GUMZO: Al Ahly ageuka kibonde baada ya mechi na Simba

Best Daddy

JF-Expert Member
Apr 2, 2019
769
1,292
Je, Simba SC kutolewa na Al Ahly SC ilipaswa kuwa story kubwa?.

Majibu ya swali hili yanaweza ibua mijadala mingi sana, ambayo si yataleta tofauti kwa mashabiki (watu kushikana mashati) bali italeta hisia tofauti kuanzia kwa ngazi ya uwekezaji, uongozi hata wachezaji kwa ujumla.

Lakini kuna baadhi ya vichekesho vinaendelea Tanzania ya kuwa Al Ahly sasa wapo "Unga", wakimaanisha Al Ahly ni timu mbovu kwa sasa.

Ila mbona Imekua mapema sana. kwanini tume-shift haraka hivyo kutoka kusema kuwa Simba atapigwa kama ngoma wengi wakisema 3+ (anaenda kuliaibisha Tanzania) hadi Al Ahly ni wabovu. Mbona imekua ghafla hivyo?

Je, hizi kauli mlikua mnasema wakati hamjamuona Al Ahly akicheza?
Je, mlikua mnasema kitu ambacho hamkijui? Tukiwaita waropokaji tutakua tunawakosea?
Tukianza kuwapuuza kile mnachokisema, tutaonekana tuna dharau?
Maana tuliwaamini zile kauli zenu za kumpamba Al Ahly...mbona sasa mmetugeuka? Tushikilie yale mliyotuambia wakati ule au haya ya Sasa? Tunaomba majibu .

Well...Sasa ngoja niwape takwimu ya Al Ahly kabla ya mechi ya Simba.
Al Ahly katika mechi zake tano(5) za mwisho kabla ya kukutana na Simba ameshinda mechi zote, amefunga mabao kumi na saba (17) na kuruhusu goli moja (1) pekee.

Why ageuke kuwa unga baada ya hizi mechi mbili na Simba?

Let me whisper something; Hizi kauli sio mara yao ya kwanza, Ni kama script inajirudia vile. Katika comment moja ya mashabiki wa Al Ahly aliyejaribu kuwapa moyo mashabiki wenzake waliolalamika kuwa wanahitaji kubadilishwa mishipa ya damu baada ya kuhisi kupasuka kutokana na pressure ya mchezo. Hii ni lugha ya picha. (Unaweza pita kwenye ukurasa wa Al Ahly kuthibitisha hili).

Ila huyo shabiki wa Al Ahly alisema bora yetu sisi, huku akiwauliza wenzake mliona kilichotokea Mohamed V? Kwa wenzetu kilikuwa ni kiwanda cha machozi, yalikua ni mateso. Akimaanisha mashabiki wa Wydad walilia sana katika mechi ile. I hope wewe unayesoma andiko hili ulishuhudia kilichotokea, kama hukuona basi nikuambie mambo yalikua hivyo japo Wydad alifanikiwa kuvuka kupitia Mikwaju ya penati(4-3).

Ila Tanzania baada ya mechi hizo mbili na Simba, tuliambiwa Wydad wa sasa ni wabovu ila chakushangaza Wydad alifika hatua ya Fainali, japo Bingwa alikua Al Ahly. Na hakuna aliyekuja kubadilisha kauli yake, mambo yakaisha hivyo.

Kuna kitu katika Kauli ya Kocha Al Ahly (Koller) kuhusu Simba;

Baada ya mchezo wa Kwanza, Koller alijinasibu kuwa yeye ndiyo kocha aliyepata matokeo bora zaidi dhidi ya Simba, maana kila Kocha aliyekuja na Al Ahly kucheza na Simba kwa Mkapa alifungwa. Hapa akimaanisha Simba sio wa kawaida kawaida kama watu wanavyosema. Ila baada ya mechi ya pili: Japo hii kauli inatamfanya awe na wakati mgumu pale Al Ahly Sc (Huwezi bishana na Mashabiki wa Al Ahly ukabaki salama, muulize Pisto) ila yeye aliwapinga vikali kusema kauli ya kusema amecheza vibaya, ila yeye anaona amecheza vizuri sana kulingana na mpinzani aliyekutana nae. Hii ina maanisha nini? Majibu unayo.

Hata alipoulizwa issue ya kufanya mabadiliko ya wachezaji, alisema alishindwa kufanya Sub za Wachezaji sababu hakutaka wachezaji wapya waingie na kutumia muda ku-adapt tempo ya mchezo..."ambapo akiamini katika muda huo ambao yeye wachezaji wake wangetumia ku-adapt mchezo, mpinzani wake (Simba) angetumia nafasi hiyo kupata matokeo". Hapa Jamaa anamaanisha nini? Japo tuliona amemuingiza modeste jioni kabisa. Ila naamini Kocha wa Al Ahly (Koller) itamchukua muda mrefu sana hili jinamizi la Robertinho na Simba yake kutoka kichwani mwake.

Mashabiki wa Mamelodi wanasemaje:
Ukipita katika comment ambazo zimeigusia Simba, wanasema afadhali wamempata Al Ahly "Babe" wao, maana Simba ni timu ambayo utajidanganya unacheza mpira, unafika final third lakini hutaliona goli. Labda kwa maneno machache hii mbinu inafahamika "Haram Ball". Hii kauli inaweza thibitika katika mechi za Simba na Yanga (Ngao), wengi walisema Yanga alipaswa kushinda hata goli tano ila takwimu zinaonesha tofauti, Yanag alikua na Shot on Target moja pekee, huku zikiwa mbili pekee kwenye mechi na Al Ahly Sc katika mechi ya jana.

Huku wengine wakisema, katika hizi mechi mbili, Simba imebadilisha mentality ya Timu za chini ya ukanda wa jangwa la sahara kuwa hawa vigogo wa Africa ambao ni Timu namba moja Africa " Al Ahly" na namba mbili "Wydad", kuwa ni kweli wanakila kitu ila wakati wa timu zetu kufanya vitu umefika na nyakati za kuteswa sana zimeisha.

Turudi kwenye kosa kosa za Al Ahly, Unahisi kwanini wali-opt kupiga mashuti ya mbali baada ya kufika final third? ambapo hii labda inawafanya wengi wamaanini Al Ahly wapo unga, ambayo mengi yalikuwa ni off target. Mambo yapo hivi, tuliona kazi/clearance zilizokua zinafanyika na Che pamoja na Inonga. It was like, nikweli utamlambisha nyasi Che lakini Mimi(Inonga) nitakua nyuma ku-clear(vice versa), Hii ilifanya wa-opt kupiga mashuti ya mbali sababu ya Strength za beki za Simba.

Je hii nguvu ya kuishusha Al Ahly ili kui-discredit Simba mnafanya kwa manufaa ya nani?
Je ni hasira za kumpa 3+ Al Ahly katika betting?

Je mlitamani kuona Simba amefungwa zaidi ya 5 ndio kuthibitisha ubora wa Al Ahly?

Je kuna boss mnamtumikia, so mnaogopa kumkosea kwa kusema kile alichokifanya Simba?

Nashindwa kupata majibu kabisa. Why Wydad na Al Ahly wageuke wabovu wakikutana na Simba pekee? Katika hizi mechi mbili nilitegemea watanzania wata-ipongeza Simba kwa kuweza kuonesha ushindani dhidi ya Al Ahly Sc kama ninavyoona watu kutoka mataifa ya Africa(Nje ya Tanzania) waliokua wakifuatilia AFL wakifurahia na kushangazwa na kile kilichooneshwa na Simba, wakisema ni beyond their expectation. Kuna shabiki mmoja baada mechi ya kwa mkapa alisema and I quotes "...I think this should be a derby of Africa". (Anaweza akawa anatania, ila kitu amemaanisha, kuna radha anaipata wanapokutana hawa wiwili maana hadi sasa ni 50- 50).

Tukubali tukatae hadi kufikia sasa, japo anaitwa Mwakarobo na timu ambayo haijafika mafanikio yake kimataifa ila Simba ni timu iliyonesha ushindani mkubwa sana kimataifa.
Pia kwa Yanga I hope itakuwa the same, wapambane kuonesha walichonacho kimataifa ili kile kilichofachanyika msimu uliopita isionekane ni "fluke" I mean walibahatisha tu.​
 
Maelezo mareeeeeeeeeefu ka treni, pumba 'ntupu'.

Jibu hoja moja tu, simba hata akibebwa akaanzia robo fainali anaishia robo fainali.

Acheni kujustify ujinga! Mmetolewa kwenye vikao vyenu fokasini kuwa mmetolewa ili mjifunze next time mpambane. Hii ya kujiona eti mmewasumbua El ahly sio Tija. Tija ilikuwa kuwatoa el ahly muingie nusu fainali. Au ndio zile kauli za 'jamaa kanibaka viwili ila nimemsumbua sanaaaaa, kwa mbinde sanaaaa .........

Makolo sijui huwa mkoje yaani
 
Je, Simba SC kutolewa na Al Ahly SC ilipaswa kuwa story kubwa?.

Majibu ya swali hili yanaweza ibua mijadala mingi sana, ambayo si yataleta tofauti kwa mashabiki (watu kushikana mashati) bali italeta hisia tofauti kuanzia kwa ngazi ya uwekezaji, uongozi hata wachezaji kwa ujumla.

Lakini kuna baadhi ya vichekesho vinaendelea Tanzani​
Wewe ni mchambuzi hasa...hongera sana unajua.
 
Je, Simba SC kutolewa na Al Ahly SC ilipaswa kuwa story kubwa?.

Majibu ya swali hili yanaweza ibua mijadala mingi sana, ambayo si yataleta tofauti kwa mashabiki (watu kushikana mashati) bali italeta hisia tofauti kuanzia kwa ngazi ya uwekezaji, uongozi hata wachezaji kwa ujumla.
Mamelodi Sundowns kila mwaka wanajipigia tu Al Ahly afu Makolokolo SC yanajisifu yana timu nzuri na Kocha bora

Mbumbumbu SC ni failed team, haiwezekani miaka nenda rudi Al Ahly anatutoa sisi Kufa Kiume SC.

Adui tunacheza naye zaidi ya miaka 6 iliyopita lakini Malalamiko SC hatuna lolote nakati ilipaswa tuwe tumeshajua mbinu zote na aina ya silaha inazotumiaga Al Ahly kimchezo ili tuwe tunamfunga na kumtoa hata mara 1 1 tu.

Makolokolo SC ni overrated team kiubora isipokuwa inaonekana ikijitutumua kwa kupata hata sare kwa Al Ahly lakini haijifunzi kwa timu kubwa kama Mamelodi Sundowns ambapo awali ilikuwa ikisumbuliwa sana na Al Ahly lakini hatimaye sasa hivi Al Ahly ni Mchumba wa kawaida sana kwa Mamelodi Sundowns.

Makolokolo SC fan nateseka sana na kujuta kushabikia timu bovu kama....................
Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
View attachment 2792291
 
Kuna kitu naona watu hawaelewi unajua kabla ya physic mpira sehem ya kwanza unachezwa kichwani yani mentality,so al ahy kulingana na historia kati ya yeye na simba huwa anaamini hawa huwa wanatusumbua sana na pia simba wana kuwa wanasema hawa tunawaweza hii moja Kwa moja inaenda kuwa applied kwenye mchezo,jiulize al ahy kakosa magoli ambayo Kwa team nyingine asingeweza kukosa mfano huo huo ni yanga na ihefu,simba na Toto africa ya mwanza
 
Je hii nguvu ya kuishusha Al Ahly ili kui-discredit Simba mnafanya kwa manufaa ya nani?
Je ni hasira za kumpa 3+ Al Ahly katika betting?
Mimi binafsi naamini wapo wanaokataa kuipa credit Simba kwa kuwa amesababisha wapigwe kwenye mikeka. Kuna watu waliweka mzigo wa maana kwa kuipa Al Ahly mabao 3+, baada ya kuliwa na muhindi wamegeuza hasira kwa aliyesababisha!
 
Kama unakubali kwamba Simba kapandisha kiwango chake kwanini unakataa kua Al ahly ameshuka kiwango chake?
Mamelodi Sundowns kila mwaka wanajipigia tu Al Ahly afu Makolokolo SC yanajisifu yana timu nzuri na Kocha bora

Mbumbumbu SC ni failed team, haiwezekani miaka nenda rudi Al Ahly anatutoa sisi Kufa Kiume SC.

Adui tunacheza naye zaidi ya miaka 6 iliyopita lakini Malalamiko SC hatuna lolote nakati ilipaswa tuwe tumeshajua mbinu zote na aina ya silaha inazotumiaga Al Ahly kimchezo ili iwe inamfunga na kumtoa hata mara 1 1 tu.

Makolokolo SC ni overrated team kiubora isipokuwa inaonekana ikijitutumua kwa kupata hata sare kwa Al Ahly lakini haijifunzi kwa timu kubwa kama Mamelodi Sundowns ambapo awali ilikuwa ikisumbuliwa sana na Al Ahly lakini hatimaye sasa hivi Al Ahly ni Mchumba wa kawaida sana kwa Mamelodi Sundowns.

Makolokolo SC fan nateseka sana na kujuta kushabikia timu bovu kama....................
Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
View attachment 2792291
Tatizo lenu hamfuatilii umebeba matokeo ya hivi karibuni.

Mamelodi Sundowns vs Al Ahly SC Wamecheza mechi 11: Al Ahly ameshinda nne(4), Mamelodi Sundowns (3) na huku sare (4).

Simba pekee ndiyo 50-50 hadi sasa.

By the way, nimependa sana wakati unaizungumzia Simba umeitaja Mamelodi Sundowns na Sio timu nyingine. Levels
 
Je, Simba SC kutolewa na Al Ahly SC ilipaswa kuwa story kubwa?.

Majibu ya swali hili yanaweza ibua mijadala mingi sana, ambayo si yataleta tofauti kwa mashabiki (watu kushikana mashati) bali italeta hisia tofauti kuanzia kwa ngazi ya uwekezaji, uongozi hata wachezaji kwa ujumla.

kuonesha walichonacho kimataifa ili kile kilichofachanyika msimu uliopita isionekane ni "fluke" I mean walibahatisha tu.​
Simba ni wachawi tu.. na kiboko yao ni timu za Jdngwa la kusini mwa Adrika kana South/ Namibia/ Botswana
 
Kama unakubali kwamba Simba kapandisha kiwango chake kwanini unakataa kua Al ahly ameshuka kiwango chake?
It's not a necessarily event. Msimu mmoja mwanafunzi A akapata alama 85% na kushika namba moja darasani na mwanafunzi B akapata alama 80% akishika nafasi ya pili. Msimu unaofuata Mwanafunzi A akapata alama 85% tena na kushika namba moja tena darasani na mwanafunzi B akapata alama 84% akishika nafasi ya pili. Je, kitendo cha mwanafunzi B kuongeza alama 4% ni lazima kishushe nafasi ya mwanafunzi A? Jibu ni hapana. B amepanda lakini haimaanishi amemshusha A
 
Je, Simba SC kutolewa na Al Ahly SC ilipaswa kuwa story kubwa?.

Majibu ya swali hili yanaweza ibua mijadala mingi sana, ambayo si yataleta tofauti kwa mashabiki (watu kushikana mashati) bali italeta hisia tofauti kuanzia kwa ngazi ya uwekezaji, uongozi hata wachezaji kwa ujumla.
kuonesha walichonacho kimataifa ili kile kilichofachanyika msimu uliopita isionekane ni "fluke" I mean walibahatisha tu.​
Binafsi nimewashangaa sana hawa wachambuzi leo mtu anakuambia ahly ktk ubora wake anakupga 5 anasahau wakati anaouzungumzia ni kipindi ambacho ligi yetu ulikuwa huwezi hta kuipambanisha na timu za Kenya na Uganda au zilikuwa sawa ni wakati ambao tulikuwa tunategemea wachezaji wetu wa kitanzania kw kiasi kikubwa lkn leo unaizungumzia Simba yenye Che na Inonga mabeki wenye ubora.

Kw ujumla ligi yetu imebadilika na imeimarika kwa kiasi kikubwa sajili zinazofanyika wakati huu.
Ahly na Waydad ni walewale km wanakutana na beki zisizojiamini goli 5 lazima zihusike tu we uwawekee Kennedy asaidiane na Watara halafu wakukose goli 5
 
Back
Top Bottom