Aliyerekodi Video ya Mwanafunzi kushambuliwa na Walimu

Aliyerekodi Video ya Mwanafunzi kushambuliwa na Walimu

Huyu ticha na mfananisha na scorpion...
 
Huyu mtu ni nani?
Je, na yeye ni mwalimu kabisa au alikuwa kwenye mazoezi?
Mwenyewe wamemchukulia hatua gani?
Akiachwa atakuwa amependelewa sana, kama mkuu wa shule alichukuliwa hatua hakuna jinsi huyu aliyerekodi video aachwe!
Mkuu wa shule hakuwa na taarifa kabisa ya tukio lile hadi anakuja kuliona kwenye mtandao siku sita baadae, lengo la mchukua taarifa halikuwa kusaidia bali ni umbea na kuwachomea wenzie.

Watanzania hebu pimeni wenyewe ni watu wangapi wamekasirishwa na tukio lile ambalo lingeweza kumalizika kwa amani kabisa ndani ya Ofisi husika. Pia hakupaswa ku concentrate kwenye video while kijana alikuwa anaumizwa, alivyoona wenzie wanahasira yeye ambaye alikuwa hajakasikirika angepaswa kuplay part hapo.

Watu tunawaona Walimu wanafunzi wale kama wanyama na tunasahau upande wa pili kabisa...

Isitoshe vijana wale walikuwa mazoezini, inawezekana bado hawajafundishwa how to handle cases of that type, au hicho kipengele hawajakifia.
Ilipaswa waonywe na wafundishwe as walikuwa kwenye Teaching Practice (ni sehemu ya mafunzo).

Ndalichako na hao waheshimiwa wengine wamekurupuka sana kwenye maamuzi, kisingizio kikiwa ni jinai kwani wameua?
Huyu aliyerekodi tukio hili asiachwe.
Mmh naona akili zako ziko likizo mkuu yawezekana ikawa nawe ni mwalimu wa mwendokasi
 
Nadhani anahitaji apandishwe cheo kabisa maana kuna wengi walikaa kimya na hawajachukua hatua yeyote huyu mtoa video mtandaoni kwangu mimi ndiye shujaa wa janga la mwanafunzi Yule.
 
Hivi kweli fimbo ni solution katika zama hizi .. Why do we have think primitively hivo kuna jinsi ya kuhandle wanafunzi hasa wanabalehe na fimbo sio solution zinduka

exactly! walimu wanatakiwa wacheze na pschology ya mwanafunzi kwa maneno tu inatosha sana na ndo wenzetu wa mataifa ya nje hufanya hivo.Binadamu maneno humuingia sana kuliko fimbo maana anakua sugu kinyume na hapo.
 
Nadhani anahitaji apandishwe cheo kabisa maana kuna wengi walikaa kimya na hawajachukua hatua yeyote huyu mtoa video mtandaoni kwangu mimi ndiye shujaa wa janga la mwanafunzi Yule.
Wengine wangechukua hatua gani kama tukio hawalijui?
We unadhani hiyo njia imemsaidia huyo mwanafunzi...
Ingekuwaje kama hao vijana wangechukuliwa hatua kwa utaratibu bila kuleta madhara zaidi?
 
Mimi najiuliza kwanini watanzania tumekimbilia kwenye tukio bila kufuatilia chanzo cha tukio?.Huyo Mwalimu aliyerecord hiyo video hana maadili alipaswa kutimuliwa pia,kimyakimya
Wanamwona ni mwalimu bora...wakati hawezi kuwa problem solver!! au walimu hawafundishwi haya mambo?
 
Wanamwona ni mwalimu bora...wakati hawezi kuwa problem solver!! au walimu hawafundishwi haya mambo?
Tumeshaondolewa hekima tumebaki kukimbizana na matukio bila kuhangaikia chanzo cha matukio.Mungu atusaidie.
 
Hilo ni fundisho kwenu walimu, na pia amewaokoa na jela kwa upigaji huo mngekuja kuua mtu siku mkanyee debe
mkuu, mi naona hajaokoa kitu! Mnasahau kuwa hao vijana walikuwa mafunzoni? Walihitaji kufundishwa zaidi na kwa utaratibu mzuri zaidi ya huu uliochukuliwa na kina Ndalichako.
 
Huyu mtu ni nani?
Je, na yeye ni mwalimu kabisa au alikuwa kwenye mazoezi?
Mwenyewe wamemchukulia hatua gani?
Akiachwa atakuwa amependelewa sana, kama mkuu wa shule alichukuliwa hatua hakuna jinsi huyu aliyerekodi video aachwe!
Mkuu wa shule hakuwa na taarifa kabisa ya tukio lile hadi anakuja kuliona kwenye mtandao siku sita baadae, lengo la mchukua taarifa halikuwa kusaidia bali ni umbea na kuwachomea wenzie.

Watanzania hebu pimeni wenyewe ni watu wangapi wamekasirishwa na tukio lile ambalo lingeweza kumalizika kwa amani kabisa ndani ya Ofisi husika. Pia hakupaswa ku concentrate kwenye video while kijana alikuwa anaumizwa, alivyoona wenzie wanahasira yeye ambaye alikuwa hajakasikirika angepaswa kuplay part hapo.

Watu tunawaona Walimu wanafunzi wale kama wanyama na tunasahau upande wa pili kabisa...

Isitoshe vijana wale walikuwa mazoezini, inawezekana bado hawajafundishwa how to handle cases of that type, au hicho kipengele hawajakifia.
Ilipaswa waonywe na wafundishwe as walikuwa kwenye Teaching Practice (ni sehemu ya mafunzo).

Ndalichako na hao waheshimiwa wengine wamekurupuka sana kwenye maamuzi, kisingizio kikiwa ni jinai kwani wameua?
Huyu aliyerekodi tukio hili asiachwe.
Huo adhabu ya nini wakati amesaidia kujua yanayoendelea mashuleni
 
Scorpion mtoboa macho watu walilalamika kwa nini waliokuepo eneo la tukio walimwacha afanye uhalifu ule ila kwa huyu mwalimu aliyerekodi hakuna hata mmoja anayemlaumu kutoenda kuamulizia yule mwanafunzi anayepigwa badala yake ndio kwanza anapongezwa.
Watu wanatumia mihemko mkuu.
 
Huo adhabu ya nini wakati amesaidia kujua yanayoendelea mashuleni
ni kweli, lakini kama tayari alikuwa na video kwanini hakwenda kwa mkuu wa shule na kumweleza lililotokea endapo mkuu angeshindwa kuchukua hatua stahiki bado angeli foward mbele...
Hapa angewasaidia hao vijana na huyo mwanafunzi bila kuleta madhara makubwa.
 
Kuna utaratibu kwamba hakimu..walimu au waziri hawaingiliana kwenye kazi zao...kuna sauti ilikua inasema mwacheni mtamuumiza sasa angefanyaje zaidi kama wanaendelea? Itoshe kusema hilo jambo ni baya kwa viwango vyote hata kama kweli mwanafunzi yule ni sugu...
 
Tatizo watu hamfuatilii ishu kwa undani, ndio kapigwa sana ila huyu dogo angekuwa nyumbani kwenu pengine angeshakutoa meno yote

Ebhu fikiria kamtukana baba yake mbele ya staff, kashavunja TV ya nyumbani kwao na baba yake hataki hata kumuona kashakamatwa shule ni anavuta bangi hapo yenyewe aliwapiga walimu watatu ngumi za hatari ila baadae wanafanikiwa kumdhibiti na zile ni hasira tu pengine ingekuwa ww ungempiga zaidi ama kumvunja mahali

Hlf tukumbuke wale walimu wapo mafunzoni na wapo chini ya uangalizi wa walimu wazoefu na chuo hili swala lingemalizwa na hao wahusika wawili kwa kutoa adhabu kali ikiwemo kurudia kufundisha tena mwakani ama kurudishwa mwaka mmoja nyuma hlf kwann wasisikilizwe kabla hawajahukumiwa watu wanaua mamilioni ya watu lakn wanapewa nafasi ya kusikilizwa mm ni mdau namba moja wa serikali iliyopo madarakani lakn kwa hili hawajajipanga nadhani waziri asingetoa maamuzi magumu kiasi hicho pengine hata angekishinikisha chuo kuwachukila hatua kali vijana hao

Kuna wanafunzi kibao wanaosomea udaktari, ufamasia na unesi hawa wanatenda maovu makubwa kwa wagonjwa pengine zaidi ya unavyoweza kudhania tena kwa uzembe tu ikiwemo kutokutoa huduma sahihi kwa wagonjwa hadi kupelekea vifo vyao lakn kigezo tu wapo mafunzoni wanapewa second chance tukiamini ipo siku watafanya kwa usahihi

Aisee nimeamini simba akimla mbuzi kawaida ila mbuzi akimla simba ndo habari ya mjini

Ni juzi juzi tu hata miezi mitatu haijaisha makamu wa shule kapigwa hadi kuvunjwa meno matano na wanafunzi bila ya kosa lakn hakuna hatua iliyochukuliwa hadi sasa ticha kibogoyo lakini juzi huyo dogo kapigwa kidogo wala hajapata jeraha lolote yupo tu anazurura mtaani ila..... Aisee tuwaache walimu wanajitoa sana
Nimekutukana Tusi 1 kubwaa sana!
 
Nimekuelewa mkuu, kuna waalimu walichapwa viboko mkoan Kagera miaka kadhaa iliopita Na aliewachapa akapanda cheo hadi Leo kesi yao mahakamani haina mashiko

Hili limeonekana tukio kubwa tu coz liko kwenye clips lkn tuliosoma enzi za mwinyi Na mkapa adhabu za walimu wetu ilikuwa ni mangumi ofisin kwake baada ya hapo yanaisha
Hilo suala lingeweza kuisha kwa aman tu lkn aliyekuwa akirecod anapiga kelele tu " mwachen mtamuumiza huku anaendelea kurecod tu ni sawa na ajari kutokea unarecod video tu baada ya kusaidia majeruh kuwah Hosp.

NB ushaur kwa waalimu fundishen WANAFUNZI wanaojitambua hasa wenye malez Bora toka kwa wazaz wao wengine achana nao wakawe mascopion mtaani.
Acha Urongoo Wewe.Mbona yule aliyechapa wanafunzi alishafukuzwaa unadhani unafatilia Taarifa pekeako..Yaani ninyi walimu wanafunzi mliofukuzwa Chuo Sasa hamna Kazi kwa Ubabe wenu mnashinda Social media kutaka Huruma.IPO Ivi inaonyesha Ndo Tabia zenu Sasa Za Mwizi Arobain.
 
Aliyerecodi hana kosa ili wengine wajifunze adhabu zipo nyingi tu cyo huo unyama
 
Kwani alikusudia kumwarifu nani. Wote pamoja aliyerekodi wana makosa. Alirekodi kwa kujifurahisha na akataka kuwafurahisha wengine bila ktafakari matokeo ya hili jambo. Uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana. Angeweza kurekodi kisha akampelekea mkuu wake au hata ikiwa vypmbo vingine lakini kurusha hewani uliuwa ukinga na imbea
Watu kama nyiee ni wajingaa Na huenda MNA Ukoo Na Watuhumiwa..Ebu fuatilia ishu vizuri Ndo uje kuropoka Hapa.Iyo Video ilikuwa ya siku 6 nyuma mrekod video akisubili haki.Cha ajabu nothing happened.Ndo Kairusha.Afiche maovu kwa kumuogopa nani
 
Back
Top Bottom