Pwani: Basi la kampuni ya Saibaba lapata ajali Kongowe, watu 18 wajeruhiwa, lilikuwa likitokea Sumbawanga

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Kuna ajali mbaya imetokea muda huu kati ya bus la Sai baba na tipper (mende) inasemekana majeruhi ni wengi na vifo pia.. Barabara ya morogoro eneo hilo imefungwa kwa muda... Kwa ambao wanatumia njia hiyo tafadhali tumieni mchepuko wa old Morogoro road

Sai baba ilikuwa linatoka Sumbawanga kama una ndugu ama jamaa jaribu kufuatilia

Jr

=====

Basi ya kampuni ya Saibaba yapata ajali asubuhi hii. Basi hiyo ilikuwa safarini kutokea jijini Dar Es Salaam kuelekea mjini Sumbawanga. Chanzo chake bado hakijafahamika mara moja

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Kongowe, basi la kampuni ya Sai baba Express baada ya kugongana uso kwa uso na lori.

1581487979034.png
PWANI: Basi la abiria Saibaba lapata ajali kwa kugongana uso kwa uso na lori na kujeruhi abiria 18, Kamanda athibitisha
PWANI: Basi la abiria Saibaba lapata ajali kwa kugongana uso kwa uso na lori na kujeruhi abiria 18, Kamanda athibitisha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa, amesema kuwa jumla ya watu 18 wamejeruhiwa katika ajali ya Basi la Saibaba lililogongana uso kwa uso na Lori asubuhi ya leo ya Februari 12, 2020.
RPC%20NYIGESA.jpg

Kamanda wa Polisi Pwani, ACP Wankyo Nyigesa

Kamanda Nyigesa amesema kuwa ajali hiyo imetokea katika eneo la kongowe na kusema kuwa majeruhi watano wamekimbizwa katika Hospitali ya Mloganzila kwa ajili ya matibabu na wengine wapo katika Hospitali ya Tumbi.

“Chanzo ni mwendokasi wa Lori uliopelekea kuligonga Basi la Abiria, Basi la Saibaba lilikuwa linatoka Sumbawanga kuelekea Dar es Salaam, hakuna vifo, majeruhi ni 18 na majina yao hayajafahamika kwasababu hawakuweza kuongea” amesema ACP Nyigesa.
picnida.jpg

Kwa mujibu wa Kamanda Nyigesa amesema kuwa Jeshi la Polisi, linajitahidi kufanya mawasiliano na kampuni ya mabasi hayo ili lilelete gari nyingine kwa ajili ya kuwachukua abiria walionusurika na kuwapeleka Dar es Salaam.

Chanzo EATV
 
Mshana ulikuwa unatokea Sumbawanga au Mpanda?

Mzigo wako wa mitishamba umesalimika.

Mungu awaponye na kuwapa wepesi majeruhi wote!
 
Mashuhuda wa ajali wanasema dereva wa bus ndio Mwenye makosa... Ni ile tabia yao ya kuchomoa na kuchomeka.. Alipochomoa akashindwa kurudi kwa wakati ndio ikatokea head collision...


Jr
 
Usahihi wa taarifa toka kwa abiria aliyenusurika ni kwamba gari lilikuwa uelekeo wa Dar kutokea Sumbawanga na walitembea usiku kucha mpaka Moro ambapo walipumzika saa moja tu na kutembea mwendo mdundo
From Dsm to Sumbawanga... na sio Sumbawanga to Dsm, I guess.

Jr
 
Back
Top Bottom