Albert Msando apotoka tena

Albert Msando apotoka tena

Tatizo watu wanataka kupiga story za mwanamke gani mjini ana ------ makubwa au anatembea na Diamond.

wewe mbona sikuelewi umekaa au umesimama au umechuchumaa!wewe ni gamba au ngozi!ueleweki au msando ni mwanasheria wa nyumbani kwenu!kwenda uko na magamba yenu.
 
Why are you taking it public kama wewe ni mwanachama na mbali ya hapo ni diwani hujui taratibu za chama kweli? Serena Hotel imekuwa sehemu ya mamlaka za chama hadi ujitokeze kila siku kwenye hadhara
Unaonekana mtoto kweli aisee
Nyie pro-Chadema mbona mnakuwa na siasa za makengeza Lema alivyokuja JF kumshambulia Zitto mbona mlikuwa kimya au kwa sababu wa nyumbani.
 
Jibu ni simple tu: anzishe uzi wa hayo mambo mengine tutaujadili bila tatizo,Chadema ni chama cha siasa kinanafasi kubwa ndani ya jamii na sasa ni Talk of the town ndiyo maana na ww umeacha mambo yako nakuja hapa kulalama that mean na ww ni mmoja wa hao hao unaowasema.

"mda mwingine kakaa KIMYA nalo ni jibu"
seeeeeeeeeee..............beee hebu nipishe huko
watu wenyewe ni bora hata gari ilokata senta bolt inaweza kufika nyie sijui mmekata chasis engo manake hamjulikan mpo wapi.............
kama ni ladha ndo kabisaa hamna hamjulikan mnanoga sukari ama chumvi ndimu ama pilipili mpo mpo tuuuu
kwa stail hii mtasubiri sana kuchukua nchi.......bora hata NRA kuliko nyie mbulula
 
Msondo tulisha kuona siku nyingi baada ya
kushauliwa ujitoe kwenye kesi ya viongozi
wetu ya Jan 5 baada ya kuja na kigezo cha
kuweka dau kubwa kuliko hata wanasheria
wakongwe halafu ukataka tukupe kabla hata
Hujkanyaga mahakamani lakani tulipofatilia
nyuma ya jambo hilo alikuwa ni zito leo
tunakuona kwenye harakati za kutaka
kukisambalatisha chama, nakuambia huto fanikiwa...
 
Dege wote wanye akinya bata kaharisha, mbona akina Tundu lisu,mnyika,dr slaa na mboe walieleza na kujibu tuhuma kwa waandishi wa habari? Hiki chama kimepoteza uelekeo hakifai kuaminiwa na kupewa ridhaa ya kutawala, wamejaa mimburaaaaaa tu, nawasiwasi na taaluma ya heche,saanane malemo yaricko na wajingawajinga wengine wa chadema.Wamejaa chuki,ujuha na uzadiki.
Kunawatu wao wanajifanya ni malaika na wana haki katika hii dunia. Bigup kwa kuliona hilo.
 
Anawafuasi wengi sana wamejiuzuru kwa ajili yake karibu kila mkoa,anawatoa matamko wengi sana karibu kila mkoa,so pls wewe kama mwanasheria wake mshaaulini tu muachane na CHADEMA muanzishe chama chenu na wewe utakua mkurugenzi wa sheria wa chama chenu achanane na hawa wahafidhina.

Pili mtaji tayari mnao na ruzuku uhakika upo maana vijana wenu wenye uhakika wa kupata ubunge ni kama wafuatao,Chagulani Adams atapata Nyamagana,Kashinje Masanja atachukua Shinyanga Mjini,Grayson Nyakalungu ye atachukua Serengeti,Mtela Mwampamba atachukua Mbozi na Habiba sorry Habibu Mchange atachukua Kibaha haya ni majimbo yenye ushindi kwa kishindo na bado jimbo la mwenyekiti Zitto Kabwe Kigoma Kaskazini atachukua kwa ushindi wa Tsunami.

ni ushahuri unawapa magamba wenzako au unawafariji kwa maafa yaliyowapata!hujui mlilia wembe kinachotokea mbele yake ni nini?pumbavuuu!!kojoa ukalale wewe!
 
Mwaikenda,

1. Kutetea utawala wa Sheria na tafsiri sahihi ya Katiba yetu ni kubomoa chama? Ndio mimi ni Diwani lakini itakuwa ajabu sana kusema kwamba kumtetea Zitto lazima nijiuzulu kwanza. Mimi sio mjumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu wala Mkutano Mkuu. Mgongano wa maslahi unatoka wapi? Naweza vipi kuathiri maamuzi ya vikao hivyo?

2. Je marekebisho ya Kanuni ya 2013 yalijumuisha kwamba kukiwa na dharura utaratibu uliotajwa kwenye kipengele (a) usifuatwe? Kwa nini kipengele kilichoongezwa cha (d) kilitaja utaratibu ambao hautafuatwa ni ule wa (b) na (c) peke yake? Hilo unalielezeaje?

3. Kikao cha Kamati Kuu kilikuwa kikao cha dharura? Waraka husika ulikamatwa siku hiyo hiyo ya kikao au jana yake kwa hiyo ikabidi maamuzi ya dharura yafanyike?

Kama ilikuwa ghafla hivyo kwa nini asingesimamishwa uongozi, apewe mashtaka kama Kanuni inavyosema halafu asikilizwe kwa dharura na adhabu itolewe ya kumvua uongozi? Dharura sio haraka kaka.

4. Kupewa taarifa rasmi kwa maandishi na mwenendo kupelekwa Baraza Kuu ni taratibu ambazo lazima zikamilike ili muadhibiwa aweze kukata Rufaa. Ndio maana taarifa ya nia imetolewa ili taratibu hizo zikamilike. Hakuna niliposema nataka mwenendo wa shauri. Tunachotaka ni taarifa rasmi ya maamuzi.

5. Mwenendo unatakiwa umefika Baraza Kuu ndani ya siku 14 toka tarehe 22/11/2013. Je umefikishwa?

Tusijadili kwa jazba na hasira. Mimi kueleweshwa kwa hoja ni mwepesi sana. Fanya hivyo na kama uko sahihi nitaconcede. Lakini sitaconcede kisa tu utasema akili au uelewa wangu mdogo.

Ahsante.

Ni vema ukaachana na habari zakujibizana na hawa watu hamtoweza kuelewana,coz akili ndogo haiwezi tawala akili kubwa na hiki ndicho kinachotokea kwa ZZK,
tunajua hizi ni hofo za uchaguzi.
Siku inakuja jiwe wanalolikataa waashi litageuka kuwa jiwe kuu la msingi
 
Mkuu,

Tangu Msando alipomaliza press conference yake mpaka sasa zimeshaanzishwa thread kama tano hivi. Zote ni za kumshambulia Msando na kumtisha kuwa atavuliwa uanachama.

Wengine wanasema hajaonekana kwenye kata yake mwaka mzima, wengine wanasema ni mtu wa starehe tu, wengine wanahoji anapata wapi pesa. Yaani ni chuki zisizokuwa na msingi kabisa

Watu kama hawa hawafai kukabidhiwa nchi. Watawafanya vibaya watu wenye mawazo tofauti nao.

siungi mkuu haya mathread, yanakera

Ila my take home message ni kwamba chadema si ya zitto wala ya cc wamekua chama cha misutano tu, wamekua kama khadija kopa na masma hamisi kidogo
 
Nyie pro-Chadema mbona mnakuwa na siasa za makengeza Lema alivyokuja JF kumshambulia Zitto mbona mlikuwa kimya au kwa sababu wa nyumbani.

wewe ndiyo makengeza. serena hotel na waandishi wa habari na uvccm siyo jf
 
Msondo tulisha kuona siku nyingi baada ya kushauliwa ujitoe kwenye kesi ya viongozi wetu ya Jan 5 baada ya kuja na kigezo cha kuweka dau kubwa kuliko hata wanasheria wakongwe galafu ikataka tukupe kabla hija kanyaga mahskamano lakoni tulipofatilia nyuma ya hambo hilo alikuwa ni zito leo tunakuona kwenye harakati kutaka kukisambalatidha chama... aise tutakuwinda

Ee Mungu kumbe huyu Jamaa ni nyoka hivyo?
 
siungi mkuu haya mathread, yanakera

Ila my take home message ni kwamba chadema si ya zitto wala ya cc wamekua chama cha misutano tu, wamekua kama khadija kopa na masma hamisi kidogo

Punguza munkari mkuu tupo busy tunakomboa nchi
 
Kunawatu wao wanajifanya ni malaika na wana haki katika hii dunia. Bigup kwa kuliona hilo.

wote nyie ni vilaza! kimya hamna sentensi wala tenzi,kojoeni kabla ya kulala msije mkakojoa kitandani maana akili zenu ni fupi kama mnavyofikiria.
 
seeeeeeeeeee..............beee hebu nipishe huko
watu wenyewe ni bora hata gari ilokata senta bolt inaweza kufika nyie sijui mmekata chasis engo manake hamjulikan mpo wapi.............
kama ni ladha ndo kabisaa hamna hamjulikan mnanoga sukari ama chumvi ndimu ama pilipili mpo mpo tuuuu
kwa stail hii mtasubiri sana kuchukua nchi.......bora hata NRA kuliko nyie mbulula

Bora msukule unaweza tumwa sehemu kuliko chuma chakavu lisilofaa kwa matumizi zaidi ya kurejeshwa kiwandani kutengenezwa product nyingine"wewe ni chuma chakavu"

kachumbari haikamiliki bila kutia mbwembwe zote ulizizitaja hapo
 
Kwahiyo hapa kosa la Msando ni kumpa Zitto huduma ya kitaalam ya sheria!!!

Mtanzania anayependa kumuona Zitto anataabika bila msaada wa kisheria hana nia ya kuona haki ikitendeka.

Mabadiliko mnayoandamana kuyalilia ndio lengo lake kuleta tabia hii ya kuchukia watu wanapopata msaada wa kisheria?

Kwanini mnataka kutoa hukumu kimyakimya vichochoroni?
 
Back
Top Bottom