GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,646
- 109,034
Taarifa ikufikie hapo ulipo kuwa Klabu ya Simba nayo imechangia katika Uboreshwaji wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kununua Fenicha zote ambazo 'Wanaowekwa' na Ihefu FC kila mara katika Ligi Kuu ya NBC wataanza kuzikuta nao wakianza kuutumia huo Uwanja kuanzia tarehe 20 Oktoba, 2023 utakapokuwa umefunguliwa rasmi kwa Mechi kubwa, ya Kihistoria na ya Kimataifa duniani baina ya Simba SC ya Tanzania na National Al Ahly SC ya kutoka nchini Misri katika Michuano mipya ya African Football League (AFL)
Hongera na hongereni sana Simba SC kwa Utu, Uthubutu na Upendo huu kwa Mpira wa Tanzania na hakika mmetuheshimisha sisi Mashabiki wenu akina GENTAMYCINE na wengineo.
Na Wengine Wavumilie tu kwa sasa ila kama Wageni watakaokuja nchini Tanzania na kukosa magodoro ya kulalia nao wanaweza kujipendekeza kwa kutoa yao ila kwa sharti tu yasiwe na kunguni na yawe yana nyama za kutosha kwa ndani ili yasiumize migongo ya wageni na wakirejea makwao wakaanza kuisema vibaya Tanzania yetu.