Ajali Arumeru Mashariki Mnara Wa Simu Waua

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,995
2,494
Mitaa Ya Mji-Mwema Sokoni Ilioko Leganga, Usa-River Katika Wilaya Ya Arumeru Mashariki Kumetokea Ajali.

Mnara Wa Kampuni Ya Simu Za Mkononi Umeanguka Na Kusababisha Moto Mkubwa Unaondelea Kuunguza Mali Na Nyumba Za Watu.

Mpaka Sasa Hivi Kuna Taarifa Kuwa Watoto Wawili Mapacha Wa Miaka Miwili Wamepoteza Maisha Yao.

Dakika Kumi Na Tano Zilizopita Gari Ya zima moto imefika na wanategemea nyingine kufika muda huu kusaidia juhudi za uzimaji na uokozi.
 
Gari Ya kwanza ya fire ilofika imekwisha maji na moto bado unateketeza mali
 
Poleni sana wana arumeru,na haya nimatokeo ya viongozi wetu kufanya kazi kwa mazoea na kukubali miradi mingine kuwa nayo majumbani pasipo kuangalia madhara yake,na sisi wananchi huwa hatuhoji madhara yanayoweza kupatikana na minara au mambo mengine yanayotokea kwenye jamii yetu
 
Polisi Na Raia Wanaleteana mtiti hapa, baadhi ya fire brigades wamekunywa
 
Wazazi wa Watoto mapacha walofariki wamezimia hapa
 
poleni sana sana wakuu
Mwenyezi Mungu azilaze roho za hao watoto mahali pema
na walioumia au kushtushwa na hilo wapate nafuu mapema
 
Sad news Nadhani hii imetokana na aina ya udongo wa pale USA. Hii minara mingi imejengwa kwenye makazi ya watu. na sasa haya makazi yetu ya high density, ni hatari kwa kweli.
 
Hii minara ya simu mitaani ilipingwa sana na wanamazingira zamani zile lakini hawakusikilizwa. Makampuni yanavyozidi kuzaliana kila kukicha ndo inaongezeka na athari zake ikiwemo mionzi hatujui ni kiasi gani. Pia udhaifu wa serikali unaruhusu minara rojo rojo kujengwa holela tu. Tuombe hili lisaidie kuiamshe serikali
 
kwanini wanajenga kwenye makazi ya watu?poleni sana mkuu..hao fire kawaida yao,mi nilishuhudia moto ukiteketeza home kwetu kisa jamaa wamekuja na nusu tenki maji yakawaishia ndo waite gari lingine...yaani unapoteza watoto kipumbavu
 
Ama kweli hatari ya moto ni mbaya sana!

Na ukizingatia chini ya yale minara kunakuwagana na jenereta kubwa sana yenye uwezo wa kubeba lt 600 ama 400 ya desel.
Je? Huo mote wenyewe wa desel si janga tosha.

Poleni sana wazazi waliopoteza watoto wapendwa.
Watoto mpumzike kwa Amani ya Bwana!
 
Back
Top Bottom