Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,592
- 11,830
Nikiwa kwenye pitapita zangu huko mitandaoni nimekutana na makala fupi ya chombo cha habari maarufu Al Jazeera, katika makala hiyo wameeleza kuwa utawala wa Magufuli umeonyesha jitihada kubwa za kunyanyua Uchumi wa Tanzania lakini pia Watanzania hawako salama chini ya utawala wake.
Masoud Kipanya, ambaye ni mchora katuni maarufu hapa nchini alihojiwa akasema kuwa anaishi kwa hofu kubwa, anashindwa kufanya kazi zake yeye kama msanii anasema kuna baadhi ya kazi ameshindwa kuzi-publish kwa kuhofia usalama wake.
Zitto pia kwa upande wake amesema kuwa ni kweli Rais ana nia ya kuleta maendeleo chanya kwa Watanzania na ni mtu mwenye msimamo na uthubutu lakini ameonesha kila aina ya udikteta hiyo imekuwa sababu ya Watanzania kwasasa kuishi kwa hofu kubwa.
Swali: Je, ni kweli Watanzania hatuko salama? Ni kweli Watanzania tunaishi maisha ya hofu?
Kuna ushahidi upi kuwa Watanzania wanaishi maisha ya hofu kama tunavyoelezwa?