"Watanzania wenzangu mimi nilipigwa tarehe 8/3/2020, nilipigwa na Elibariki Kingu alinipiga nikaenda Mandewa hospitali ya Mkoa, nikaenda Benjamini Mkapa wakanipeleka Muhimbili, nikatibiwa na kufanyiwa operation mbili kichwani, nikaambiwa nirudi mwezi wa 8 lakini sikuweza kurudi kwasababu nilikuwa sina hela.
"Watanzania wenzangu ninaomba mnisaidie kwa yule atakayeguswa anisaidie, mimi sina shida na mtu ninaomba mnisaidie. Elibariki alinipiga bila kosa, mimi sio mwizi na wala sina tatizo lolote, ninaomba mnisaidie."