Akili za wanawake bwana!

Akili za wanawake bwana!

Fundi mahiri wa Ujenzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2012
Posts
4,717
Reaction score
3,680
Wanangu hamjambo!

Kumpa siri za mambo unayoyafanya ofisini mkeo ni hatari kubwa.

Sikiliza kisa hiki..........

Kuna rafiki yangu fulani hivi alikuwa akimueleza mkewe kila kitu anachokifanya kwa ofisi
Sasa one day mwanamke akagundua kuwa mumewe ana kabinti huko mtaani anakagegeda
mwanamke aka mind sana kukawa na bonge la ugomvi bwana.....

Yule bibie si kaenda ofsini kuonana na bosi wa mumewe kusema yote anayoyafanya mumewe hapo ofsini lol.

Baada ya kumuumbua mumewe si kibarua kikaota nyasi
Haya sasa jamaa hana kazi wamebaki wanaangaliana usoni

Mama anahitaji mahitaji ya nyumbani mshikaji hana mkwanja
maisha yamekuwa magumu

Nyie wanawahi hizi ni akili au matope?
 
::
Hawara anahusika vipi na kazi za ofisini au ni shirika la dini?
=
 
Unampa siri zako mwanamke shambenga unategemea akutunzie siri?
Hata wanamme mashambenga mbona wapo?

Nna siri nzito zake za ofisini na sijawahi hata mwambia ndugu yangu.

Hawa watu sijui wakoje ......... e mwenyezi mungu tunusuru nao
 
kumsimulia mwanamke mambo ya offisi na mengine yasiyomhusu ni UDHAIFU MKUBWA mwanamume hutakiwi kuwa dhaifu
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Wanangu hamjambo!

Kumpa siri za mambo unayoyafanya ofisini mkeo ni hatari kubwa.

Sikiliza kisa hiki..........

Kuna rafiki yangu fulani hivi alikuwa akimueleza mkewe kila kitu anachokifanya kwa ofisi
Sasa one day mwanamke akagundua kuwa mumewe ana kabinti huko mtaani anakagegeda
mwanamke aka mind sana kukawa na bonge la ugomvi bwana.....

Yule bibie si kaenda ofsini kuonana na bosi wa mumewe kusema yote anayoyafanya mumewe hapo ofsini lol.

Baada ya kumuumbua mumewe si kibarua kikaota nyasi
Haya sasa jamaa hana kazi wamebaki wanaangaliana usoni

Mama anahitaji mahitaji ya nyumbani mshikaji hana mkwanja
maisha yamekuwa magumu

Nyie wanawahi hizi ni akili au matope?

Ukitumia sentensi "Akili za wanawake bwana" inakuwa kama umewaambia wanawake wote wana hizo tabia. Ila ukweli ni kuwa inawezekana ni baadhi yao wenye hizo tabia zilizotajwa hapo. Najaribu pia kufikiria kwa upande mwingine kuwa inawezekana ni hasira za huyo mwanamke kugundua kuwa mumewe anatoka nje ya ndoa ndiyo zilizompelekea kutoa siri. Laiti kama jamaa angekuwa mwaminifu hayo yote yasingetokea!!!

Kwa kesi hii, wote wana makosa maana mwanaume kagegeda nje, mke katoa siri kazini na matokea yake amebwagwa kazi. Kwa kifupi, mume kamwaga ugali mke akaamua kumwaga mboga, sasa ngoma droo wote wako kijiweni. Kama wana akili, huu sasa ni wakati wa kujifunza, huyo mmbea aache tabia yake na huyo wa nyumba ndogo naye atulie ili watafute kazi na kuanza maisha upya.

Hongera yao kwa changamoto hii!!!!
 
Baibo ilidhamaliza kila ktu. Fundisho hilo na kutomwambia siri mwanamke lipo kwa Samon na Delila.
 
huyo mwanamke aliona kazi ya mume wake ndio inampa wanawake wengne ili kuzuia ni kuarbu kibarua..Kama ni mm nampa likzo aende kwao mpaka ntapopata kaz
 
Yalekea sio mke wake aliyetoa siri bali ni hawara wa hawara.
 
Mambo ya kazini ni ya kazini na ya nyumbani ni ya nyumbani. Pia katika hili hapo hapakuwa na ndoa imara, unapokuwa kwenye ndoa lazima umpende mwenzako katika shida na raha, upendo hauhesabu makosa, mabaya nk. Alitakiwa kukaa chini na kuongea na mwenzi wake na kumwombea kwa Mungu aachane na yote mabaya ya kazini na huyo kimada. Hakika kwa uzembe wetu na papara tunaziweka ndoa zetu katika mazingira magumu na pengine hata kuzivunja.

Tutende mapenzi ya Mungu daima katika maisha yetu ya kila siku, na pale tunapokosea tulekebishane maana sisi sote ni binadamu wa kawaida na tunaishi na mapungufu yetu na Mungu daima anatupenda tumrudie yeye.

Hasira hasara, imeandikwa (uwe na hasira lakini usitende dhambi), na tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi na uchafu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom