GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,738
- 109,173
Ukibisha unataka tu Kubisha ila Al Ahly FC wako dunia yao Kimpira kwani Wanajua na wataendelea Kuujua kutokana na Kujipanga Kwao katika kila Sekta.
Kama si bahati jana ( na nahisi hata Babu yetu wa Kiutamaduni namaanisha Mganga wa Kienyeji ) alitusaidia mno kwani tulikoswakoswa zaidi ya mara Nne Kipindi cha Kwanza na kama yote yale yangeingia na ukajumlisha na Mawili yao Matokeo yangekuwa ni 6 - 2 na Shughuli ingeishia hapa hapa Benjamin Mkapa Stadium Dar es Salaam Tanzania.
Hata hivyo Simba SC nao wamejitahidi kuonyesha kuwa katika Ukanda huu hakuna wa Kuwafikia na nitashangaa kuona Timu zingine Kubwa za huu Ukanda zisipojifunza kutoka kwa Simba SC kwani Kucheza na Vilabu Vikubwa Barani Afrika ( tena kutoka kwa Waarabu ) na Kuwamudu Kimatokeo si Kitu chepesi bali Maandalizi ya uhakika pamoja na Kujipanga kunahitajika sana.
GENTAMYCINE nasema endapo tu Wachezaji wa Simba SC wakiamua Kucheza Mpira wa pamoja, kuepuka Makosa ya Kitoto, kupunguza Papara, Concetration na Marking yao ikiwa ni ya 100%, wasipotegeana na kuwa Wavivu nina uhakika Jumanne ( tarehe 24 Oktoba, 2023 ) Simba SC inaenda Kuitoa Al Ahly FC katika Mashindano haya ya AFL huko huko Kwao nchini Misri.
Pongezi nyingi kwa Wachezaji wa Simba SC kwa Kujitahidi kujitoa Kuipambania Klabu ili Mapungufu yafanyiwe Kazi upesi, wasilaumiane, watiane moyo, wajiamini kwani dalili za Simba SC kuwatoa Al Ahly FC huko Kwao katika Mechi ya marudiano naziona na Afrika pamoja na Dunia haitoamini.