The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,121
Nikiwa natoka mihangaikoni, mara paaap, nikiwa sehemu moja inaitwa Taula, kilometa chache kutoka Segera uelekeo wa Dar, nakutana na raia wapo nduki wakiwa wamebeba viroba vya unga wa Azam.
Kumbe bwana, kuna gari lilipata ajali na raia wakaona pa kuponea. Watu wa Taula watakula sana chapati na maandazi wiki hii. Huenda wengine wakaanzisha biashara za migahawa.
Ubaya nilichelewa kutoa kamera kwa mshangao ulionikumba baada ya kuona jamaa mmoja kubeba viroba vinne vya kg 25 kwa mpigo. Jambo hili ni kengele kwa Jamhuri kuwa watu wana njaa kali - ya pesa, huenda, na msosi.
Kwa hali ilivyoonekana, sina hakika kama dereva na utingo wake wapo salama. Ila unga umepatiwa hifadhi majumbani.
Hii si stori ya kulaumu Polisi (walinzi wa usalama wetu na mali zetu) kuwepo na kuacha watu kuendelea kubeba mzigo; ni stori tu ya kufa kufaana ya Wabongo. Tumeona kwenye stori za magari ya mafuta kule Moro na kwingineko.
Hii imenikumbusha maeneo fulani gari la bia lilivyopata ajali na watu wakaanza kusepa na kreti za bia. Polisi waliingilia kati wakasema watu wanywe bia palepale wasiondoke na chupa au kreti.
Vipi wewe, gari la mchele wa Kyela likidondoka utamcheki dere anaendeleaje au utaokota kiroba watoto wakaufinye?