Ajali Karatu: Basi la Coastline lapinduka kwenye kona maarufu kama 'Kona ya Hatari'

client

JF-Expert Member
Dec 13, 2015
661
846
Wakuu mida hii kuna pilika nyingi mno inasemekana basi kubwa aina ya Coastline linalofanya safari zake za musoma kwenda arusha imepinduka kwenye kona maarufu kama' Corner ya hatari' iliyoko mita chache kabla ya kufika Mto wa Mbu


MwanaJamiiForum aliyeko maeneo atupe taarifa zaidi

Updates
Shughuli za uokoaji zinaendelea,inasemekana gari limepinduka juhudi za kulipindua zinaendelea

Coastline.JPG

Maelfu ya watu wamekusanyika eneo la tukio wakishuhudia suala la uokozi

Magari mbalimbali ya watu binafsi na ambulance za hospital ziko busy kwa sasa kukimbika kila abiria alitolewa katika basi hilo lililokwama,magari 3 ya shirika la TANAPA wapo shughuli za uokozi

Greda limefika kwa ajiki ya kupindua gari

Updates: Gari tayari limepinduliwa na abiria wengi wao wamepelekwa hospital ya Rhotia na ambao hali ziko vibaya wamehamishiwa hospital ya Lutheran karatu

Update:T aarifa ambazo hazijadhibitishwa ni kwamba watu wanne wamefariki

Wengi Wa abiria hao inasemekana wamevunjika viungo mbalimbali vya mwili

Chanzo cha ajali inasemekana ni break kufeli katika mteremko mkali wenye corner

----
WANANGU WAWILI WAPATA AJALI, MMOJA AVUNJIKA MGUU NA MWINGINE MKONO

Kuna ajali limetokea karibu na Karatu ambapo Basi la coastline limeanguka na kuua na kujeruhi watu. Watoto wangu wawili Ni miongoni mwa waliokuwemo.

Nimeongea nao kidogo Sana maana wote wamevunjika, mmoja mguu mwingine mkono. Sikuweza kupata Hali halisi kutokana na wao kuanza matibabu.

Basi lilikuwa linatoka Musoma kwenda Arusha. Please mwenye taarifa kamili au jirani na matukio atujuze.

UPDATE
Washapata huduma ya x-ray aliyevunjika mguu anahamishiwa KCMC
 
Kama ni ni upande wa kulia kushuka mlimani itakuwa HATARI SANA hiyo kona Z macheje weka mbali

Eneo la Ajali ni KILIMATEMBO kuna mteremko kiwembe sana jamaa kaamuwa kulipiga chini .....vinginevyo lingepaa juu ya Migunga huko chini...
 
Coastline ya wapi mkuu? Maana jama gari zake nyingi zinaenda chaka sana.
 
Poleni sana coastline na abiria wahanga wa ajali.
Huo mtelemko na kona kali ni hatari sana.Madereva jitahidini sana kuchukia tahadhari
 
ila hawa coastline basi zao zinakwenda mwendokasi sana, poleni sana majeruhi
 
  • Thanks
Reactions: rr3
Back
Top Bottom