Ajali ya gari la polisi imetokea uwanja wa ndege Dar

Ajali ya gari la polisi imetokea uwanja wa ndege Dar

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Ajali hii imetoa ujumbe mbaya sana wa chuki ya wananchi kwa Polisi yaani Polisi wanaomba Masaada raia wanaangalia tu, sijawahi kuona hii kwenye Taifa langu ila leo nimeona kwa macho yangu, hii ni mbaya sana kwenye nchi yetu kiwango cha chuki kwa wananchi ni kikubwa sana, nchi yetu inahitaji kuponywa hatupo salama hata kidogo.

Hapo kuna majeruhi wapo pembeni wametapakaaa Damu wote ni polisi wamegongana na eicher ya Chanika watu hawatoi msaada inawanasema pembeni jamani polisi hayo maumivu ndio waliyokuwa wanapitia ndugu zetu waliopigwa risasi tarehe 29-30.

Endeleeni kuona hili ni jambo la kawaida sio jambo jema wala sio utamaduni wetu, hatua za haraka zichukuliwe kuponya Taifa letu.
 
Nashindwa kuelewa hizi porojo
Yaani wananchi wasaidie nini?
Uokoaji sio kazi ya wananchi, kwanza wanafanya nini hapo hawana kazi ya kufanya?
wanakusanyika hapo ili iweje ? mibongo ikona tu tukio inaweza kushinda hapo mpaka jioni
Hili ndio tatizo la kutokujishughulisha
 
Pandisha video inayo jieleza mojakwamoja, apo inaonekana kweli Kuna ajali na kwa hapa kwetu nikawaida watu kushangaa tukio likitokea.
Ila video Yako haionyeshi ao polisi wanao hitaji msaada na Wananchi Waka kataa kuisaidia.
Tupunguze ujuaji kwa vitu vya ki puuzi
 
Back
Top Bottom