Albert Msando apotoka tena

Chadema inapaswa kujivunia kuwa na vijana kama Msando.

Hapa CCM ina jambo la kujifunza.

Cc Ritz VUTA-NKUVUTE Ng'wamapalala
Tatizo la CHADEMA imejaza vijana ambao wengi wao wanasumbuliwa na inferiority complex na katika kukabiliana na hali hiyo, inawabidi wawe wapiga majungu na kujipendekeza kwenye CHADEMA party machinery as a "survival of the fittest".

Nimepatwa na butwaa na pia kicheko kusikia wengine wanadai wana 'uwezo' wa kushawishi viongozi waliopewa majukumu ya kiuongozi ili kuongoza kwa misingi ya katiba inayoainishwa katika kanuni, maadili na itifaki ili waitishe mkutano wa Baraza Kuu kwa nia ya kuwapokonya baadhi ya wanachama kadi za chama kwa vile tu mitazamo yao ni tofauti na wao.

This is intimidating, threatening in order to induce someone to bend to their twisted politics. Huu ni udikteta wa kiwango cha juu kabisa kama kweli hilo wazo litatimizwa. Hii inatuambia kwamba Kadi ya CHADEMA inauzwa kwa watu ambao hawana mawazo na fikra huru.

Siasa za Tanzania zimejaa personal hatred na ni janga kwa kizazi hiki na kinachokuja.
 
dah! pole sana mkuu bila shaka umejifunza kiswahili ulipokuja mjini inavyoelekea hujui matumizi ya msamiati 'haraka' hebu tafuta mtoto wa secondary anayesoma masomo ya kiswahili akufundishe ngeli za majina, zipo tisa tu mkuu hata hutapata shida saana kuzielewa!
Kweli we kianzi,hicho kiswahili umejifunzia mombasa,kwa hiyo kama haraka ni 'kitu' kwenda speed/kasi isiyo ya kawaida hata gari likipita speed au ndege au jiwe tunasema linaharaka,rudi shule we kilaza ukasome tena kiswahili..
 
Huu upuuzi wenu unaligharimu taifa ,hebu ninyi mawakili na wanasiasa uchwara jitegemeeni kiakili simamieni mnachokiamini kwa misingi husika na sio huu uvuvuzera mnaotuletea humu mitandaoni aisee .

Kama zito anaona hajatendewa haki afuate taratibu husika au kama vp anyooshe goti na kama kamati kuu ya CDM itaona yafaa kumrudisha kijana wao kundini kwakujiridhisha kua hata sababisha madhara kwa uwepo wake chamani bora ikae nae mezani mambo yaishe sio kila siku kusikia hivi vimipasho kama tupo pemba aisee . (wakati fulani maamuzi magumu hua msaada sana kwa watu makini )
 
Umaarufu unadhani utanisaidia nini Mkude? Sihitaji umaarufu hata kidogo. Mbona haukusema haya wakati nilipomtetea Mh. Mbowe; Mh. Ndesamburo; Mh. Nassari; Mh. Lema nk kwenye kesi zao?

Kwa hiyo ghafla nakuwa kenge nikitetea Kanuni na Katiba ya chama kisa tu anayehusika ni Zitto?

Naamini kwenye hukumu na adhabu kwa mujibu wa Katiba na Kanuni. Niko tayari kuadhibiwa, kutukanwa, kudharauliwa, kuonekana mjinga nk lakini Katiba na Kanuni LAZIMA ziheshimiwe na kufuatwa.

elezea pia namna ambavyo uliwasaliti mpaka walipokushitukia na kukutoa nduki...
 
Mdogo wangu kwanza wewe unapaswa kujitibia hiyo identity crisis uliyonayo. Pili sijawahi kuficha ukaribu wangu na Zitto. Ni wewe ndiye unayeshindwa kujitambulisha kama mfuasi mkubwa wa genge la Mbowe na mdau wake wa mud Dr Slaa na kuwa wewe CHADEMA ni chama cha nyumbani ambacho kinapaswa kulindwa kuingia mikononi mwa wakuja ambao kwenu ninyi wao wapo kwa ajili ya kutumika tu na sio kuongoza chama. Tatu, nadhani kama unafiki wewe ndiye sura ya unafiki katika siasa za CHADEMA na ndizo unazitegemea kujenga nafasi yako ndani ya chama pamoja na uchaga wako ukiamini kuwa CHADEMA ambao unaamini ndio asset kubwa kwako kisiasa ndani ya CHADEMA. Angalao mimi ni msaidizi wa Dr Salim kama unavyosema lakini wewe ni mpambe wa Mama Josephine aka mwenza wa Dr Slaa. Angalao hata ungekuwa Msaidizi wa Dr Slaa mwenyewe ungeweza kuwa na uhalali wa kuhoji kazi yangu ambayo wengi wenu mnaiotea ndoto. Kama mlizoea kutengeneza uongo na watu wakawaangalia tu huku wakiamini busara ya kukaa kimya ingeliweza kuokoa chama, hapa mlipofika mmepoteza nguvu hiyo. Ni tit for tat inakuja soon....

Kwanza,Niombe radhi kwa kunihusisha na rhetorics zako za ukabila.Siku zote unajenga hoja kwa misingi ya kikabila na kidini.Hiyo ndio common denominator kati yako na unaiwaita maswahiba wako.

Mimi "Mdogo wako" (Kwa reference yako) ninapata fedheha sana kuona kaka zangu walionizidi umri na uzoefu wa kisiasa(Weledi wa Kitaaluma hauhusishwi) mnaegemea katika siasa za kijinga kama hizi.

Pili,Sijawahi kuwa msaidizi wa mtu binafsi.Na siwezi kujivunia kuwa msaidizi wa mtu binafsi kama unavyojinadi wewe.Kama hii sio maana halisi ya mtu mwenye tatizo la 'Identity Crisis" basi msamiati huu wa Kiingereza unatumika vibaya

Tatu,Kusimamia misingi ya CHADEMA kama chama cha siasa sioni aibu hata kidogo.Wewe unaona fahari kusimamia uswahiba juu ya misingi ya kikabila na kidini.Nonesense!

Nne,Tangu nikiwa mdogo nimekua nikipenda harakati za upinzani hasa NCCR-Mageuzi na Baadae CHADEMA.Je, nilikipenda NCCR-Mageuzi kwa kuwa ni chama cha nyumbani?

Tano,Falsafa ya Chura kuwa ndani ya bwawa alikoweka makazi ndio dunia nzima inakusumbua sana acha kufuata falsafa hii maana wewe ni binadamu mwenye utashi na maarifa.Sijawahi kutamani nafasi ya kuwa msaidizi wa mtu binafsi.Kwa mtazamo wako huu wa kujifariji unaonyesha jinsi ulivyo na ambition ndogo.You must be aiming too low.

Sijawahi kuwa na ambition ya kubebea watu mikoba.Nafedheheka sana unaponiita "Mdogo wako" lakini huwezi ku-reason according to your age.

Ungekua kaka yangu niliyezaliwa tumbo moja nawe ningekushauri politely,ikishindikana kwa ukali na kama ungeendeleza mentality hii ningeku-disown.

Usiidhalilishe familia kwa kauli za kijinga kama hizi kwenye public arena.Mume wa mtu na baba wa familia una ambition za ovyo kama hizi?And you are just proud of this? Goshhhh! ! !

Eti kuna maprofesa walikaa darasani na kujivunia kuwa na dumb product kama hii?Kuna classmates wanaoweza kutaja hadharani kwa ujasiri kuwa na historia ya kitaaluma na wewe?

Namuonea Huruma Dr.Salim.Heshima yangu kwake iko pale pale kwa kile ambacho amekua akifanya kwa Tanzania na Afrika.Post yangu hii isitumike kumuhukumu.
 
Nimesoma post zote toka mwanzo mpaka hapa naandika nimegundua mambo muhimu ambayo wengi hawayafahamu.
  1. Wengi wenu mmekariri sura ya sita kipengele (a) -(d) bila kujua nini kinaongelewa ndani yake.
  2. Kushindwa (akiwemo msando na zitto) kutoifautisha kati ya kufukuzwa uachama na uongozi.

UKWELI WA SURA YA SITA KANUNI ZA UENDESHAJI KAZI ZA CHAMA

Sura ya sita inahusiana na UANACHAMA (ADHABU ZA KINIDHAMU AU KUFUKUZWA CHAMA).

Nanukuu

"6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za
kinidhamu:-

6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama wa tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.

6.5.2 Kwa mujibu wa ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:

(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
(b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
(c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.

d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.

6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa kifungu 5.4 cha Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.

6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.

6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
6.5.5.Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.

6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.

6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kuKata rufani au la.
6.5.9 Mwadhibiwa atakaye amua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.

6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya
kikao cha maamuzi. " mwisho wa kunukuu

SASA TUONE IBARA YA 5.4.3 NA 5.4.4 INASEMAJE

Nanukuu

"5.4 Kukoma kwa UanaChama

5.4.1 Kwa kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake.
5.4.2 Kutokana na kufariki.
5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama. Mwanachama atakuwa na haki ya kuKata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na adhabu hiyo.

5.4.4 Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha katiba, Kamati Kuu inaweza kumwachisha ama kumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na kanuni za Chama.

5.4.5 Kukosa sifa za uanachama.
5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa nidhamu."

Mwisho wa kunukuu

ANGALIZO KUHUSU UONGOZI NA KUKOMA KWAKWE KWA MUJIBU WA KATIBA

Nanukuu

"6.3.4 Kukoma kwa Uongozi

(a) Kwa kiongozi kujiuzulu kwa hiari yake
(b) Kwa kiongozi kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama
(c) Kwa kiongozi kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya katiba, kanuni au maadili ya Chama.
(d) Kwa kufariki
(e) Ibara hii inahusu pia uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ya Chama.

6.3.6 Mamlaka za Nidhamu na Uwajibishaji

(a) Kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu ataweza
kusimamishwa uongozi tu kama ifuatavyo:-
(i) Kiongozi ngazi ya Msingi na Kamati Tendaji ya Tawi
(ii) Kiongozi wa Tawi na Kamati ya Utendaji ya Kata/Wadi
(iii) Kiongozi wa Kata/Wadi na Kamati ya Utendaji ya
Jimbo/Wilaya.
(iv) Kiongozi wa Jimbo/Wilaya na Baraza la Mkoa
(v) Kiongozi wa Mkoa na Kamati Kuu.
(vi) Kiongozi wa Taifa na Baraza Kuu.
Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza
kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua.
(c) Bila kuathiri masharti ya vipengele (a) na (b) hapa juu, kiongozi yeyote anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao cha juu ya ngazi yake ya uongozi.
(d) Kiongozi aliyechukuliwa hatua za nidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile ya mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho.
(e) Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu.
(f) Viongozi wa ngazi ya kitaifa waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wanaweza kusimamishwa uongozi endapo theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza Kuu watapiga kura ya siri na kutokuwa na imani na kiongozi mhusika. Baraza Kuu litakuwa na wajibu wa kuteua atakayeshika nafasi hiyo kwa muda hadi uamuzi wa mwisho kufanywa na Mkutano Mkuu."

Mwisho wa kunukuu

HITIMISHO

  1. Kuhusu kuwavua au la uachama watuhumiwa , CHADEMA imefuata taratibu zote hapo ju. Zitto na wenzie wasubiri kuitwa na kamati kuu kwa mahojiano ya ana kwa ana. Baada ya hapo watapewa majibu ya maamuzi ya kamati kuu kwa maandishi ndani ya siku 14 toka mahojiano. Wanaweza kukata rufaa kama hawajaridhika na maamuzi
  2. Kuhusu kuvuliwa uongozi chadema walitumia katiba ibara ya 6.3.4 (c). Hili watuhumiwa waliitwa, wakahojiwa na kamati kuu, wote kwa pamoja wakakiri makosa kwa kuhusika na waraka wakaomba kujiuzuru nyazifa zao.
  3. Wanadai taratibu hazikufuatwa kuwapoka vyeo vyao. Ukivunja katiba na miiko ya uongozi hakuna cha taratibu, katiba iko wazi unapoteza wadhifa ulionao mara moja pamoja na kuchuliwa hatua zingine ikwemo kuvuliwa uanachama ambazo taratibu kwenye hili lazima zifuatwe kama ilivyoainishwa hapo juu.

CC: Albert Msando

Hakika hapa UMEMFANYA HAKUNA(KAUWOSHI) Yani hakuana RANGI HATA ACHA ONA.

Ndugu upo UFIPA nini au wewe ndio LISU ?
 
Tatizo la CHADEMA imejaza vijana ambao wengi wao wanasumbuliwa na inferiority complex na katika kukabiliana na hali hiyo, inawabidi wawe wapiga majungu na kujipendekeza kwenye CHADEMA party machinery as a "survival of the fittest".

Nimepatwa na butwaa na pia kicheko kusikia wengine wanadai wana 'uwezo' wa kushawishi viongozi waliopewa majukumu ya kiuongozi ili kuongoza kwa misingi ya katiba inayoainishwa katika kanuni, maadili na itifaki ili waitishe mkutano wa Baraza Kuu kwa nia ya kuwapokonya baadhi ya wanachama kadi za chama kwa vile tu mitazamo yao ni tofauti na wao.

This is intimidating, threatening in order to induce someone to bend to their twisted politics. Huu ni udikteta wa kiwango cha juu kabisa kama kweli hilo wazo litatimizwa. Hii inatuambia kwamba Kadi ya CHADEMA inauzwa kwa watu ambao hawana mawazo na fikra huru.

Siasa za Tanzania zimejaa personal hatred na ni janga kwa kizazi hiki na kinachokuja.

Siasa za Tanzania zilizojaa personal Hatred zimejengwa na watawala na chama tawala kwa kutoandaa mazingira ya kisasa kwa siasa za upinzani.Funny enough waliotufikisha hapa wanawatumia baadhi ya watu miongoni mwetu kuendeleza mfumo huu wa kinafiki.CHADEMA na wanachama wake hawapaswi kulaumiwa!Bali wale wanaotumiwa na mfumo uliotufikisha hapa na wewe unayeelekeza lawama sehemu isiyo sahihi
 
dah! pole sana mkuu bila shaka umejifunza kiswahili ulipokuja mjini inavyoelekea hujui matumizi ya msamiati 'haraka' hebu tafuta mtoto wa secondary anayesoma masomo ya kiswahili akufundishe ngeli za majina, zipo tisa tu mkuu hata hutapata shida saana kuzielewa!
Kumbe kiswali kinafundishwa mjini ndio ulikofundishwa matumizi ya neno haraka,wewe ndio wale wa chimbo..
 
wana jf,

naomba ieleweke kuwa katiba ya chadema toleo la mwaka 2006 ndiyo msingi mkubwa wa kuendesha taasisi. ufafanuzi uliotolewa leo kwa vyombo vya habari na wakili albert msando ni upotoshaji mkubwa wa katiba ya chadema na hii inatokana na aidha uelewa mdogo wa katiba hiyo na/ au ni makusudi kwa malengo ya huyo anayedai kumwakilisha.

upotoshaji huo ni kama ufuatayo;

mosi, hatua iliyochukuliwa kamati kuu kumsimamisha uongozi huyo anayedai kumwakilisha ilifikiwa kwa lengo moja tu la kunusuru chama kama hatua ya dharura kwa mujibu wa ibara ya 6.5.2 ya kanuni za uendeshaji kazi za chama pamoja na marekebisho ya mwaka 2013 ili kuruhusu utaratibu wa kinidhamu wa kawaida kwa mujibu wa katiba na kanuni.
itakuwa ni taasisi ya ajabu ambayo itasubiri madhara makubwa ya uharamia uliokuwa unataka kufanyika alafu kamati kuu kama chombo cha kusimamia utendaji wa sekretarieti ikae kimya alafu wahaini waendelee kuutumia mwanya wa kikanuni kuharibu na kuathiri taasisi nzima. hata hivyo kanuni ipo kimya kuhusu dhana ya dharura, lakini kisheria dharura ni kutokana hali husika katika wakati huo au kutokana na mazingira yaliyopo (prevailing circumstance).

pili, kuhusu kupatiwa taarifa kamili ya mwenendo wa kikao cha kamati kuu kama ambavyo amedai kuwa mpaka sasa yeye na huyo anayemwakilisha hawajapokea, amepotoka kabisa. Kanuni aliyonukuu ambayo ni ibara ya 6.5.10 ya kanuni za uendeshaji kazi za chama inatamka kuwa taarifa kamili ya mwenendo itawasilishwa kwenye kikao cha juu. Suala hapa ni je msando amekuwa kikao cha ngazi ya juu pamoja huyo anayedai kumwakilisha?

tatu, kuhusu anayedai kumwakilisha kutotajwa kwenye waraka wa uhaini na hivyo kutokuwa na makosa ni jambo ambalo linaingia kwenye maudhui na hoja ambazo anayedai kumwakilisha anatakiwa kuzijibu katika muda aliopewa na kikao cha kamati kuu na hivyo hatua yake ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari ni aina ya utoto na kutaka msamaha/huruma ya umma (public sympathy) na kuendeleza mjadala usio na tija kwa vyombo vya habari.

nne, wakili msando ameshindwa kutoa dhana ya anayedai kumwakilisha kupewa mashtaka na kutakiwa kujibu ndani ya siku 14. Je haikidhi matakwa ya kikanuni kama alivyoainisha?

tano, anayedai kumwakilisha anakwepa kujibu tuhuma 11 zilizoainishwa katika hati ya mashtaka ili baada ya maamuzi, na kama hataridhika na maamuzi akate rufaa.

sita, itakuwa ni taasisi ya ajabu ambayo inaona hujuma kubwa dhidi yake alafu iache kuchukua hatua za dharura kujinusuru.

saba, ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya katiba ya chama toleo la mwaka 2006 ikisomwa pamoja na marekebisho ya kanuni za uendeshaji kazi za chama ya mwaka 2013, vifungu vyote hivyo vinazungumzia hatua za kuvuliwa uanachama. Ikumbukwe kuwa hatua zilizochukuliwa ni za kiuongozi na sio kumvua uanachama huyo anayemwakilisha. Hata hivyo hati ya mashtaka pamoja na agizo la kujibu ndani ya siku 14 imekidhi utaratibu wa kikanuni kama anavyodai wewe.

nane, ieleweke kuwa wakili msando ni diwani wa chadema katika akiwakilisha kata ya mabogini huko moshi. Naomba arejee kanuni za madiwani ibara ya 5.0 (d) ambayo naomba kuinukuu "diwani anawajibika kutumia hadhi, uwezo, wadhfa na nafasi aliyonayo kama diwani kukijenga chama ndani na nje ya halmashauri". kama wakili naamini anajua hatua za kuchukua akiendelea kukomalia suala hili, nimkumbushe tu kuwa anatakiwa ajiuzulu hiyo nafasi ili kuondoa mgongano wa kimaslahi na afanye kazi yake ya uwakili kama anataka kuendelea na kushiriki kupinga maamuzi ya kamati kuu.

naomba kuwasilisha.

mwaikenda

=========================
majibu kutoka kwa albert msando
=========================

inavyoonekana hapa chadema ina mamluki wengi sana.zitto aliachiwa kwa muda mrefu sana kutengeneza mtandao wake.ndio hao wanajitokeza sasa.eti diwani wa chadema anatetea usaliti ndani ya chama?na anapingana na maamuzi ya kamati kuu?nawaomba sana wanacdm wawe macho sana sasa hivi watawajua mmoja mmoja.kumbe tulikuwa tunafuga nyoka wengi wenye sumu.ninachojiuliza kwa nini ccm inatumia mbinu hizi haramu kupambana na chadema?ndio kusema imeshindwa kabisa majukwaani?hivi kweli haioni madhara yake kwa chama cho na kwa taifa.kweli haioni?
 
Labda vijisent vya uswiz teh teh teh
its surprises me a lot, Msando sijui imekuaje amevaa hii njuga

haina tija kwake wala kwa taifa, its just a bad lead kwa siasa za leo hasa vijana na hasa hasa vijana wa upinzani
 
Ukomavu wa siasa ni kupingana kwa hoja siyo matusi jenga hoja.

Hivi huwa unasoma post kweli au ukiona jina langu unakimbilia kujibu kuwa nimetukana kwa taarifa yako nimepunguza kama moderator wataendelea kuwashughulikia wanao anzisha matusi...
 
Hivi huwa unasoma post kweli au ukiona jina langu unakimbilia kujibu kuwa nimetukana kwa taarifa yako nimepunguza kama moderator wataendelea kuwashughulikia wanao anzisha matusi...

MsandoAlberto hakuna rangi utaacha kuona mwaka huu!
 
Last edited by a moderator:
Kwanza,Niombe radhi kwa kunihusisha na rhetorics zako za ukabila.Siku zote unajenga hoja kwa misingi ya kikabila na kidini.Hiyo ndio common denominator kati yako na unaiwaita maswahiba wako.

Mimi "Mdogo wako" (Kwa reference yako) ninapata fedheha sana kuona kaka zangu walionizidi umri na uzoefu wa kisiasa(Weledi wa Kitaaluma hauhusishwi) mnaegemea katika siasa za kijinga kama hizi.

Pili,Sijawahi kuwa msaidizi wa mtu binafsi.Na siwezi kujivunia kuwa msaidizi wa mtu binafsi kama unavyojinadi wewe.Kama hii sio maana halisi ya mtu mwenye tatizo la 'Identity Crisis" basi msamiati huu wa Kiingereza unatumika vibaya

Tatu,Kusimamia misingi ya CHADEMA kama chama cha siasa sioni aibu hata kidogo.Wewe unaona fahari kusimamia uswahiba juu ya misingi ya kikabila na kidini.Nonesense!

Nne,Tangu nikiwa mdogo nimekua nikipenda harakati za upinzani hasa NCCR-Mageuzi na Baadae CHADEMA.Je, nilikipenda NCCR-Mageuzi kwa kuwa ni chama cha nyumbani?

Tano,Falsafa ya Chura kuwa ndani ya bwawa alikoweka makazi ndio dunia nzima inakusumbua sana acha kufuata falsafa hii maana wewe ni binadamu mwenye utashi na maarifa.Sijawahi kutamani nafasi ya kuwa msaidizi wa mtu binafsi.Kwa mtazamo wako huu wa kujifariji unaonyesha jinsi ulivyo na ambition ndogo.You must be aiming too low.

Sijawahi kuwa na ambition ya kubebea watu mikoba.Nafedheheka sana unaponiita "Mdogo wako" lakini huwezi ku-reason according to your age.

Ungekua kaka yangu niliyezaliwa tumbo moja nawe ningekushauri politely,ikishindikana kwa ukali na kama ungeendeleza mentality hii ningeku-disown.

Usiidhalilishe familia kwa kauli za kijinga kama hizi kwenye public arena.Mume wa mtu na baba wa familia una ambition za ovyo kama hizi?And you are just proud of this? Goshhhh! ! !

Eti kuna maprofesa walikaa darasani na kujivunia kuwa na dumb product kama hii?Kuna classmates wanaoweza kutaja hadharani kwa ujasiri kuwa na historia ya kitaaluma na wewe?

Namuonea Huruma Dr.Salim.Heshima yangu kwake iko pale pale kwa kile ambacho amekua akifanya kwa Tanzania na Afrika.Post yangu hii isitumike kumuhukumu.

Sawa wewe mwenye ambition ya kubeba majungu ya Mama Josephine Mushumbuzi aka Mwenza wa Dr Slaa na kujikweza kwako kujifanya unjua siasa huku utaalamu pekee ulio nao ni kubeba majungu na kuyasambaza kwa ajili ya nafasi. Mwenzio najua umuhimu wa kujifunza na kujishusha na pia sina ulimbukeni wa nafasi kwani maisha yangu yamekuwa ya nafasi nyingi tu ambazo sina haja ya kujigamba nazo lakini niko tayari kujigamba na nafasi za kubeba mafaili na kuelimika kwa wenye elimu, uzoefu na heshima na sio kwa ajili ya nafasi tu kama wewe. Naona udini na mkabila unakuwa mbaya tu pale ambapo unatuhumiwa lakini ni assent pale unapotumika kujijenga... hilo sio tatizo lako pekee, ni tatizo la kibinadamu ambalo kwa wenye akili fupi wanaweza kudhani ni ukawaida wa binadamu lakini ukijengeka kwa fikra ambazo zinapatikana kwa kuwabebea mafail wenye upeo wa juu, huwezi kukubaliana na ukawaida huo na utakuwa tayari kuupiga vita hata pale ambapo unakusaidia wewe. Mdogo wangu Ben ambaye sikujui hata kwa sura, jifunze kujishusha kunalipa, yawezekana sio kimaslahi lakini kifikra... ukombozi wa kifikra ndio hatua muhimu ya ukombozi wa kimaisha. Hata hivyo sikushangai sana maana trait yako ni ya kawaida kwa wenye kugubigwa na ulimbukeni uwe wa kimali au kinafasi, kunakufanya ujione ni muhimu sana ndani ya CHADEMA wakati umuhimu wako unaishia katika kutumika tu tena na watu wasio na chembe ya integrity... Mimi sina ndoto za kuwa fulani, nina ndoto za kuchangia kubadili nchi yangu kufanikisha ujenzi wa Tanzanianjema. Natambua kwako ni vigumu kuelewa hilo.
 
inavyoonekana hapa chadema ina mamluki wengi sana.zitto aliachiwa kwa muda mrefu sana kutengeneza mtandao wake.ndio hao wanajitokeza sasa.eti diwani wa chadema anatetea usaliti ndani ya chama?na anapingana na maamuzi ya kamati kuu?nawaomba sana wanacdm wawe macho sana sasa hivi watawajua mmoja mmoja.kumbe tulikuwa tunafuga nyoka wengi wenye sumu.ninachojiuliza kwa nini ccm inatumia mbinu hizi haramu kupambana na chadema?ndio kusema imeshindwa kabisa majukwaani?hivi kweli haioni madhara yake kwa chama cho na kwa taifa.kweli haioni?

Mkuu huyu Mwanasheria wa zitto Arusha tuna mjua ni mwizi kama ana bisha aje hapa akanushe kama hakuiba mil 60 za Nyaga ambazo alipewa za ujenzi wa barabra ya kutoka Dodoma Road mpaka ofisi za Nyaga, Licha ya kutuzwa kama mke wa jamaa lakini jamaa alimwimbia hapo kijana kanunuliwa gari, kapewa nyumba iliyoko njiro nyuma ya Njiro Complex..Huyu mwanasheria uchwara alitaka kuwauza akina mbowe,Dr Slaa, Lema,Ndesa wakamshitukia waka mkataa.....Huyu hana tofauti na Zitto kwani naye aliwahi kufanyiwa mema tu na Mbowe lakini amegeuka kutangaza ubaya wa Mbowe mbaya zaidi ni wa uongo....
 
Ninyi na kauli mbiu zenu. Ukiulizwa usaliti upi huna majibu utabaki kuimba ngonjera za riwaya za kina Kubenea na wehu kama Yericko Nyerere... ukiulizwa una ushahidi gani huna cha kujibu. Kuna usaliti kama wa viongozi wenu walioingia mkataba wa mashirikiano na kinara wa mfumo fisadi endapo atanyimwa nafasi ya kugombea CCM?
 
Sawa wewe mwenye ambition ya kubeba majungu ya Mama Josephine Mushumbuzi aka Mwenza wa Dr Slaa na kujikweza kwako kujifanya unjua siasa huku utaalamu pekee ulio nao ni kubeba majungu na kuyasambaza kwa ajili ya nafasi. Mwenzio najua umuhimu wa kujifunza na kujishusha na pia sina ulimbukeni wa nafasi kwani maisha yangu yamekuwa ya nafasi nyingi tu ambazo sina haja ya kujigamba nazo lakini niko tayari kujigamba na nafasi za kubeba mafaili na kuelimika kwa wenye elimu, uzoefu na heshima na sio kwa ajili ya nafasi tu kama wewe. Naona udini na mkabila unakuwa mbaya tu pale ambapo unatuhumiwa lakini ni assent pale unapotumika kujijenga... hilo sio tatizo lako pekee, ni tatizo la kibinadamu ambalo kwa wenye akili fupi wanaweza kudhani ni ukawaida wa binadamu lakini ukijengeka kwa fikra ambazo zinapatikana kwa kuwabebea mafail wenye upeo wa juu, huwezi kukubaliana na ukawaida huo na utakuwa tayari kuupiga vita hata pale ambapo unakusaidia wewe. Mdogo wangu Ben ambaye sikujui hata kwa sura, jifunze kujishusha kunalipa, yawezekana sio kimaslahi lakini kifikra... ukombozi wa kifikra ndio hatua muhimu ya ukombozi wa kimaisha. Hata hivyo sikushangai sana maana trait yako ni ya kawaida kwa wenye kugubigwa na ulimbukeni uwe wa kimali au kinafasi, kunakufanya ujione ni muhimu sana ndani ya CHADEMA wakati umuhimu wako unaishia katika kutumika tu tena na watu wasio na chembe ya integrity... Mimi sina ndoto za kuwa fulani, nina ndoto za kuchangia kubadili nchi yangu kufanikisha ujenzi wa Tanzanianjema. Natambua kwako ni vigumu kuelewa hilo.

Naona una utani na MACCM na hasa dr.dr.dr.dr. KIKWETE
 
Mkuu huyu Mwanasheria wa zitto Arusha tuna mjua ni mwizi kama ana bisha aje hapa akanushe kama hakuiba mil 60 za Nyaga ambazo alipewa za ujenzi wa barabra ya kutoka Dodoma Road mpaka ofisi za Nyaga, Licha ya kutuzwa kama mke wa jamaa lakini jamaa alimwimbia hapo kijana kanunuliwa gari, kapewa nyumba iliyoko njiro nyuma ya Njiro Complex..Huyu mwanasheria uchwara alitaka kuwauza akina mbowe,Dr Slaa, Lema,Ndesa wakamshitukia waka mkataa.....Huyu hana tofauti na Zitto kwani naye aliwahi kufanyiwa mema tu na Mbowe lakini amegeuka kutangaza ubaya wa Mbowe mbaya zaidi ni wa uongo....

Tatizo lenu ndio hilo mnaamini kuwa mtu akikusaidia wakati fulani basi ni lazima ugeuke kuwa ndondocha wake hata pale anapofanya mambo ya kishenzi kabisa. Wote ni victims wa fikra za siasa za matumbo ndani ya CHADEMA halafu mnajifanya kuwa mnapambana na siasa za matumbo za CCM. Bila ya Zitto Mbowe angeweza kufanya mabadiliko ya CHADEMA kuanzia miaka ya 2004 hadi 2006 yaliyopelekea rejuvination ya chama hicho baada ya miaka mitano ya kumsusia chama Mzee Mtei ambaye alikuwa chaguo la wanachama dhidi ya chaguo la wenye chama Mzee Ndsamburo. Bila ya Zitto huyo mbowe anayejitapa kumsaidia, which is true in a way, angekuwa anamiliki mali yoyote hivi sasa kama angefilisiwa na NSSF kwa deni analokataa kulilipa kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Na mangapi Zitto amemsaidia kisiasa na hata kijamii ikiwemo kuokoa ndoa yake ambayo sasa ndio inaelekea kaburini? Jikomboeni na hili janga la fikra za siasa za matumbo (patronage) ndani ya chama kwanza ndio mjinadi upambanaji wa kitaifa.
 
Hizi siasa za character assassination haziwezi kuisaidia CHADEMA na taifa kwa ujumla na kikubwa kabisa hii huwa ni dhambi kubwa sana katika siasa na haiwezi kuisha pindi ikitendwa. Ni sawa na kula nyama ya binadamu.

Kutaka kulazimisha mawazo na mitazamo ya watu wengine lazima iwe kama ya kwako ni dalili ya udikteta kwa kiwango cha juu kabisa.

Ni ukosefu wa fikra pevu na uduni wa mitazamo kuanza kumshambulia wakili kwa vile unamuwakilisha mteja ambaye mnapingana naye kisheria. Toka lini kwenye jamii yanye fikra pevu mjumbe akauwawa.

Kuna baadhi ya watu wangefurahi sana kama Mh. Zitto asingepata wakili katika shauri lake, kitu ambacho kinaenda kinyume na misingi ya demokrasia na usawa wa binadamu kama ulivyoainishwa katika katiba ya nchi kwenye kipengele cha 13(1-3).

Hawa hawa wanaosema Albert Msando anapingana na katiba, kanuni na itifaki za chama kwa kumtetea Mh. Zitto wanasahau kama Mh. Zitto bado ni mwanachama wa CHADEMA na kiongozi wa wananchi achilia mbali haki yake ya msingi kama raia inayolindwa na pia na Presumption of innocence katika macho ya sheria.

Kwa mawazo haya, hamuwezi mkasema mnasimamia misingi ya demokrasia na haki za binadamu wakati maamuzi ya kisheria na kikanuni mnataka/mnapenda yafanyike kwa mtindo wa kangaroo court.

Mbona conflict of interest inaonekana kwa Albert Msando tu wakati kuna viongozi kama Mabere Marando ambaye alikuwa anatetea mafisadi ambao chama kiliwataja na kusema ni maadui wakuu wa ustawi wa nchi lakini hakuna aliyepaza sauti kumkemea ili asiwatetee.

Mbona baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanatumia majukwaa ya kisiasa mikoani kuelezea hatua zinazochukuliwa na chama kuhusiana na sakata hili lakini Mh. Zitto akisema hatua anayochukua mbele ya wananchi kupitia press conference inakuwa ni nong'wa. Kwani mnataka na yeye aanze kufanya ziara za mikoani kwa kupitia njia ya "kuimalisha chama"

Mbona baadhi ya viongozi na wanachama wanaofahamika wa CHADEMA wanaanzisha thread hapa kila wakati kuhusiana na swala hili hakuna kiongozi au Mwanachama anayewanyoshea kidole.

Pambaneni katika hoja zinazohusiana na misuguano ya kikatiba, kikanuni na kiitifaki na siyo katika human character. Nje ya hapo ni dalili ya kushindwa katika hoja.

Hizo mbona mbona nyingi ni dalili ya kukosa umakini, kama kawaida yako hujifanya una point na uko makini kumbe zero!
Ni wewe na wenzako mara nyingi mnalaumu CDM eti kama CCM wanafanya kosa fulani sio passport ya CDM nayo kufanya, inatakiwa ijipambanue na iwe mfano. Sasa kwa huyu Bwana Msando kumtetea umeweka misururu ya mbona nyingi tu mara baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanatumia majukwaa ya kisiasa, mbona baadhi ya viongozi na wanachama wanaofahamika wa CHADEMA n.k. Toa hoja madhubuti ya kumtetea sio mbona, mbona.
Albert ni Diwani kwa nini asijiuzulu kwanza ndio apambane na Kamati Kuu, sasa tuanzie hapo acha longolongo!
 
ZZK hafit kuwa kiongozi wa CDM; mitaa hii tunahitaji kiongozi makini mtulivu mvumilivu na asiyekurupuka. Mitaa hii mishale ni mingi sana kutoka CCM, Usalama, polisi, na serikaalini , bungeni nk. Ukiwa na kiongozi kama ZZK ambaye ana hasira muda wote, chuki na wahauri kama Msando ambao wanakurukupuka na kupumulia nguvu ya fedha huwezi kushinda vita. Ndio maana ZZK ana Diwani Mmoja tu jimboni kwake baada ya kuwa mbunge na Naibu katibu Mkuu takribani miaka 7 sasa.

Huku site tunasema ZZK anafaa kuhamasisha tu. Uongozi hauwezi, kama huwezi huvumilia, kama huwezi sikiliza, ushauri umekushinda. Nikinukuu waraka wao wenyewe ambao waliuuandika " ZZK ni mtu wa kukurupuka, kupanic na kujibu pasipo hitajika au bila kujali hadhira, anapapara, kiburi, na kudhira" mwisho wa kunukuu waraka wa mabadiliko 2013 by Dr K.
 
Back
Top Bottom