Msando,
1. Kanuni ya 10.1 (xi) ya Kanuni za Uendeshaji kazi za Chama inasema hivi naomba kunukuu " Kiongozi anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na viongozi wa ngazi ya juu au vikao halali na kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kwa kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye Kanuni" mwisho wa kunukuu. Je Serena Hotel ni ngazi gani ya kikao cha Chama katika Katiba unayodai kuitetea? Wewe ni Kiongozi wa Kata wa Chama kwa mujibu wa Katiba, jipime.
2. Sababu zilizotolewa mngezijibu kwanza na kusubiri kikao husika ndipo mkate rufaa lakini kabla ya hatua mnazotaka tayari mmekimbilia Serena, Childish strategy and lack of confidence.
3. Kama sababu hazijitoshelezi je zinakosa uhalali wa kuwa sababu? ulitaka zijitosheleze kwa namna gani? Beyond reasonable doubt? utoto
4. Chadema wanasheria ni wengi mkuu. Do your home work
Ujinga uliofanywa leo kwenda kukianika Chama Serena ni sababu tosha ya Kamati Kuu kuchukua maamuzi magumu.
Baraza Kuu libariki tu maamuzi ya Kamati Kuu.