Albert Msando afunguka kuhusu Zitto Kabwe

Albert Msando afunguka kuhusu Zitto Kabwe

Mwanasheria ambaye pia ni diwani kupitia CHADEMA, Ndugu Albert Msando amehoji yafuatayo;

1. Amehoji je, kama
CHADEMA kinasema ni Cha Kidemokrasia kwanini kinaaamuru Afukuzwe tu kwa kuwa ameenda mahakamani?

2. Amehoji je, ni nani mwenye mandate ya kumvua mwanachama uanachama wake.

3. Je, uamuzi wa kumvua uanachama ulipaswa kutangulia kwa umma au kwa Zitto kwanza?

4. Amehoji je, imekuwaje mtu anayesimamia sakata la Escrow afukuzwe kwa sasa?

5. Amesema pia kuwa Zitto hana haja ya kubaki
CHADEMA kwa kuwa hata akiomba kubaki haitakuwa na mashiko. Pia ameuliza itakuwaje akae meza moja na Tundu Lissu,Wakati Tundu Lissu anatangaza amesema walishamfukuza toka mwaka jana. Naye anaona kuwa Zitto hahitajiki CHADEMA.

6. Pia amesema lengo la kumfukuza Zitto limefanywa kinafiki tu.

7. Amesema kuwa haoni haja ya kulazimisha kila mtu awaze kama Tundu Lissu au Mbowe au Slaa.

9. Pia amesema kuwa mgogoro huu ni funzo kwa Zitto, Wanachadema na Watanzania kujua aina ya viongozi walionao.Pia amesema kuwa migogoro hii isitumike kujenga chuki.

Chanzo: Clouds TV

ulitakaje
 
Kuna tatizo na hili kama watanzania wako makini inabidi liwe funzo kubwa. Watanzania wanahitaji chama mbadala cha kuwaletea matumaini. Na Mara nyingi pa kukimbilia huwa ni chadema Kwa Kuwa ndo tu chama kikubwa. Watanzania hatuna utamaduni wa kusoma kwani hata katiba yetu mama hatuijui. La hili linatakiwa liwe fundisho kwani wanasiasa ni watu hatari sana duniani kote. Tunahitaji tuzibebe katiba zote tuzisome ili tuzielewe. Chadema imeonyesha kwa namna mbali mbali Kuwa katiba yake imebakwa na viongozi wachache. Basi inaniaminisha Kuwa kwa kuwa sisi si wasomaji kuna kila uwezekano wa Kuwa na vipengele vya kuwaandaa akina Mugabe wa Tanzania kwani wanachama wameshajengewa utamaduni wa ndio mzee. Viongozi hawasemwi na hawaguswi na yeyote. CCM imetutawala na katiba yake tunaijua ila imechafuliwa na viongozi wake. Ni dhahri haina hizo chembe za ukandamizaji. Basi nawashauri watanzania wenzangu tuamke tuzisome katiba za vyama vyetu. Mpaka hapa nashindwa kuamini kwa dunia Ya leo kama kuna chama kinaweza Kuwa na katiba inayokandamiza utafutwaji wa haki. Na tumeshuhudia katiba ikibadirishwa kinyemela ,kwa Kuwa watanzania hawako serious wa nashindwa kupata message inayotumwa na hao wanaotaka utawala.na hii inatakiwa Kuwa message tosha kwani leo wanakandamizwa wanachama kesho utakuwa umma wote wa watanzania.

Nimekuelewa sana mkuu.....inatakiwa hii elimu nzuri uliotupa uiendeleze katika mahali unapotoka....naamin Tanzania bora itapatikana.....
 
wangemuacha mngesema anaogopwa,katimuliwa mnasema kaonewa!!!
 
Kama kweli ZZK anahusika na ACT ni wazi kuna tatizo, huwezi kuanzisha taasisi ndani ya taasisi nyingine tena kwa siri.
Wanaolifahamu hili na kulielewa wanajua kuwa huwezi kukaa na mwanachama wa namna hii. Ndio maana Mh. Kafulila alivyotofautiana na chama chake 'hakufungua ofisi' FB/Twitter bali aliomba msamaha na akasemehewa na sasa anajenga taifa.
Alafu kama huyu wakili kayaongelea haya kwenye hiyo radio ni wazi lao ni moja!

Wanazani CHADEMA ni CCM ambayo SAMWELI SITA na NAPE NAUYE walianzisha Chama wakiwa Bado CCM na wakafumbiwa Macho, CHADEMA ni zaidi ya Makini.

Nape aliwaiomba gombea jimbo la Ubungo kupitia CDM akiwa mwana chama wa CCM, chama cha majambazi wakafumba macho.

Mwambieni ZZK cdm si ccm
 
Albert Msando Mmmmh!!

Ukimya ungetosha tu kwenye hili.
 
Labda kama ningekutana na huyo Msando ningemuuliza kwanza....Yeye yupo Chadema na inaifahamu chedema kuliko sisi wengine ambao ambao hatupo huko...sasa Msando anaijua vizuri katiba ya chama chake? na anaielewa? ok kama anasoma hakuona hivyo vipengele ambavyo yeye leo anaona chama chake si cha kidemokrasia?
 
Hoja dhaifu kabisa na zisizo na mashiko kutoka kwa mtu ambaye ni ati ni mwanasheria. Na kama hoja zenyewe ndio hizi hata huyo Zito mwenyewe namuonea huruma kwa ushauri aliokuwa akipewa na kuupokea.
 
Naye si aondoke tu CHADEMA.

Analialia nini sasa?

Kesi mmeshindwa. Mteja wako kafukuzwa. Hivyo kulialia hakusaidii. Au analialia ili aonewe huruma?

Umefukuzwa, ondoka. Vyama vya kisiasa Tanzania si CHADEMA peke yake.

Kajiungeni na chama cha Dovutwa huko.
 
Msando kama anaona hakuna demokrasia CHADEMA kwanini yeye anaendelea kuwa mwanachama? si bora atafute chama kingine ambacho anaona kinatenda haki zaidi kadri anavyotaka yeye
 
CHADEMA watamkumbuka sana ZITTO.

Ni zaidi ya miaka miwili na zaidi sasa tokea CHADEMA iwe mbali na ZZK, kama hakukumbukwa kipindi chote hicho si rahisi kukumbukwa sasa wala badae. Hata angeendelea kuwepo ndani ya chama, mchango wake ulishapotea muda mrefu sana.

Hili suala limefikia lilipofika kwa sababu ZZK mwenyewe kaamua lifike hapo, angetaka lisingefika hapo. Mbona David Kafulila alikumbwa na tatizo kama lake, lakini sasa hivi yupo na anaendelea kuwepo ndani ya NCCR? Kafanya nini Kafulila ambacho ZZK kashindwa kufanya?

Nafikiri alitakiwa kutambua tokea mwanzo kuwa demokrasia ni sauti ya wengi hata kama hawapo sahihi. Inawezekana kweli kamati kuu wapo wrong, lakini tukumbuke kuwa wao ndio walioifikisha CHADEMA hapo ilipo na hivyo ili waendelee ni lazima wawe sauti moja.

Kama ndani ya kamati kuu kuna mtu ambae hakubaliani na ile sauti moja, basi si vibaya akitoka ili wanaokubaliana waendelee kwa namna ile ile wanayokubaliana. Ni vizuri atoke ili akaendeleze harakati zake sehemu nyingine, chama kiendelee kuwepo na yeye aendelee kuwepo. Bila shaka siku moja wote watakutana katika kujenga nchi yetu wakiwa vyama tofauti lakini vyenye lengo moja.
 
katiba ni chombo kilicho tungwa ili kusimamia haki na usawa hivyo yeyote ataye kiuka masharti ya katiba lazima katiba hiyo hiyo imwajibishe pole sana kamanda zitto kabwe
 
Back
Top Bottom