lilikuwa kutoa taarifa zisizo sahihi kiasi cha kupotosha maamuzi ya TFF kinyume cha kanuni nambari 41 kifungu kidogo cha sita cha kanuni za Ligi toleo la mwaka 2014.

Akiwa kama Wakili pia alifungiwa miaka saba kwa kosa la pili, ambalo lilikuwa ni kushawishi au kupotosha na kuzuia maamuzi ya TFF kupitia bodi ya Ligi kinyume cha kanuni ya nne kifungu kidogo cha 16 toleo la mwaka 2014.

Wakili Ndumbaro (enzi hizo) a akiwa mwanafamilia wa TFF kwa vyeo vyake vya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba na Mjumbe wa Bodi ya Ligi, alikubali kuziwakilisha klabu dhidi ya TFF.
Ambavyo anajua kufanya hivyo ni makosa kwa sababu yeye alikuwa ndani ya TFF na maana yake anajua siri za shirikisho, kwa hivyo alichotakiwa ni kukataa.

huyu huyu Ndumbaro aliyekula chuma Na TFF Kwa kufungiwa Miaka 7 leo ndo Boss wa TFF...

Hii naifananisha na nyimbo ya Alikiba Kuwa sisi kama Pipo Tutakutana Na sisi Kama pipo zitaumanaa...Siku zote usikate Tamaa mpaka uwe Boss wa Wabaya Wako

KARIBU TFF DR DAMAS NDUMBARO (WSNM)
 
TFF ni waoga sana Sasa wanachoogopa ni nini Kama walikuwa kwenye Haki si watulie Wanatoa Taarifa yenye Maelezo Mengi mara uongozi uliomfungia Ni uongozi uliopita,,Mara alishinda Rufaa Tulieni Dawa iwaingie

🤣🤣🤣...Mweshimiwa Ndumbaro kazia hapo hapo Usiachie
WhatsApp Image 2023-09-02 at 11.36.03.jpeg
 
Watanzania huwa ni wasahaulifu.

Matatizo yaanzia mbali ila wanajifanya kama mbuni kufukia kichwa chini ya mchanga na mwili ukibaki juu kanakwamba hawajui linaloendelea..
 
Back
Top Bottom