masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,903
- 13,197
FUNDISHO, tunalolipata katika ajali hii iliyompata mh. Kigwangala ni kubwa sana.
Magari haya Toyota Landcruiser V8, 8cylinder, iwe petrol au diesel zina mwendo hadi 260km/hr!
Hapa nchini sioni sehemu ambayo unaweza kwendesha gari bila bugudha hata 200km/hr.
Barabara zetu hazijasanifiwa kwa spidi zaidi ya 120~140km/hr.
Nikienda mikoani, hasa Dodoma, nimeona hayo magari yakipaa, literally!
Hata misafara ya viongozi wetu, tumeona huko mikoani spidi ya magari ni ya kutisha sana.
Sawa, polisi haiisumbui hii misafara na wakati mwingine wanawasafishia njia, lakini kuna watumiaji wa barabara kama wanyama (au hata watoto wadogo vijijini) ambao hawaelewi cha polisi wala msafara.
Vyombo vyetu vya usalama viamke sasa na hii threat ya viongozi kuweza kujimaliza wenyewe kwa mwendo kasi usio wa lazima.