Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mmoja kati ya wanafunzi watatu kutoka vyuo vikuu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, waliodaiwa kumshambulia mwenzao wakimgombania msanii na mtangazaji wa vipindi vya redio, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku, ameswekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya jinai inayomkabili na wenzake hao.
Mwanafunzi huyo Mary Gervas Matogolo (22), mwanafunzi wa
Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, leo Mei 30, 2025.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, wanakabiliwa na jumla ya mashtaka manane ya kusababisha madhara kim-wili, kutishia kuua, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na uharibifu wa mali.
Mbali na Mary wanafunzi wengine waliopandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa tuhuma hizo ni Ryner Ponci Mkwawili wa
Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam na Asha Suleiman Juma, wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam (TIA) wanakabiliwa na mashitaka manane.
Hakimu Gwantwa, alitaja masharti ya dhamana, kuwa kila mshitakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili, wenye barua za utambulisho, vitambulisho vya Taifa, watakaotia watakaosaini Bondi ya dhamana ya Sh5 milioni kila mdhamini.
Washtakiwa Ryner na Asha wametimiza masharti hayo na kuachiliwa huru kwa dhamana lakini Mary ameshindwa kutimiza
masharti hayo ya dhamana.
Hivyo Hakimu Mwankuga ameamuru apelekewe mahabusu gerezani mpaka Juni 13, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena