Ajali nyingine yaua watano Kilimanjaro, wanne wajeruhiwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Watu watano wamefariki dunia papo hapo baada ya lori lililobeba katoni za maji ya kunywa kufeli mfumo wa breki katika eneo la mteremko barabara ya Mwika-Himo na kuigonga kwa nyuma gari dogo la abiria aina ya Toyota Noah lililokuwa likitokea Rombo kwenda Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Ajali hiyo imetokea jioni ya Jumapili Januari 15, 2023. Daktari wa hospitali ya Faraja, Samweli Minja amethibitisha kupokea miili ya watu watano na majeruhi wanne.

"Ni kweli tumepokea miili ya watu watano wako mochwari na majeruhi wanne leo hapa hospitalini kwetu," amesema Dk Samweli

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza anaeleka eneo la tukio na atatoa taarifa baada ya kufika na kuona hali ilivyo

"Naelekea eneo la tukio kulikotokea ajali nikifika nitatoa taarifa kamili,"amesema Kamanda Maigwa

MWANANCHI
 
Mzembe dereva wa roli. Kisingizio breki wakati hazingatii kanuni za kuendesha kwenye mteremko. Engine braking inatosha kabisa kushuka mlima pasipo brake nyingi.
Ajali za mlima huu pia zinachangiwa na uelewa mdogo WA polisi wetu, wamekuwa wakiwinda Magari madogo Kwa speed camera ili Gari zote ziende Kwa speed 30kph walizowekewa malori!! Hivyo unakuta Gari ndogo zinaongozana na malori ambayo ni rahisi kugongwa na hayo malori!! Magari madogo ni rahisi kumudu mlima kushuka au Kupanda!! Ila polisi wamefanya kitega uchumi!! Woga WA hizi faini zisizokuwa za haki zinafanya Magari madogo kuongozana na malori speed 30 hadi 50kph!! Jamani polisi waongezewe weledi !! Hili nalisema nikiwa na uhakika asilimia 100! Huu mlima ni mkali na hatari sana, ila polisi wanatumia vibao vya malori kupatia Hela Kwa Magari madogo!!! Polisi kituo cha Himo hili linawahusu!!!!
 
Mzembe dereva wa roli. Kisingizio breki wakati hazingatii kanuni za kuendesha kwenye mteremko. Engine braking inatosha kabisa kushuka mlima pasipo brake nyingi.
Yeah ni kweli, unaweza zako namba moja kisha unaacha silence..., taratibu inashuka
 
Ajali nyingi zipo Tanzania tu, hizi geographical factors (milima, mabonde, nk) kwa wenzetu hazipo! Au wenzetu barabara zao ni za viwango tofauti na za kwetu? Kama sio hivyo, basi wengi wetu ni wenda wazimu! Kipi sahihi katika hayo mawili?
 
Wewe ni FALA.
Thanks,u feel much better now?,dot.com generation mnachojua ni kukimbizana na viajira uchwara mnavyotupiwa ,na sikulaumu maana uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo, unaona ni vema wewe upate taarifa za mama yako kufa kupitia social media na SIO police Kuja kwako kwanza na kukupa hizi taarifa ukiwa ndiye next of kin, tatizo la kukulia in a upper class, Nkanini hajakulia huko ,ndio maana mpaka leo yupo lingusenguse, sehemu ambayo haijawahi kutembelewa na kiongozi yeyote wa top 4 toka nchi hii iwe huru!
 
Back
Top Bottom