Aliyerekodi Video ya Mwanafunzi kushambuliwa na Walimu

Aliyerekodi Video ya Mwanafunzi kushambuliwa na Walimu

hivi kwanini hii isingekua kesi wakaitwa wale walimu, wanafunzi mashahidi na walimu
na huyu mdundwaji tukajua nini hasa?
na nani kaonewa
 
Sababu za kuchukua hiyo video ilikuwa nini hasa? Anajua taratibu za kazi yake:?

Well, amechukua picha, baada ya hapo "mwalimu" anarusha mitandaoni ili kila mtu aone "ofisini kwake" wanavyofanya kazi. Hakika huyo hata taratibu za kazi yake hazijui, hajui kuna mwalimu na kamati ya nidhamu shuleni, hajui yupo mwalimu mkuu wa shule, kaona the best way ni kuonyesha ulimwengu ofisi yake inavyofanya kazi.

Ni mtizamo wangu, sidhani kama anafaa kuwa mwalimu, hata kuwa personal secretary hafai.

Inaonekana una busara sana mkuu. Ilitakiwa tujue displine master wa shule na kamati yote ya nidhamu kama walikaa hata kabla ya kurusha hiyo clip. Siafiki waliokifanya hao walimu. Lakini pia siafiki ukurupukaji katika utoaji wa maamuzi!
 
Cjakuelewa yaani wataka kutuambia kuwa,wale walimu wametenda haki kwa yule mtoto?au heb tueleweshe vizur
 
Sababu za kuchukua hiyo video ilikuwa nini hasa?

Sababu anaijua yeye mwenyewe. Lakini vipi kama nia yake ilikuwa ni kufichua maovu yafanywayo na walimu?

Anajua taratibu za kazi yake:?

Mimi sijui. Wewe unajua?

Na hizo taratibu zake zinamzuia kurekodi matendo maovu?

Well, amechukua picha, baada ya hapo "mwalimu" anarusha mitandaoni ili kila mtu aone "ofisini kwake" wanavyofanya kazi.

Naam, ubaya uko wapi hapo? Bila hiyo video wewe ungejua kuwa huyo dogo walimfanyia hivyo?

Hakika huyo hata taratibu za kazi yake hazijui, hajui kuna mwalimu na kamati ya nidhamu shuleni, hajui yupo mwalimu mkuu wa shule, kaona the best way ni kuonyesha ulimwengu ofisi yake inavyofanya kazi.

Kwanza, umejuaje kama hazijui hizo taratibu? Pili, hizo taratibu ni zipi? Ziweke hapa ukitoa na rejeo la kimamlaka.

Tatu, umma umejua yanayofanyika ofisini kwake. Baya liko wapi hapo?

Ni mtizamo wangu, sidhani kama anafaa kuwa mwalimu, hata kuwa personal secretary hafai.

Sawa, ni mtazamo wako. Lakini nami mtazamo wangu juu ya mtazamo wako ni kwamba mtazamo wako haufai. Umepotoka.
 
Huyo ni mnafiki alikuwa na uwezo kabisa wa kuzuia lile, mie nishawahi mdaka mwalimu wa kiume alotukanwa tusi na mwanafunzi akataka kumvaa mwanafunzi kwa hasira, tulifurukuta hadi tukaanguka chini then wengine wakaingilia kati na kumshika mtoto.

Unadhani hizo hasira hazitokei? Ila akitokea mmoja akatake action basi taratibu na wengine wanarelax na kutuliza munkari then case inakuwa solved ikiwa wote wako calm.
Hata mimi ninaamini kabisa huyo mchukua video ni mnafiki.
Maajabu hakumshirikisha hata Mkuu wake au hata kiongozi mwingine, yeye anakimbilia mitandaoni.
 
angeanzia kw mkuu iyo kesi icngekua na nguvu tena ingezimwa shuleni na hao walimu wa field wasinge adhibiwa na serikali
 
angeanzia kw mkuu iyo kesi icngekua na nguvu tena ingezimwa shuleni na hao walimu wa field wasinge adhibiwa na serikali
Kiukweli dogo kabla ya pale, alikataa kuchapwa wala kuchuchumaa pamoja na kwamba wenzie wamechapwa ambao wote hawakufanya zoezi darasani alipohojiwa akamjibu vibaya mwal katika kumshika wamchape akampa ngumi ya mdomo mwalimu. Ilibidi Wamchukue wampeleke ofisini lakini mwl aliyepigwa ngumi awali alirudi darasani kutuliza wanafunzi wengine. Alipoona wametulia alianza kurudi ofisini kumbe yule dogo pale ofisini alipoona walimu wamebaki wawili tu akawapa dozi ya ngumi wakamshindwa. Akaanza kutoka nje ya ofisi anakimbia yule mwalimu alikuwa darasani akamuona na kumuwahi ukapigwa mkono kidogo akammudu na kumrudisha ofisini kwa walimu wengine hapo ndio kila mmoja akajikuta anahitaji kumaliza hasira zake. Walimu kadhaa wakiwa wanaugulia maumivu.

Unajua kwa huyu dogo yeye aliridhia kichapo alichopewa na walimu ndo maana siku11 toka tukio limetokea wala hajaripoti. Hata home hakwenda kusema kwakuwa anakesi tatu nzito na aliwahi kumjibu hovyo baba yake mbele ya walimu alipokuwa ameenda kutetea asifukuzwe. Achilia mbali hayo ameshavunja tv ya dingi yake home wiki mbili zilizopita. Wiki hili amekamatwa na walimu akivuta bangi shuleni na wenzake. Baba yake anasema simtaki huyu nyumbani kwangu. Hivyo tusiangalie mtu alipojikwaa tuangalie pia source ya kujikwaa. Tunapotoa maamuzi tuangalie mambo kwa ujumla wake.
 
Kila kitu kinasababu hapa duniani. Hata inzi pamoja na kuchukiwa na uchafu wake anakazi ya kufanya
 
Hakuna upande wa pili tulichoona ni kipondo tu wasikate tamaa waombe kazi jeshini
 
yule ticha mpiga picha ni genious sana kaitumia smartphone yake ipasavyo safi sana.
 
Back
Top Bottom