Ajali mbaya Handeni, basi la Burudani limeua 12

Allah awalaze mahala panapostahili marehem wote na awape nafuu ya mapema wale wote waliojeruhiwa
 
Sio uongo hili bus linajaza sana abiria kupita uwezo wake sijui ni unafuu wa nauli au nini??
 
du polen wafiwa wote na mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.
 
Duhhh,so sad!Jamani na kipindi hiki cha kukaribia sikukuu,madereva kuweni makini sana barabarani na wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri hakikisheni vyombo vyenu vinapata matengenezo ya mara kwa mara,walinzi wa usalama(askari) simamieni sheria za usalama barabarani!
 
Soo sad! Nimepita pale hali inatisha!!inasemekana kulikuwa na ukungu na kuna lorry liligonga bus ubavuni ndio likakosa mwelekeo likaenda bondeni!! Nimeshindwa kabisa kuchukua picha
 
Wee mpenda picha huwa unaona ufahahari gani kuomba picha ambazo wakati mwingine zaeza kuwa ni za marehemu au mazingira ya tukio hayastahili kuchukua picha?? ili iweje?? hebu tupe majibu huwa zinakungezeanini labda ili tuongeze bidii ya kutafuta picha hata kwa tukio usilositahili kuona??
 
ila KABUKU NA MBWEWE ni maeneo ya ajali sana kwa hii njia ya kwenda kaskazini,

kinachonishangaza siku ya uhuru basi la kampuni hii hii lilipata ajali maeneo hayo hayo sasa je kuna nini hapo??
je madereva wake ni wagen kiasi kwamba hawajui hilo eneo?? ama je wanadharau alama za barabaran zilizoko hapo maeneo?? ama hakuna alama za kutosha kuongoza magari eneo hilo??
 
basi linaitwa burudani linatoka korogwe limedumbukia kwenye korongo karibu na kwarugulu estate.

kwa mujibu wa askari niliyemkuta hapo wakisaidia majeruhi,watu 12 wamefariki hapo hapo. wangine kadhaa wamelaliwa na hilo basi.

wale wapicha wanisamehe,nimeshindwa kuchukua picha kutokana na mazingira.

ImageUploadedByJamiiForums1386829774.246369.jpg
 
Habari ya kusikitisha sana hii...

Burdan ni basi lenye jina kubwa na kwa routes za Lushoto - Dar - Lushoto...ni basi litumiwalo sana na raia wa kada zote.

Mungu awape afya majeruhi wote waliokutwa na ajali hii.
 
kama unasafiri kwa kuendesha ama kwa mabasi utajua ni kiasi gani madereva wa mabasi ni 'wendawazimu' na ajali kama hizi zikitokea huwa sishangai ingawa nasikitika sana.....zinaepukika!
 
jamani polena wahanga wote wa tukio hili, wote tuwaombee majeruhi ili wapone haraka na wafiwa wafarijiwe
 
Back
Top Bottom