Al Jazeera: Watanzania wanaishi maisha ya hofu na mashaka katika utawala wa Rais Magufuli. Je, hili lina ukweli wowote?

Kama siyo mhalifu, hofu ya nini?
Watu wawili Kioanya, Zito ndiyo watanzania hao?
Utafiti was wapi huo? Au na All jazira wamekuwa poyoyo kama Tanzania Daima?

Hakuna chombo cha Tanzania kinatakiwa kutoa takwimu bila ridhaa ya serikali, na yoyote anayetoa takwimu isiyomfurahisha Yesu, anatekwa au anashughulikiwa, mfano mkurugenzi wa Twaweza, mpaka leo kaporwa paspoti kwa kuchapisha habari za kweli zisimfurahisha Yesu.
 
Kama ambavyo mh Mbowe alivyoshambuliwa hivi karibuni na kundi la wasio julikana na kuvunjwa mguu ama sivyo mkuu?

Ndio, na polisi mpaka sasa wanaishia kutoa ripoti ya kupika bila kutupa kilichorekodiwa kwenye CCTV Cameras.
 
Unamaanisha nini kutawaliwa bila ridhaa yao?

Chaguzi zote kunajisiwa ili wagombea wa ccm kutangazwa washindi. Toka ameingia madarakani, chaguzi zote kumefanyika, hujuma, ukatili na uhayawani wa wazi, na yote hayo ni maagizo yake. Watu wanakaa kimya sio kwa kuridhika, bali ni kuhofia maisha yao.
 
Ndio, na polisi mpaka sasa wanaishia kutoa ripoti ya kupika bila kutupa kilichorekodiwa kwenye CCTV Cameras.
Ila mkuu wewe unafurahisha sana, nimeamini sometimes siasa ni kitu kibaya sana.!
 
Kwa nini hawakwenda hoji raia wa kawaida kabisa mitaani?

Raia wa kawaida wanaogopa kutoa maoni yao kuepuka kukutana na mkono wa vyombo vya dola, au kundi la watu wasiojulikana. Ila huku mitandaoni raia wa kawaida tunafunguka vizuri. Kinachofanyika hivi sasa hapa nchini, ni kama mtu anambaka mtoto kisha anamtishia akisema atamuua.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Chaguzi zote kunajisiwa ili wagombea wa ccm kutangazwa washindi. Toka ameingia madarakani, chaguzi zote kumefanyika, hujuma, ukatili na uhayawani wa wazi, na yote hayo ni maagizo yake. Watu wanakaa kimya sio kwa kuridhika, bali ni kuhofia maisha yao.
Kwahiyo ndio anatawala bila ridhaa ya wananchi, kwani walio muweka madarakani ni kina nani mkuu?
 
Pamoja na hayo ila chadema na upinzani huu uchwara lazima wapotee kwenye sura ya siasa...

Watapotea kwenye bunge la makondoo, lakini sio kwa mapenzi ya wapiga kura, bali ni kupitia chaguzi za kishenzi.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Alzeera hawana akili walitakiwa kaandika baadhi ya watanzania waishi kwa hofu.Neno baadhi ni muhimu sababu ukisema watanzania kitakwimu ina maana ulihoji watanzania wote milioni sitini kitu ambacho Sio kweli sababu kuna watoto wachaga wasioweza jibu kitu,kuna wagonjwa wako ICU hawajui lolote,kuna wanaofaidika na utawala uliopo nk hiyo statement ya aluazeera haiko sahihi proffesionaly
 
Kama ambavyo mh Mbowe alivyoshambuliwa hivi karibuni na kundi la wasio julikana na kuvunjwa mguu ama sivyo mkuu?

Mmmh Mbowe alilewa akaanguka akitoka kwenye uzinzi na ulevi!

IMG_0430.jpg
 
Hivi Masoud Kipanya anaishi kweli kwa hofu? Mmmh napata shaka na hii habari hakika! Mbona yeye ndio anaongoza kumchora Magufuli kila leo na Magufuli alishasema hana shida yeyote ndio uhuru wa habari?

Siamini kama Masoud Kipanya kasema haya!
 
Kwahiyo ndio anatawala bila ridhaa ya wananchi, kwani walio muweka madarakani ni kina nani mkuu?

Unakaa madarakani kwa ridhaa ya kura za wananchi walio wengi iwapo wanaridhika na mifumo ya uchaguzi. Kama wananchi hawaridhiki na mifumo ya uchaguzi, huku tukishuhudia ukiukwaji mkubwa wa hata hizo sheria zilizopo kwa manufaa yake na chama chake, huwezi kusema unakaa madaraka kwa ridhaa ya wengi. Hata akina Elibashir, Mugabe nk walikuwa wanashinda chaguzi zao kwa kishindo, ila ilikuwa ni chini ya chaguzi zilizojaa Hadaa, ukatili na ushenzi wa hali ya juu. Hatua ya hizo chaguzi za kishenzi, hivi sasa watanzania tunazishuhudia kwa macho yetu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK

Similar Discussions

Back
Top Bottom