gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,714
mmmh!............sasa hapa kuna imani naona inaingia na hii haitofautiani na ile ya mwanamke akiumwa uchungu basi afunge fundo kanga yake dogo kama vile kafunga hela, basi akifanya hivyo atafika hosp bila kuzaila njian na akishafika tu kwenye meza ya kujifungulia basi hupaswa kulifungua fundo ili mtoto azaliwe.
tena husadikika kwamba lisipokumbukwa kufunguliwa basi mama ataumia kwa uchungu tu ila mtoto hatazaliwa. binafsi sijawah kujaribu hili manake nilihofia isije ikawa kweli nikamkosa mtoto. ila kiuhalisia sioni mantiki.
pia naweza kufananisha na ile dhana ya siku mwali anatoka ndani basi hufungiwa pini kwenye moja ya kanga zake ambayo haionekani ama kuekewa njiti ya kiberiti ana sindano eti ili mtu mwenye jicho baya asimwone kwa husda mwali sidhan kama yana ukweli ila tu tuliaminishwa na mabibi zetu kwa minajili kwamba pini itamchoma mtu mwenye husda ama sindano na njiti ya kiberiti itamuunguza.........lol! snowhite unakumbuka haya??

Last edited by a moderator: