Alinisaliti, nilichomfanyia hatokaa anisahau daima

Alinisaliti, nilichomfanyia hatokaa anisahau daima

I don't hit and run(atleast not anymore)
Nipo kwenye relationship(s) lakini nakua muwazi tangia mwanzo kua sihitaji a serious relationship
Brother pole ila unaujasiri wa tofauti. Unamuona wife akipanda bajaji na gari anakabidhiwa mtu mwingine then unamwacha tu dah unakitu fulan cha tofauti. Walau hata ungefuatilia uone ile gari inapoelekea. Au hata mngefika nyumbani then umwambie wife twende tukaifate gari huko kazini.
 
Pole sana wanawake kuna muda hatueleweki tunataka nini, mtu kakupa kila kitu anakuonyesha mapenzi yote lakini unamsaliti sijui huwa ni pepo gani aisee
Tena jamaa kaamua kutoangalia wanawake wengine wa pembeni akaona this is the wife material bado unamsaliti. Kiukweli wanawake nadhani kuna mahali kuna nature inawatesa.

Kuna jamaa angu anatumiwa picha na video alizojirekodi make wa mtu na pete ya ndoa inaonekana katika hizo video akiwa uchi. Mume wake akiwa sebuleni yeye chumbani anajirekodi na kumtumia jamaa. Dah hii si dunia tena ni laana
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana, nilikuwa na mwanamke nishamtolea mahali na akawa mjamzito kwa bahati nzuri nikapata scholarship kwenda kusoma nikimuacha kwangu ili nikitulia na shule tufunge ndoa!!
Baada ya miezi michache akijifungua na baadae mtoto kufariki, baada ya miezi michache nikawa nikipiga simu usiku iko busy sana, nikimwuliza anasema anaongea na kaka ake nikumwuliza tena kila siku mnaongea usiku tu?
Halikunipa shida sana, bahati mbaya nilipata msiba nikarudi home nilifika usiku sana, asubuhi kulipo kucha nikamwambia inabidi twende msibani lakini sina hela akanijibu ngoja niende kwa Dada ataniazima, nikasema sawa lakini ukweli nilkuwa na hela.
Baada ya kurudi akasema haja pata amesema atamrushia kwenye mpesa twende tu nikasema poa, tukiwa tupo stand simu yake iliisha charge akasema aweke laini kwangu nikasema poa, lakini simu nilibaki nayo Mimi!!
Baada ya mda iliingia sms ya mpesa ikiwa imetumwa tu kama text ya kawaida na ikafwata SMS ya kuwa umepata mke wangu?
Nikamwuliza huyu ninani akasema nishemeji yake, mimi nikampigia yule aliyetuma ile hela bahati nzuri jamaa alionesha ushirikiano mkubwa sana!!! Swali langu kwake lilikuwa vipi umekosea namba? Akasema hapana, nikamwuuliza tena huyu uliye mtumia hela unamfahamu na kama unamfaham ni nani yako? Akajibu na mfahamu ni mchumba wangu ameniomba hela anaenda msibani, nikasema ok!!!! Tulivyo fika kijijini simu za yule jamaa zilikuwa ninyingi sana ikabidi niongee nae kumweleza ukweli ulivyo akawa pia anashangaa!!!
Kwa kufupisha baada ya hapo nilimfukuza kama mbwa mwizi na nilipigiwa simu na wazazi wake na Dada zake lakini sikukubali ule ujinga, ndio ikawa mwisho wa yote
Dah hizi mambo ni nyingi sana. Kiufupi wanawake wote wanashahabiana. Wamezidiana tu viwango vya makinikia
 
Mahusiano mengi kwa sasa ni mwiba aisee,yalinipata magumu katika mahusiano miaka kadhaa iliyopita,nikaja kumwaga nyongo humu,lakini kwa namna nlivyokuwa affected nilishindwa kumalizia kuisimulia,pole sana mkuu
..malizia mkuu..
 
Unasema mwanamke akisalitiwa ni less painful kwake? Kwa kuwa yeye ana moyo wa jiwe ama hana hisia? Ila nyie mkisalitiwa ndo panauma kwa kuwa mna mioyo ya nyama sio? Endeleeni kusaliti, wanawake nao siku hz wameamka, wamechoka kufanywa wajinga. Ukimsaliti huku na yeye anakusaliti kule. Sasa ukijua unasalitiwa kunywa maji ushushie... Usaliti unauma pande zote. Usijidanganye eti kwa mwanamke ni less painful
..usishindane na wanaume,..ukigundulika unaachwa..
 
Duh, we jamaa, pole aseh, ungembwaga bila kumfanyia chochote, sasa kuruka ukuta umejiongezea dhambi. Kusamehe ni rahsi, ila inshu kusahau
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom