Aliepigwa risasi na polisi Mahonda - Zanzibar, afariki dunia

Calipso

JF-Expert Member
Mar 25, 2009
284
15
Baada ya harakati za kwenda donge kufanya mhadhara jumuiya ya Muamsho,wakati wapo njiani maelfu ya wananchi walikutana na polisi wakiwa wameweka road-block ktk kiji cha mahonda njiani,wananchi hao wakaamua kukaa kitako chini kwa wote waume na wanawake,Polisi baada ya kuona hivyo wakaamua kupiga mabomu ya machozi na kupiga risasi za mpira kwa watu na ndipo risasi zikawaangukia watu wawili, kati ya hao wawili mmoja amefariki dunia na waliingia mpaka misikitini kupiga watu na ktk msikiti mmoja pale mahonda umejaa damu mpaka jana..

Chanzo cha vurugu:

Jumuiya hii ilianda mhadhara huu zaidi ya wiki mbili nyuma na walikuwa wamekamilisha taratibu zote za kisheria na kukubaliwa kufanya,siku ya mhadhara ilipofika wakati watu wengine wengi sana washafika mapema donge kutoka maeneo ya jirani na donge na upande wa kaskazini,wakabaki watu wanaotoka mjini na kusini wao wakakutana mjini kwa ajili ya kuondoka, Mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya na Polisi wakawafuata maamiri wa muamsho ktk sehemu ya mbuyuni mjini znz na kuwaambia wasiende donge,maamiri hao wakawajibu tumekamilisha taratibu zote za kisheria tena kupitia kwenu,mbona hamkutwambia kabla kama tusifanye? leo watu washakusanyika hapa kutoka maeneo mbali mbali na washakodi magari na wengine wapo njiani kuelekea huko na wengine washafika donge tena wengi sana,ndio mnakuja kutwambia tusifanye,sisi tufanye nini wakati huu tena,basi angalau mngetwambia asubuhi mapema tukawatangazia watu kuwa hakuna mhadhara,(wakati huo walokutana ilikuwa ni saa saba mchana) mnatwambia wakati huu? hatuna jinsi kama mumeshadhamiria vibaya basi fanyeni,sisi hatuna la kufanya kwa wakati huu.
 
usongo wa nini? huu mtandao wa JF member wake hawafagilii mambo yanayo fanywa na wazenji, halafu nyinyi mnatuletea habari za UAMSHO na Wazenji, hatutaki
Wewe ndio hutaki,wengine tunaitaji kupata abari.kama hutaki nenda facebook kajadili mapenzi.
 
Poleni wote waliofiwa,kweli inasikitisha kama polisi watawatendea watu hivi.ingawa mimi sio uamsho wala muislam Lakini inasikitisha kama polisi walishatoa kibali kwa nini wafanye hivi.Mungu anatuagiza tupendane wote bila kujali kabila dini wala hali .Ni jukumu la polisi sasa kubalili muelekeo sasa watumie hekima na busara LAKINI KUTUMIA KUVU HAKUTASAIDIA ZAIDI YA KULETA MADHARA.
 
Ukiona mwenzio anaonewa piga kelele.wakati polisi walipouwa arusha wengine walinyamaza kwa sababu wao sio waarusha sasa imefika zenz wanapiga kelele!tungepiga kelele wote polisi wangekuwa walishaacha kuuwa raia.sasa zamu kwa zamu leo wanauwa huku kesho kule.haya bwana Mungu tupe hekima tupone.
 
serekali ya TANzanIA imeamuwa kutuuwa wazanzibar kwa kukataa muungano na tanganyika, haya ndio malipo yetu kukataa nchi yetu kufanywa mkoa wa tanganyika. ASANTENI majirari wabaya hawa.damu hii haitakwenda bure.

kinachofuata hapa si kurudi nyuma ni kubadili mtindo wa kudai haki maneno hayaeleweki soon political movement will change to conflict and general turmoil in tanzania

kisha bada ya hapo zanzibar na tanganyika zitachukuwa mfano wa korea ya kaskazini na korea ya kusini majirani mahasimu wakubwa(maji na mafuta hayata changanyika kamwe) VIONGOZI MAFISANI WAMEIANGAMIZA NCHI SASA KWA KUONGOPA MAONI TAFAUTI NA YAO.
 
Dhambi hii ya kuchoma makanisa itaendelea kuwalilia mpaka kikundi cha Kigaidi Cha UAMSHO choote kitakapo angamia
 
serekali ya TANzanIA imeamuwa kutuuwa wazanzibar kwa kukataa muungano na tanganyika, haya ndio malipo yetu kukataa nchi yetu kufanywa mkoa wa tanganyika. ASANTENI majirari wabaya hawa.damu hii haitakwenda bure.

kinachofuata hapa si kurudi nyuma ni kubadili mtindo wa kudai haki maneno hayaeleweki soon political movement will change to conflict and general turmoil in tanzania

kisha bada ya hapo zanzibar na tanganyika zitachukuwa mfano wa korea ya kaskazini na korea ya kusini majirani mahasimu wakubwa(maji na mafuta hayata changanyika kamwe) VIONGOZI MAFISANI WAMEIANGAMIZA NCHI SASA KWA KUONGOPA MAONI TAFAUTI NA YAO.

Mkuu! TL si aliwapa ufumbuzi mkamzomea?
 
zanzibar sio NCHI

Wakikusikia wahusika? Niliona jamaa mmoja ameleta picha ya Rais wa Nchi akikagua gwaride sijui ya KMKM! Maana kule kwetu Ushirombo tuna magwaride ya mgambo na hatujawahi kujitangaliza utaifa.
 
Back
Top Bottom