Ajali Morogoro: Mrithi wa Villa Park Makambako afariki

Ajali Morogoro: Mrithi wa Villa Park Makambako afariki

Huyo chalii hajafariki wala nini,yuko pale Moro dingi ake anafanyaga biashara ya Magari.

Hakupata ajali yoyote zile picha za ajali wala hazikua za Mark x kama uliangalia vzr.
Kama yuko hai yule Chalii ana hatari , na barabara zenyewe hizi!
 
Kwa jinsi alivyo, huyo atakuwa ni wale vijana wa kuendesha subaru kwa spidi na sauti kubwa.

Halafu huwez amini mkuu. Dogo alikua mtaratibu sana na aliendelea kuishi maisha ya upole na unyenyekevu hata baada ya kukabithiwa urithi. Tena gari aliyopata nayo ajali siyo anayoitumia makambako akiwa mtaani, anatumiaga kanoah kabovu bovu tu
 
Mchiz yuko pale Moro wala hakupata ajali wanamzushia,dingi yake ni dealer wa Magari so anafuataga magari dar kuyaleta Moro.
Mi mwenyewe nashangaa watu walivyokomalia kafa wakati najua hajafa. Wanaokufa ovyo ni washamba wa magari huwezi kimbia na gari at full speed kwa njia ambayo hujaimaster vizuri kisha ubaki salama. Njia ya dar moro inanyookaga vizuri sana ukishapita bwawani pale.
 
Mi mwenyewe nashangaa watu walivyokomalia kafa wakati najua hajafa. Wanaokufa ovyo ni washamba wa magari huwezi kimbia na gari at full speed kwa njia ambayo hujaimaster vizuri kisha ubaki salama. Njia ya dar moro inanyookaga vizuri sana ukishapita bwawani pale.
Si unajuaga wabongo tuna tatizo la kusambaziana uongo kwenye mitandao mkuu.

Unachosema ni kweli mkuu maana huyo chalii ndio shughuli zake kwenda kuchukua hayo Magari Dar to Moro so hio barabara anaijua mwanzo mwisho mkuu.
 
R.I.P kijana mbichi kabsa...
Kaka na mdogo wote wamefia morogoro kwe ye ajali ya gari.... mwaka jana na mwaka huu...
Interesting...
 
Unafikir ni nini sasa, kwani Kanumba alipenda kuacha ji Lexus cruiser lile na maisha ya kubadili malaya town. Ndio alikuwa kafika patamu ila ikabidi adondoshwe tu
Hahah mkuu unaamini Kanumba alikua ni "Memba" kule kwenye hako ka mtandao?
 
Muffler tamu sana hawajui hao raha yake hasa ukiwa na six cylinder manual kama cruiser 80 utaipenda. 1HD
Ile engine noma sana aisee ikinipataga sehemu nahakikisha nakimbizana nayo hapo nyuma nisikie jinsi inavyocheua hahah
 
Unafikir ni nini sasa, kwani Kanumba alipenda kuacha ji Lexus cruiser lile na maisha ya kubadili malaya town. Ndio alikuwa kafika patamu ila ikabidi adondoshwe tu
Duuh acha nibaki tu na umasikini wangu nikufe kwa mipango ya Mungu
 
yule kaka yake mwaka jana kabla japata ajali..mke wake alifariki kama sijakosea akiwa anajifungua..wakafa mama na kichanga..wakazikwa kaburi moja la gorofa. (mama akaanza chini kisha mtoto akazikwa juu yake...
akabaki huyo mume wake ambae nae akala mzinga mbaya sanaakiwa na dem mmoja (mwalimu na MKE wa mtu) ..aliianzia safari yake pale mafinga jion baada YA MECHI..
sasa dogo mrithi nae kafata kwa staili ile ile kama ya kaka yake..zote ajali...

huyo mjane wa kaka mkubwa ni yupi? maana alianza yy kufa
hee kumbe wamekufa kwa utata namna hii. huu uchawi sio wa nchi hii
 
Wabongo tumezidi ujinga, eti wanakufa kila mwaka...hiyo familia wapo wangapi na mpaka sasa wameshakufa wangapi?

Na hakuna pesa za uganga/masharti, ina maana kuna mfumo mwingine wa pesa tofauti na mfumo unaosimamiwa na benki kuu ya taifa? na hayo masharti yanakupa pesa kiasi gani? maana basi Wenye pesa wote ulimwengu huu wangekuja huku.

Duniani kuna pesa za aina mbili tu, pesa halali na pesa haramu...kuna wale wanaopata pesa kwa ubunifu/juhudi zao za kazi..na wapo wanaopata pesa kwa kudhulumu Wenzao, kuiba, kuuza bidhaa haramu kama dawa za kulevya, kutapeli wengine n.k.

Ndio maana Waganga na Mapasta feki wanatumia ujinga uliotujaa vichwani kutuambia wanaweza kutusaidia tupate pesa, ili hali yeye tunamkabidhi pesa halisi tulizozitolea jasho, nae ndio akanunue Vogue aje kuwatambia nalo.

Kama tukio linashabihiana na lililomkuta ndugu yake sidhani kama ni hali ngeni saana kutokea dunia hii, hata yule binti wa Whitney Huston alikutwa na umauti kwa njia ile ile kama iliyomkuta Mama yake.

Hebu Wabongo tuache ndoto za mchana na imani za kijinga.
umeandika utumbo, pesa za majini zipo...usiamini
 
kuku atakuwa alikula punje mbili,si unajua ule uganga wao kuku anarushiwa mahindi atakayokula ndo miaka mtakayoishi sasa huyu kuku wao naona alikula punje mbili tu maskini
Sasa mbona miaka miwili hajamaliza nimesikia hapo kaka akee kafa mwaka jana ndio kamrithi
 
Back
Top Bottom