Aliyerekodi Video ya Mwanafunzi kushambuliwa na Walimu

Aliyerekodi Video ya Mwanafunzi kushambuliwa na Walimu

alieachishwa chuo kama ni mwanao utaripokeaje,kumbula kijana alibakiza mda mchache amalize chuo asaidie jamii yake,, hilo suala lingebakia shuleni wangelimaliza kwa taratibu zinzofaa kwa kuangalia pande zote
Subiri mwanao afanyiwe hivyo half uache ulimalize kwa taratibu.
 
kuna watu wana akili za kitoto mpaka unaogopa.

yaani jamaa amekaa akawaza mchukua video ana kesi ya kujibu daaa kweli tunatofautiana kuwaza.

utoto wa hali ya juu kumshushia tuhuma aliye rekodi
 
Kosa jingine...
Kwanini wapewe ofisi yao,? Watajifunza nini sasa?
Sababu za kuwatetea zinazidi kuwa nyingi, pengine hawajui wenyeji huwa wanawaadhibu vipi wanafunzi wao.
Turudi kwa mrekodi video, kama walipewa ofisi yao wenyewe hilo swala mkuu wa shule angelijuaje? Kwanini kama alikuwa ana nia njema aisende kumtaarifu mkuu wa shule kabla ya ku publicity hiyo video,?
mkuu mtoa Uzi hapo juu anajaribu kuwa defend ( kuwatetea hao walim) lakini Mara nyingi sana WALIMU wa vitendo hupewa mandate ya kuwaadhibu wanafunzi ikitokea mamefanya kosa but shida ni moja hapo , shule nyingi hazitoi maelekezo jinsi na tabia za wanafunzi wao kwa WALIMU wa vitendo ,jinsi gani ya kuwa treat ndo hapo unampiga mtoto kama unafanya mafunzo ya ukakamavu

yani kwa tukio hill mtoa mada umekurupuka kuwatetea hao vilaza na WALIMU up to now wapo desperate kwa hill tukio[emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
iwe fundisho maana sasa hv smart noma ukifanya tukio watu wanachukua video mapema kuweni makin watoa rushwa na wapokeaji huku tunako enda balaa
 
Mwalimu wa mwaka huyo pale angeingilia tusingejua na wale wangeendeleza ukatili wao uko kwingine . Mungu ambariki mwalimu paparazi
 
NI UJINGA TU.

Ukisikiliza tukio la Mwanafunzi kupigwa na walimu jinsi linavyojadiliwa utadhani hiyo ni dhambi kubwa Duniani.Kuna matukio mengi ya walimu kudhalilishwa na wanafunzi lakini jamii inaziba maskio.

Tusipokuwa makini itafikia mahali walimu wa shule za serikali wataacha wanafunzi wafanye wanavyotaka. Sina muda wa kutetea hoja yangu ila naomba watanzania mjiulize maswali haya:

1. Je,ni lini ulisikia mwanafunzi wa shule BINAFSI amepiga mwalimu au kufungia mwalimu chooni?

2. Je,kati ya shule za Serikali na BINAFSI ni zipi zinatoa adhabu kali kwa wanafunzi?

3. Je,ni lini ulimuona mzazi mwenye mtoto shule BINAFSI anaenda shuleni kulalamika kuwa mtoto wake ameadhibiwa/Ameonewa?

4. Je, ulishajiuliza ni kwanini wanafunzi wa shule BINAFSI wana nidhamu kuliko wanafunzi wa shule za serikali?

5. Je, ulishajiuliza ni kwanini viongozi wote wanapeleka watoto wao shule za BINAFSI?

6. Je,Unadhani walimu wakiweka fimbo chini kwa kizazi hiki tunajenga taifa gani?

NB: KAMA UNADHANI MWANAFUNZI KUMKABA KOO MWALIMU NI SAWA,JIULIZE PIA WEWE KAMA BABA MTOTO WAKO AKIKUKABA KOO MBELE YA WADOGO ZAKE UTASEMA NI HAKI YAKE?
Hivi kweli fimbo ni solution katika zama hizi .. Why do we have think primitively hivo kuna jinsi ya kuhandle wanafunzi hasa wanabalehe na fimbo sio solution zinduka
 
Atateuliwa hivi karibuni kuwa Mkuu wa wilaya kati ya Moja ya wilaya mpya
 
Tatizo watu hamfuatilii ishu kwa undani, ndio kapigwa sana ila huyu dogo angekuwa nyumbani kwenu pengine angeshakutoa meno yote

Ebhu fikiria kamtukana baba yake mbele ya staff, kashavunja TV ya nyumbani kwao na baba yake hataki hata kumuona kashakamatwa shule ni anavuta bangi hapo yenyewe aliwapiga walimu watatu ngumi za hatari ila baadae wanafanikiwa kumdhibiti na zile ni hasira tu pengine ingekuwa ww ungempiga zaidi ama kumvunja mahali

Hlf tukumbuke wale walimu wapo mafunzoni na wapo chini ya uangalizi wa walimu wazoefu na chuo hili swala lingemalizwa na hao wahusika wawili kwa kutoa adhabu kali ikiwemo kurudia kufundisha tena mwakani ama kurudishwa mwaka mmoja nyuma hlf kwann wasisikilizwe kabla hawajahukumiwa watu wanaua mamilioni ya watu lakn wanapewa nafasi ya kusikilizwa mm ni mdau namba moja wa serikali iliyopo madarakani lakn kwa hili hawajajipanga nadhani waziri asingetoa maamuzi magumu kiasi hicho pengine hata angekishinikisha chuo kuwachukila hatua kali vijana hao

Kuna wanafunzi kibao wanaosomea udaktari, ufamasia na unesi hawa wanatenda maovu makubwa kwa wagonjwa pengine zaidi ya unavyoweza kudhania tena kwa uzembe tu ikiwemo kutokutoa huduma sahihi kwa wagonjwa hadi kupelekea vifo vyao lakn kigezo tu wapo mafunzoni wanapewa second chance tukiamini ipo siku watafanya kwa usahihi

Aisee nimeamini simba akimla mbuzi kawaida ila mbuzi akimla simba ndo habari ya mjini

Ni juzi juzi tu hata miezi mitatu haijaisha makamu wa shule kapigwa hadi kuvunjwa meno matano na wanafunzi bila ya kosa lakn hakuna hatua iliyochukuliwa hadi sasa ticha kibogoyo lakini juzi huyo dogo kapigwa kidogo wala hajapata jeraha lolote yupo tu anazurura mtaani ila..... Aisee tuwaache walimu wanajitoa sana
Sasa mvuta bangi kwanini hawakumpeleka polisi alafu hioo tv umeiona imevunjika??
 
Anaweza kuwa mbuzi wa kafara na kupigwa mawe....ila anesaidia sana kupunguza ukatili wanao fanyiwa watoto masiki kwenye shule za kata, jambo kama hilo huwakumba watoto wa walala hoi. Maana shule binafsi hakuna fimbo. Hivyo anesaidia kiasi kikubwa kwa Waalimu kujieshimu na kufuata taratibu za uwalimu.
 
Kuna uwezekano mkubwa ile sauti onayosikika kwenye video ikiwahimiza wenzie waache kumshambulia mwanafunzi lakini bila mafanikio.
Huyo binti anastahili nishani sio adhabu.
 
Nimekuelewa mkuu, kuna waalimu walichapwa viboko mkoan Kagera miaka kadhaa iliopita Na aliewachapa akapanda cheo hadi Leo kesi yao mahakamani haina mashiko

Hili limeonekana tukio kubwa tu coz liko kwenye clips lkn tuliosoma enzi za mwinyi Na mkapa adhabu za walimu wetu ilikuwa ni mangumi ofisin kwake baada ya hapo yanaisha
Hilo suala lingeweza kuisha kwa aman tu lkn aliyekuwa akirecod anapiga kelele tu " mwachen mtamuumiza huku anaendelea kurecod tu ni sawa na ajari kutokea unarecod video tu baada ya kusaidia majeruh kuwah Hosp.

NB ushaur kwa waalimu fundishen WANAFUNZI wanaojitambua hasa wenye malez Bora toka kwa wazaz wao wengine achana nao wakawe mascopion mtaani.
Ujue kuna kipindi watu walijua wazungu ni miungu ila sasa zama zimebadilika watu wana akili na sio wakushadadia uonevu inawezekana dogo mtukutu au vyovyote kama mnavyosema ila kupita yeye ujumbe umefika na uonevu hauto endelea tena mashuleni na hadi shule binafsi zitachukua tahadhari.
Dada aliyechukua video hii kaleta mapinduzi katika utoaji wa adhabu mashuleni.
 
we unayemlaumu mchukua video utakuwa na tatzo akilini......kwa uonevu uleeee
 
Huyo ni m.p.u.m.b.a.v.u hana ethnic za utumishi, hebu tujiulize hivi ni Kazi gani isiyo kuwa na changamoto? Mfano polisi kama wangekuwa wanarekodi na realese clips zao siingekuwa ni hatari? Majeshi Mbalimbali kama hawana kiapo cha uutii nahisi wengi wangefukuzwa kazi. Kwa kitendo cha kurekodi na kuachia clip hiyo, huyo mwalimu aogopwe kama ukoma hafai kuishi na jamii ya kufanya naye kazi. Bodi ya shule imchukulie hatua kali sana
Sasa polisi ni taasisi ya kupambana na uhalifu na shule ni mahali pakutoa mafunzo kwa wanafunzi ebu muwe mnafikiri hata kidogo basi
 
Sidhani kama alikuwa mwalimu kabisa nahisi alikuwa wa field maana mshambuliwaji alisema kuwa walimu wote wengine walikua kwenye kikao wakati tukio hilo la mashambulizi likitokea..source mshambuliwaji
 
Ila alochukua video kasimu kake kazuri kweny upande wa video.
Kana camera bomba kiaina.

Sijui alitumia MB za kifurushi cha chuo kusambaza hiyo video!!!?
 
Huyu mtu ni nani?
Je, na yeye ni mwalimu kabisa au alikuwa kwenye mazoezi?
Mwenyewe wamemchukulia hatua gani?
Akiachwa atakuwa amependelewa sana, kama mkuu wa shule alichukuliwa hatua hakuna jinsi huyu aliyerekodi video aachwe!
Mkuu wa shule hakuwa na taarifa kabisa ya tukio lile hadi anakuja kuliona kwenye mtandao siku sita baadae, lengo la mchukua taarifa halikuwa kusaidia bali ni umbea na kuwachomea wenzie.

Watanzania hebu pimeni wenyewe ni watu wangapi wamekasirishwa na tukio lile ambalo lingeweza kumalizika kwa amani kabisa ndani ya Ofisi husika. Pia hakupaswa ku concentrate kwenye video while kijana alikuwa anaumizwa, alivyoona wenzie wanahasira yeye ambaye alikuwa hajakasikirika angepaswa kuplay part hapo.

Watu tunawaona Walimu wanafunzi wale kama wanyama na tunasahau upande wa pili kabisa...

Isitoshe vijana wale walikuwa mazoezini, inawezekana bado hawajafundishwa how to handle cases of that type, au hicho kipengele hawajakifia.
Ilipaswa waonywe na wafundishwe as walikuwa kwenye Teaching Practice (ni sehemu ya mafunzo).

Ndalichako na hao waheshimiwa wengine wamekurupuka sana kwenye maamuzi, kisingizio kikiwa ni jinai kwani wameua?
Huyu aliyerekodi tukio hili asiachwe.
Kiukweli kunawatu watatuzaidi wakuchukuliwa hata hapo ,1;mwalimu wazamu,yeye hakufikiaha matuko kwa mkuu.
2;aliyechua hiyo video, yeye ameleta uchochezi,
3;mwanafunzi kwaaneyefikili vizuri kwanza hujiuliza ilikuaje hadi kutokea vile,kiundani utagua tu mwanafunzi anamtatizo,
NAJUA WAKLUPUKAJI WOTE HAWEZI KUKUBALI HAY ila kwa wanofikilitu,
 
Back
Top Bottom