Mbeya: Basi la Kampuni ya BEST LINE lapata ajali katika Kijiji cha Ilongo

Mbeya: Basi la Kampuni ya BEST LINE lapata ajali katika Kijiji cha Ilongo

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,277
Basi la Kampuni ya BEST LINE lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza limepata ajali ya kupinduka asubuhi ya leo Machi 28, 2018 katika Kijiji cha Ilongo kilichopo mkoani Mbeya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema kwamba hadi sasa bado hakuna taarifa za vifo, isipokuwa majeruhi tu...!
IMG_20180328_084217_966.jpg


=======

CHANZO CHA AJALI BEST LINE MBY

Anaandika afande RTO MBEYA.
Ni kweli ajali imetokea lakini hakuna madhara kwa binadamu.

Chanzo cha ajali ni kwamba lorry lililokuwa linatoka Njombe kuja Mbeya lilikuwa linaovateki magari mengine na basi la Bestline lilikuwa linatoka Mbeya kuelekea Mwanza likiwa kwenye "lane" yake.

Baada ya kuona watagongana uso kwa uso dereva wa basi akaona atoke nje ya barabara na kwenda kutumbukia kwenye mtaro kushoto. Juhudi ya kuwafaulisha abiria zinafanyika.
 
Poleni sana majeruhi wa ajali..madereva kuweni makini mkiwa barabarani kuepusha ajali.
 
Treni utakua usafiri wangu pekee miaka yote
 
Mwenyezi Mungu awaponye Majeruhi
Na wawe na afya kama hapo awali. Ameen. Dereva wa Lori ni mzembe kwa kutaka kuyapita magari mengine aisee..!
 
Back
Top Bottom