Ajali Barabarani: Tuzijue sababu, kuepuka upotoshwaji

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,891
Ajali barabarani ni janga kubwa lenye kuhitaji ufumbuzi sahihi.

Ajali zinaleta vifo, majeruhi, umasikini, hasara, na vyote vyenye kuambatana na hayo.

Ni ukweli usiopingika kuwa ajali zinasababishwa na haya:

1) ujinga - mwendo kasi wa kizembe, ulevi, fujo, utoto, nk barabarani yakiwamo matumizi hovyo ya simu.

2) Kukosa umakini kutokana na usingizi, uchovu, ulevi, nk.

3) Ubovu wa magari, barabara.

#1 linabeba zaidi ya 90% ya tatizo. Jitihada za mwendazake kutaka minimum education kwa madereva kwa kuanza na wale wa Serikali alikuwa na hoja.

#1 Linajieleza zaidi kwanini nchi zilizoendelea Wana viwango vidogo zaidi vya ajali pamoja na kuwa na
magari mengi zaidi per capita.

Ninakazia: Siyo 1, 2, wala 3 yenye kutanzuliwa na polisi wa usalama barabarani.



Viva Abdulhaman Omari Kinana wiki moja iliyopita wengi wetu matumizi kwa rushwa barabarani yalipungua sana.
 
Hiyo point #1 ndio tatizo kubwa. #1 ikidhibitiwa, ndio inakuwa suluhisho la #2 na #3.

Kwa hakika watu hawa hawawezi kusaidia kuondoa tatizo la ajali:



Kivyao vyao bila shaka sasa IST, Tractor, Hilux, na Scania zote zinapaswa kuwekwa pembeni ya kuwa ni mbovu kwani hivi karibuni zimehusika kwenye ajali.

Polisi traffic mmetunyonya sana kwa rushwa zenu. Hatutapoa hadi kieleweke.
 
Kinachoumiza zaid sisi abiria hatupazi sauti kwa hawa madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani kukemea maovu yao, kama speed kali, matumizi ya simu au utoto. Pia hatutoi taarifa kwa mamlaka husika juu ya ukiukwaji huo.
TUBADILIKE WATANZANIA

Ujinga - dawa yake ni elimu. Pana haja ya kupigania minimum education kwenye usukani. Kelele kwa wajinga haziwezi kuwaelimisha wala kuwa mbadala katu.
 
Uchambuzi mzuri. Madereva wakijitambua vema, wakaacha ulevi na ligi za kipuuzi barabarani, ajali zitapungua sana.
 
Ajali za barabarani Kwa tanzania Kwa asilimia 90 ni Uzembe WA Madereva.

Imagine zile basi za sauli na Newforce huwa zinashindana Nani atafika Mbeya Mapema.

Solution: serikali iwekeze kwenye technology ; nchi hii ina vijana wengi wanaojua kutengeneza mifuno ya kupunguza hizi ajali. Traffic police pekee hawawezi. Wizara ya sayansi waitishe Challenge ya vijana kubuni mifuno ya technology ya kupunguza ajali. Nakuhakikishia itapatikana mifumo hizi ajali zinaweza kupungua hata Kwa asilimia 90.

Tatizo la nchi yetu siasa ni nyingi kila sehemu. Na WAnasiasa ndio wanaonekana kuwa na akili kuliko watu wote wakiwemo hata wataalam WA technology sababu inayopelekea wao pekee kuwa wanatoa mawazo.



Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
🙏🙏Asante mkuu Kwa kupaza sauti Yako juu ya hili linaloongeza watu tegemezi kila kukicha.
#1 Ujinga kiukweli unatumaliza na kutufanya tudumu kwenye dimbwi la umaskini. Mjinga mMoja anambebra buku mjinga mwenzake Ili punde tu anapokamatwa Kwa kosa lolote ampatie yeye aendelee na Ujinga wake na yule mwingine abaki na Ujinga wake.
It's shame.
 
Panueni njia kisha tenganisheni. Hakuna haja ya Camera wala askari. Wa kwenda waende wakiwa upande wao wa kurudi warudi wakiwa upande wao uone kama utasikia story za ajali.

Serikali yenye uwezo wa kutoa ruzuku ya billion 100 kila mwezi kwa mwaka ni kilometre ngapi itajenga? Do the maths
 
Hoja nzuri ila umeiandika kisiasa na kiuoga,#3 ndio tatizo kubwa hapo, freeways zetu ni mbovu mno na zimejengwa chini ya kiwango,T1 life span yake imeisha miaka mingi iliyopita,hii barabara imejengwa miaka ya 60s!,kinachofanyika sasa wanatia vilaka visivyoendana na barabara yenyewe, na why uweke matuta kwenye freeways?,elewa pedestrians, bodaboda, etc etc hawaruhusiwi kuwa ndani ya freeways, mkuu Dar to Mbeya ni almost 800km huu ni mwendo wa masaa 9 kwa bus tuache uzuzu hapa, Sauli wapo speed ya kawaida ni wapi safe, personal advice no one forcing you kusafiri na SAULI, kuharibu brand ya Sauli ambayo wamewekeza kwa muda mrefu binafsi will fight for sauli brand, kawaida bus ikiondoka Dar 6am by 1600 iwe Mbeya tena nimeweka na muda wa mapumziko na matatizo ya kitonga pass
 
Mwakata saa nne usiku siku ya nane nane:

1. Tractor na tela yalikuwa barabarani bila taa wala reflector.
2. IST ikiendeshwa kwa kasi iliyopitiliza na bila tahadhari yoyote dereva wake hakubaini uwepo wa chochote barabarani.
3. Hiace ikiendeshwa kwa kasi kupita eneo lililokuwa na ajali iligonga gari lililosimama kwenye shughuli za uokoaji.

4. School bus ya Mtwara ikiendeshwa kwa kasi isiyo mithilika ilitumbukia kwenye shimo ikiwa imebeba watoto wa umri wa miaka 5 wakiwamo.
5. Nk nk.

Ndugu mjumbe camera au barabara pana kiasi gani zingeepusha haya na madereva kama hawa?
 
Sehemu kubwa ni ubovu wa miundombinu...
Magari mengi hasa makubwa tena mabasi mengi ni mapya

Sehemu kubwa ni ujinga mkuu. Rejea Mwakata saa nne usiku hata Mtwara asubuhi asubuhi na school bus.
 
Kuna changamoto nyingi, lakini pia madereva wasio wazoefu ni chanzo. Unakuta mtu hajawahi kuendesha njia ndefu mfano dar mwanza, kila siku yuko dar mjini anazunguka. Hyo siku ya ajali anaamua kufungua mapafu long trip tena kwa kuamka usiku kukwepa tochi na wakati hajui barabara. Na unakuta anatembea kibati, chochote kikitokea lazma ale mzinga.
 
Uko nje ya mada. Rejea thabiti ajali karibuni Mwakata, Singida au ya Mtwara ya watoto wa shule.

Uoga? Siasa? Labda kama hujui maana ya maneno hayo.

Mwakata saa nne usiku siku ya nane nane:

1. Tractor na tela yalikuwa barabarani bila taa wala reflector.
2. IST ikiendeshwa kwa kasi iliyopitiliza na bila tahadhari yoyote dereva wake hakubaini uwepo wa kizingiti chochote barabarani.
3. Hiace ikiendeshwa kwa kasi kupita eneo lililokuwa na ajali iligonga gari lililosimama kwenye shughuli za uokoaji.

4. School bus ya Mtwara ikiendeshwa kwa kasi isiyo mithilika ilitumbukia kwenye shimo ikiwa imebeba watoto wa umri wa miaka 5 wakiwamo.
5. Nk nk.

Muundo mbinu upi ungepisha haya na madereva wajinga na wazembe kama hawa?
 
Hizo ni isolated accidents, main reason ya ajali nyingi ni miundo mbinu mibovu tuliyokua nayo, hata alama za usalama barabarani hakuna
 


Hii ndio suluhu kuu
 
Yani hapa mkoani kahama kiufupi madereva wengi wanajifunzia humu humu hakuna bajaji,pikipiki,gari na vyombo vingine.

nilichoka yani mtu unavuka barabara na anakuona ila ndio kwanza anaongeza mwendo .

mfano wa pili hapa kahama watu hawafahamu sheria hata kidogo na hakuna ukaguzi makini ili mradi maisha yana songa.
 

Hii inaanguka sawia kwenye ujinga kipengele #1 kwenye mada.

Ninakazia: Traffic police hana kazi hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…