1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,802
- 10,306
Huyu mtu ni nani?
Je, na yeye ni mwalimu kabisa au alikuwa kwenye mazoezi?
Mwenyewe wamemchukulia hatua gani?
Akiachwa atakuwa amependelewa sana, kama mkuu wa shule alichukuliwa hatua hakuna jinsi huyu aliyerekodi video aachwe!
Mkuu wa shule hakuwa na taarifa kabisa ya tukio lile hadi anakuja kuliona kwenye mtandao siku sita baadae, lengo la mchukua taarifa halikuwa kusaidia bali ni umbea na kuwachomea wenzie.
Watanzania hebu pimeni wenyewe ni watu wangapi wamekasirishwa na tukio lile ambalo lingeweza kumalizika kwa amani kabisa ndani ya Ofisi husika. Pia hakupaswa ku concentrate kwenye video while kijana alikuwa anaumizwa, alivyoona wenzie wanahasira yeye ambaye alikuwa hajakasikirika angepaswa kuplay part hapo.
Watu tunawaona Walimu wanafunzi wale kama wanyama na tunasahau upande wa pili kabisa...
Isitoshe vijana wale walikuwa mazoezini, inawezekana bado hawajafundishwa how to handle cases of that type, au hicho kipengele hawajakifia.
Ilipaswa waonywe na wafundishwe as walikuwa kwenye Teaching Practice (ni sehemu ya mafunzo).
Ndalichako na hao waheshimiwa wengine wamekurupuka sana kwenye maamuzi, kisingizio kikiwa ni jinai kwani wameua?
Huyu aliyerekodi tukio hili asiachwe.
Ni kweli kabisa. Huyo aliyerikodi ili video amefanya kosa litakaloigharimu sana tasnia ya ualimu na walimu kwa muda mrefu.
Jamii kwa muda mrefu ilishaanza kuwachukia walimu.Sasa huyo aliyerikodi amezidisha chuki maradufu kwa walimu na labda anadhani kuwa yeye atapona dhidi ya chuki waliyonayo wananchi kwa walimu.
Ni kweli kabisa Prof. Ndalichako asimuache huyu Mwalimu aliyerikodi .
Nadhani ni jambo baya sana kwa wafanyakazi kurikodi baadhi ya matukio ambayo yangeweza kuripotiwa kwenye uongozi na kupatiwa uvumbuzi.
Hebu tuchukulie mfano manesi na madaktari nao waanze kurikodi yale yanayofanyika huko hospitalini ama kwa kukusuadia au ni ajali kazini?
Au atokee askari polisi aanze kurikodi wenzake wawapo kazini hasa wanapofanya upelelezi na kuamua kutumia nguvu kiasi fulani kwa lengo la kupata ukweli wa jambo. Eti atokee askari na kuwarikodi wenzake kisha kusambaza video hizo kwenye mitandao kwa lengo la kuwashitaki wenzake.Nadhani huyo atakuwa hafai kabisa na atazidi kujenga uhasa na jamii.
Au mfano tu ndani ya baraza la mawaziri ikitokea kuwa kuna mmoja amefanya jambo lisilofaa kwa jamii ndani ya kikao halafu mwingine amrikodi na kuweka kwenye mitandao. Itakua ni jambo la kupigwa vita kwa nguvu zote.
Haya yakiruhusiwa kuendelea kuna siku itafika ambapo walimu wote watakuwa wanashambuliwa na wanafunzi na watakosa pakusemea kwani jamii itawaona kuwa ni watu katili wasiojua malezi.
Mi naamini hata mtoto wa kumzaa anapojaribu kumpiga mama yake mzazi ni lazima familia nzima itasimama na kumtwanga vizuri sana na hata ikiwezekana kumkata shingo kabisa. Kila idara inataka kuheshimiwa na wale walioko chini yao.
Nakumbuka wakati wa kampeni mwaka 2005 Kule mwanza kuna mtu alijaribu kumshambulia mgombea wa CCM lakini kipigo alichokipata hata sahau maishani mwake. Yote aliyataka mwenyewe kwa kutoheshimu mamlaka .
Tena nadhani walimu wa siku hizi ni wapole sana. Enzi zetu hakuna mwanafunzi ambaye angeweza kuthubutu kuwapiga walimu tena akiwa kwenye ofisi ya walimu mbele ya walimu wengine halafu abaki salama kama shujaa.
Naunga mkono kwamba huyo mwalimu aondolewe kwani pia itakua ni vigumu hata kwa walimu wenzake kufanya naye kazi kwa upendo.
Jamii ina mambo mengi yanayofanyika kwa siri hasa huko maofisini lakini kila jambo linashughulikiwa kiofisi na sio kurikodi na kurusha kwenye mitandao.