Ajali ya Happy Nation yaua Hakimu na mume wake Bukoba

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1670420792167.png
Polisi mkoani Kagera inamshikilia dereva wa Basi la Happy Nation, Shaaban Khatibu 38 mkazi wa Dare es Salaam akidaiwa kusababisha vifo vya watu wawili.

Tukio hilo inadaiwa lilitokea Barabara ya Biharamulo, Kata Ijuganyondo, Manispaa ya Bukoba, Jumanne Desemba 6, mwaka huu majira ya saa 5.30 asubuhi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amewataja marehemu hao kuwa ni Geofrey John (42), mfanyabiashara na Tumaini Jofrey (41), ambaye ni hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kata ya Maruku.

Amesema Geofrey na Tumaini walikuwa wamebebana kwenye pikipiki, yenye namba za usajili T308CLH, ambapo walisukumwa na mwendesha pikipiki aliyekuwa amebeba magunia ya mkaa na kisha kuangukia uvunguni mwa gari la kampuni ya Happy Nation, yenye namba za usajili T70DFV, aina ya Youtong, inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Bukoba.

Amesema polisi inaendelea kumtafuta dereva wa pikipiki iliyokuwa imebeba mkaa na kwamba uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Katika mitandao mbalimbali ya Whatsapp ya mjini Bukoba, kulisambazwa ujumbe wa Tanzia ulioonesha umetoka Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba kwamba na ukieleza kifo cha hakimu huyo pamoja na mumewe kwa ajali ya gari, ingawa polisi haikusema kama ni mke na mume.

‘Tanzia: Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, inasikitika kutangaza kifo cha Tumaini John Kiyeyeu-C/No.11510783 Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kolekero, Bukoba na mme wake kilichotokea mchana huu kwa ajali ya gari na kupelekea wote kupoteza maisha. Tutaendelea kutoa taarifa kuhusiana na taratibu za mazishi,” unasomeka sehemu ya ujumbe huo.

HABARI LEO
 
Barabaran kuna ujinga sana

Dereva hana kosa lakin kakamatwa na atatoa hela nying tu mpaka kumaliza hyo kesi na akitoka anakosa ajira anaanza tena kutafuta

Mimi kuna liboda boda lilishika brek kwa nguvu likateleza likaja upande wangu nikalikwepa ila likajigonga kwenye body,nikasimama kusikilizia,wanazengo walipokuja naambiwa nimpeleke hospital mara polisi nikaambiwa nitengeneze pikpik na kuhudumia mpaka atakapopona likidonda nalo limegoma kupona heri ningekimbia tu siku hyo
 
Back
Top Bottom