Ajali yaua mkuu wa ujasusi ECUADOR

Ajali yaua mkuu wa ujasusi ECUADOR

Miss Halima

Senior Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
140
Reaction score
345
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa la Ecuador, Michele Sensi Contugi pamoja na Mkewe ni miongoni mwa watu saba ambao wamefariki dunia baada ya helikopta kuanguka katika eneo la Mlima Ololokwe, Kaunti ya Samburu nchini Kenya.

Duru za siasa za Kimataifa zinapata wasiwasi kuwa huenda ni tukio la kigaidi au tukio lililopangwa likimlenga Mkuu huyo wa ujasusi ambaye inaaminika alikuwa Kenya kwa mapumziko.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA) imethibitisha ajali hiyo ikisema imehusisha helikopta aina ya Eurocopter EC130 B4 yenye usajili namba 5Y-GYM, kwa mujibu wa KCAA, helikopta hiyo ilikuwa imetoka Loisaba ikielekea Ewasonyiro wakati ajali ilipotokea majira ya saa 3:13 asubuhi Agosti 19, 2026 kwa saa za Afrika Mashariki,

Helikopta hiyo imeua pia Wamarekani watano ambao Ubalozi wa Marekani Nchini Kenya umethibitisha vifo vyao huku Televisheni ya Telemundo ikisema imempoteza Kiongozi wake Jose Suarez kwenye ajali hiyo.

Ripoti ya Polisi imeeleza kuwa Ndege hiyo ndogo iliyofahamika kwa jina la Lady Lorry ilikuwa ikisafiri kutoka Soyian-Laikipia kuelekea Loisaba Conservancy kabla ya kuanguka.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Samburu, David Nkoroi,amesema moshi mzito ulionekana ukitanda eneo la tukio huku vikosi vya uokoaji vikifika haraka kutoa msaada, huku Mashuhuda wakieleza kuwa moshi mweusi na moto mkubwa vilionekana mara baada ya helikopta hiyo kuanguka, hali iliyowafanya wakazi kutoa taarifa na kuhamasisha hatua za dharura kutoka kwa Vyombo vya usalama na timu za matibabu.

==============================

Director General of the Department of National Security of Ecuador, Michele Sensi Contugi and his wife are among seven people who died after a helicopter crashed in Mount Ololokwe, Samburu County in Kenya.

International political circles are getting worried that it might be a terrorist event or a planned event targeting that intelligence chief, who is believed to be in Kenya on vacation.

The Kenya Air Transport Authority (KCAA) has confirmed the accident, saying it involved a Eurocopter EC130 B4 helicopter with the registration number 5Y-GYM. According to KCAA, the helicopter was leaving Loisaba heading to Ewasonyiro when the accident occurred around 3:13 am August 19, 2026, East African time,

The helicopter has also killed five Americans, whose American Embassy in Kenya has confirmed their deaths, while Telemundo Television says it has lost its leader, Jose Suarez, in the accident.

The small aircraft known as Lady Lorry was travelling from Soyian-Laikipia to Loisaba Conservancy before it crashed, a police report has revealed.

The Samburu County Police Commander, David Nkoroi, has said heavy smoke was seen sweeping the scene as rescue teams rushed to render assistance. Witnesses narrated that black smoke and heavy flames were seen immediately after the helicopter crashed; the situation prompted residents to issue a statement and prompted emergency measures. From the security forces and medical teams.

KENYA.png
 
Back
Top Bottom