Ajali mbaya Handeni, basi la Burudani limeua 12

Dah dereva ndio mtu wakwanza kupoteza maisha anaitwa luta name mwingine ninae mjua ni majeruhi sana wanapenda kumuita ukimwi R.I.P
 
Otatenaneeee. Burdan nkwai? Nkwai? Hili basi linapendwa sana na ndugu zangu wa pale Korogwe. Sijui sababu ni nini? Ngoja niwatafute ndugu zangu maana moyo unanienda kwa kasi mno
 
Kama anatoka kigoma kwenda tunduru hazifiki
Kigoma dar km 1500 dar tunduru via masasi 1200 = 2700km

mkubwa,dar>tunduru via masasi huo umbali umeutolea wapi?
dar>lindi km ngapi?
lindi>masasi.??
masasi>tdr..?..
JIPANGE.
 
Kila siku tutabaki Rest In Peace...lkn mamalaka husika ni rushwa rushwaaaaaa.......magari hayakaguliwi kwa ubora wake,juzi tu hapo Kilinjiko watu kibaoo wamekufa,tutabakia kusema Rest in Peace....Ovyoooooo #TeamWekaPicha #
 
ajali imenipoteza Auntie yangu R.I.P auntie, inauma sana mtu anapofariki kwa ajali ya gari ni bora mgonjwa utakuwa umemuuguza ila sio ulietoka kumuaga na mnapeana ahadi za muda mfupi baadae.
 
ajali imenipoteza Auntie yangu R.I.P auntie, inauma sana mtu anapofariki kwa ajali ya gari ni bora mgonjwa utakuwa umemuuguza ila sio ulietoka kumuaga na mnapeana ahadi za muda mfupi baadae.

Ndo mitihani. Rip wote waliotangulia.

Na Mungu awape afua njema majeruhi wote.

Inna lilah wainna ilayh rajiuun
 
sikubaliani na wewe kwenye issue ya leseni, bali naungana na wewe kwenye kipengele cha uzembe na mwendo kasi, overtaking without precation, etc. sheria za barabarani hazifatwi japo wanazijua vizuri. Sisi abiria pia tuna tatizo, hatuna msimamo mmoja.
 
Nimepokea taarifa basi burdani likitokea korogwe asubuhi ya leo limepata ajali maeneo ya kabuku na inasemekana zaidi ya abiria 22 wamefariki hapo hapo

Inasemekana lilikuwa linatoka Korogwe likielekea Dar e Salaam.

Limeanguka katika kijiji cha Taula Handeni.

Limeua abiria 12 hapo hapo na majeruhi ni wengi kwa mujibu wa Breaking News ya Radio One.

Poleni sana mliopoteza wapendwa wenu, na majeruhi ugueni pole.

Natoa pole kwa majeruhi na familia za marehemu.

Watoa habari, ipi ni idadi sahihi; 12 au 22?
 
burudani.jpg

Hivi ndivyo jinsi basi la burudani lilivyoharibika katika ajali iliyotikea leo asubuhi wilaya ya handeni

burudani5.jpg

Majeruhi wakipatiwa matibabu na huduma ya kwanza

burudani6.jpg
Manesi nao wakiendelea kutoa huduma kwa majeruhi
Mungu atujalie usalama hasa wakati huu wa msimu wa siku kuu.
 
Mungu awarehemu ndugu zetu wote waliotangulia mbele ya haki, pamoja na kuwapatia nafuu ndugu zetu waliojeruhiwa.Vilevile awape mioyo ya subira wale wote walioondokewa na ndugu, jamaa na marafiki zao.Ameen!
 
Back
Top Bottom