Aliyepata elimu ya msingi na sekondari katika shule za serikali hajui chochote zaidi ya kukariri majibu kwaajili ya mitihani ya taifa

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,124
Habari!

Hii mada imeshushwa kama ina kakejeli ndani yake ila ndio ukweli.

Ukiondoa shule chache za msingi za serikali ambazo kidogo zina afadhali kama Diamond primary school and like. Ukuondoa sekondari zile za vipaji vya juu na kati tulizosoma zamani ambazo mnakutana wanafunzi kutoka kona zote za Tanzania shule zingine zote za serikali hamna kitu.

Shule za kata za sekondari wakuu wa shule wanapambana watoto wapate kufaulu ili wasishushwe madaraka, wakuu wa shule za msingi za serikali vivyo hivyo hupambana watoto wafaulu kwa % kubwa waende sekondari ili wasishushwe au kuvuliwa madaraka.

Mwanafunzi aliyesoma shule hizi za hovyo hata akipata PhD bado PhD yake itakuwa ya kuungaunga tu.
 
Shule za English medium primary zinaongoza kuwapa watoto wa majibu kwenye mitihano ya taifa...!hao diamond na olyimpio ndo balaa kwa cheating!

Narudi kwenye hoja yako ya msingi.

Shida hapo ni mfumo wa Elimu ndo umeoza,haiwezekani mtoto wa Feza,St Fransis umpime sawa na mtoto wa Sangamwalugeshi kipimo hiko hiko kwa mitihani ya Kiingereza wakati huyu wa Sangamwalugeshi Kiswahili tu hajui anaongea kisukuma.

Walimu wanaangalia matakwa ya serikali na wanaoharibu ni hao serikali wenyewe maana wanasema ktk usahihishaji wa kitaifa mtoto asahihishiwe idea tu kama mfano jibu la swali ni 3,dogo akaandika 2.5 baasi amepata huyoo!

Au jibu la swali ni nations, dogo akaandika neshno. anapewa tiki!

Na hyo ndo system ya elimu ndo maana mpk vyuo vikuu kuna shida MTU ni graduate lakini hana uwezo wa kureseaon chochote kile!!!

Na kuhusu kata wapo watoto wanafanya vzr sana sasa hivi huku katani maana wanaletwa watoto wanaojua vingereza walosoma English medium primary pia!!! Wapo ambao wanapata mpk 1 za single digits

Hvyo before kulaumu watoto ,tubadilishe mfumo kwanza!
 
Hakuna kitu kibaya maishani kama kujidanganya nafsi. Uzoefu unaonyesha kuwa elimu ni kitu kipana sana. Huwezi kutumia mambo machache kuamua nani ana elimu na ameelimika.
Hata private schools, zinatoa watu wanaofaulu mitihani na wachovu wakubwa kwenye maisha. Wengine ni watoto wa mama na baba mpaka wanatangulia mbele ya haki
 
Point yako haiko sahihi kabisa, hata shule hizi za English medium watoto wengi wanakririshwa ukipindisha swali hawachomoki, suala la kuelewa mwanafunzi inategemea kafundishwa na kufanyishwa mazoezi ya hilo somo na mwalimu anayejua namna ya kutegua mitego ya maswali ili apate kuelewa
 
Shule za English medium primary zinaongoza kuwapa watoto wa majibu kwenye mitihano ya taifa...!hao diamond na olyimpio ndo balaa kwa cheating...!!!

Narudi kwenye hoja yako ya msingi!!

Shida hapo ni mfumo wa Elimu ndo umeoza,haiwezekani mtoto wa Feza,St Fransis umpime sawa na mtoto wa Sangamwalugeshi kipimo hiko hiko kwa mitihani ya Kiingereza wakati huyu wa Sangamwalugeshi Kiswahili tu hajui anaongea kisukuma...
Walimu wanaangalia matakwa ya serikali na wanaoharibu ni hao serikali wenyewe maana wanasema ktk usahihishaji wa kitaifa mtoto asahihishiwe idea tu kama mfano jibu la swali ni 3,dogo akaandika 2.5 baasi amepata huyoo!!
Au jibu la swali ni nations, dogo akaandika neshno...anapewa tiki!
Na hyo ndo system ya elimu ndo maana mpk vyuo vikuu kuna shida MTU ni graduate lakini hana uwezo wa kureseaon chochote kile!!!

Na kuhusu kata wapo watoto wanafanya vzr sana sasa hivi huku katani maana wanaletwa watoto wanaojua vingereza walosoma English medium primary pia!!! Wapo ambao wanapata mpk 1 za single digits

Hvyo before kulaumu watoto ,tubadilishe mfumo kwanza!
Mwenye sekta yako umeandika vizuri.
Mimi nimesoma shule anazozisema yeye lakini nina ufahamu kuliko hao waliosoma huko. Nina rafiki zangu huwa nawauuliza walipitaje form four na form six kwa namna walivyo na akili ndogo ya kureason.
 
Sijawahi kutukana mtu ila daa, ulitakiwa uwe wa kwanza aisee, sijui unakwama wapi, mwishoe mtasema na waliosomesha la bodi ya mikopo nao hamna kitu pia.
Watu na utajiri wenu
Achana nae huyo. Ukimfuatilia kwa karibu unawezakuta ukoo wake wote haujaenda shule ndio maana ana hasira na waliosoma.
 
Ambao wametoka shule za kama za kata wenye division 3 wakikutana na wenye division 1 kutoka hizo shule kubwa kubwa za private utaweza kupata majibu vizuri nani mwenye uelewa mpana
 
Nakutana na madogo wanasoma hivi Vi-english medium zingine zinaongoza kimkoa kabisa, lakini ni weupe kabisa kichwani.

Hata mimi kipindi niko primary japo kidumu na mfagio ila wangenizidi kiingereza tu.
 
Aliwahi uliza swali prof Ndalichako k=kuwa " hivi wale wanafunzi wanaokuwa bora na kuongoza kitaifa huwa wanaishia wapi, mbona huku vyuo vikuu hatuwaoni" hii ni baada ya kuona hata wale wanaoitwa bora kitaifa wakifika huko juu wanakuwa wakawaida sana! so wakati mwingine aina ya shule unayosoma haiwezi ku determine your future au your intelligence!
 
Ajabu ni pale hao wanafunzi wa asante kayumba wanapo wa buruza wa private kwenye masomo ya juu.
Ukiondoa form one na two,hao wa private kwingine huko ushikishwa namba za viatu balaa.
 
Bila shaka umezaliwa jana. Hivyo kwa akili yako unajua kulikuwa na hizo shule unazozifikiri kuwa zilizkuwepo tangu zamani.

Kwa habari yako kwa taifa hili wote wenye umri wa kuanzia miaka 40 walisoma shule za Serikali na zilikuwa nzuri sana. Zamani wasio na akili ndo walikuwa wanasoma shule za private na ufaulu wao na uwezo wao wa kuatambua mambo ulikuwa hafifu sana.
 
Back
Top Bottom