Ajali mbaya Handeni, basi la Burudani limeua 12

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,391
2,000
Inasemekana lilikuwa linatoka Korogwe likielekea Dar e Salaam.

Limeanguka katika kijiji cha Taula Handeni.

Limeua abiria 12 hapo hapo na majeruhi ni wengi kwa mujibu wa Breaking News ya Radio One.

Poleni sana mliopoteza wapendwa wenu, na majeruhi ugueni pole.


Picha:Vijimambo
 

Attachments

  • DC Korogwe.png
    File size
    544.4 KB
    Views
    1,173

Watu

JF-Expert Member
May 12, 2008
3,234
2,000
Nimepokea taarifa basi burdani likitokea korogwe asubuhi ya leo limepata ajali maeneo ya kabuku na inasemekana zaidi ya abiria 22 wamefariki hapo hapo
 

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,524
2,000
So sad! RIP Marehemu wote.Kabuku,mahali pabaya sana pale kwa njia ya Moshi-Arusha.Sijui kwanini!?
 

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
13,459
2,000
Mwisho wa mwaka kuna matukio sana ya namna hii. Madereva wawe makini. Pole kwa majeruhi na wafiwa.
 

Blessed

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
3,123
2,000
Inasikitisha sana,Pole kwa majeruhi Mwenyezi Mungu awape uponyaji mapema!
 

mnyepe

JF-Expert Member
Dec 1, 2008
1,914
1,225
Hilo basi mwezi wa 10 ilipata ajali mbele ya kabuku. Hay a majeruhi mungu awape nafuu ya haraka na waliotangulia wapumzike kwa amani
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,108
2,000
Kwa habari nilizonanzo ni abiria 12 kama wamefikia 22 sina uhakika. Majeruhi wako Hospital ya Magunga Korogwe. Poleni sana. Ilikua gari ya kwanza kutoka Korogwe-Tanga Kuja Dar ambapo ingefika saa nne. Mungu awarehemu na kuwatia nguvu wote
 

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,797
0
Nimepokea taarifa basi burdani likitokea korogwe asubuhi ya leo limepata ajali maeneo ya kabuku na inasemekana zaidi ya abiria 22 wamefariki hapo hapo

Hili bus huwa linatembea speed ya kawaida sijui nn imelisibu.
 

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
36,740
2,000
basi linaitwa burudani linatoka korogwe limedumbukia kwenye korongo karibu na kwarugulu estate.

kwa mujibu wa askari niliyemkuta hapo wakisaidia majeruhi,watu 12 wamefariki hapo hapo. wangine kadhaa wamelaliwa na hilo basi.

wale wapicha wanisamehe,nimeshindwa kuchukua picha kutokana na mazingira.
 

kyanaKyoMuhaya

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,952
2,000
Tarehe 9.10.2013 lilipata ajali eneo hilo hilo.
image.jpg


Picha ya basi la kampuni ya Burdan linalofanya safari za Lushoto-Korogwe (Tanga) na Dar es Salaam limepata ajali katika eneo la Kabuku, Handeni wakati likielekea Dar es Salaam. Taarifa za watu wa maeneo hayo zinasema mtu mmoja ameripotiwa kufa huku wengine wakiachwa na majeraha. Kandili Yetu Leo: PICHA: AJALI MBAYA YA BUS LA BURDAN, HANDENI MKOANI TANGA

NA leo tena. RIP
 

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
36,740
2,000
watu8 nimepita hapo ndani ya nusu saa iliyopita naeleka tanga. nilisimamishwa na askari vijiji viwili nyuma kufika eneo la tukio. nikakabidhiwa bahasha yenye fomu za pf3 na kuzikabidhi katika eneo la ajali.
askari anasema watu 12 wamefariki hapo na kadhaa wamelaliwa na hilo basi.
 
Last edited by a moderator:

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
May 10, 2012
5,290
2,000
basi linaitwa burudani linatoka korogwe limedumbukia kwenye korongo karibu na kwarugulu estate.

kwa mujibu wa askari niliyemkuta hapo wakisaidia majeruhi,watu 12 wamefariki hapo hapo. wangine kadhaa wamelaliwa na hilo basi.

wale wapicha wanisamehe,nimeshindwa kuchukua picha kutokana na mazingira.
kabanga asante kwa taarifa picha bado muhimu siku hapa jf
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom