halafu abiria wa mabasi tunalazwa standi za mabasi usiku kwa mabasi kufika usiku mono na kushindwa kwenda makwetu. basi toka Dar kwenda Songea badala ya kufika saa mbili kama lingetembea walau speed 100 kwa saa na kuruhusiwa kuanza safari saa 11 alfajiri, tunatembezwa a mazimum of 80 km/h na kila penye kibanda kuna speed limit ya 50 km/h, halafu ukaguzi kila mji.mizani zote mabasi yanapima na kupoteza muda mwingi ( mfano basi linapima mizani mbele ya mlandizi, halafu tena karibia morogoro, halafu mikumi, kisha mikumi, halafu iringa, makambako, halafu songea na kila mizani basi linatumia si chinii ya dakika 15) nchi hii tunaenda wapi jamani?Mbona mambo haya hakuna nchi nyingine duaniani?
Mkuu umenena vyema sana. Ni vizuri wakajua pasi na shaka hatuwaungi mkono kwa spidi hizi restrictions za spidi kwa mabasi.
Ilikuwa jambo la kheri kuona nchi zingine kukosea vipi.
Uhakika sote tungejipanga sawa mbele ya sheria tungekuwa na sheria muafaka (no wonder and without being a prophet) indeed hawa hawa wanaotulaza majiani kwa kushinikiza 80km/h na 50km/h wangependekeza twende angalau 100km/h na 60km/h respectively.
Badala ya kuwataka ku uplift hizi zingine tupiganie usawa kwenye sheria. Kitaeleweka tu.