Airtel: Kifurushi cha intaneti cha TSHS 2,500/-

Airtel: Kifurushi cha intaneti cha TSHS 2,500/-

SASA okoa hadi 90% ya gharama zako za internet.Jiunge na kifurushi maalum cha sh 2500 tu kwa mwezi na upate MB 200.kujiunga Sms neno INTERNET kwenda 15444..
Yep!! Washachomoa plug...nimebaki njia panda..niendelee nao au ndo mda wa kushuka basi umefika!!
 
Mbona jana nimejiunga mkuu na kulamba MB 400 au hiyo kitu imeanza leo?!
 
wamenirushia ujumbe wao wa kutangaza 2500 kwa mb 200, nimerusha hewani wametoa mb 400. kinachokera, hata speed ya kinyonga ni kubwa. kama hawataki tutumie huduma zao, si waache tu kuliko kutudanganya?
 
Hiyo sms me pia nimeipata leo asubuhi,hawa jamaa wameamua kutuchezea kama kagame
 
kuna kila dalili kuwa hawa jamaa wamelewa sifa na soko limewashinda,hakuna cha 3G wala 3.75G,ni upuuzi mtupu ,bei ya sasa itanifanya nifikirie kuwahama hawa jamaa
 
jana nimejiunga na kupata mb400 balaa lake speed kichefu chefu
 
Hawa jamaa speed yao ni ndogo sana tofauti na wanavyojitangaza. Nilidhani ni modem yangu tu kwaajili nipo machakani huku.
 
Mbona mimi wamenitumia 400mb kwa 2500.Iweje wewe wakutumie tofauti?Au wewe airtel mimi zain
 
nyie hamjaelewa speed zao zipoje the more urahisi wa bundle the more speed ndogo na soon wataanza kutoa bundle za 2g ambazo hupat 3g kabsaaaaaaaaa. Huo ndo ukapitalisti ila kama utatoa laki ununue net yao tegemea more speed
 
NOW save up to 90% of your internet charges.Subscribe to a special bundle for only 2500 sh per month and get 400 MB.Sms INTERNET to 15444 NOW

mimi nimepata hii lkn ni 400mb leo saa tano
 
Ni mtandao gani huu kuna mb400 kwa sh 2500? Maana airtel walishaiondoa siku nyingi sana. Kuna mb25 kwa sh 1500/ piga *154*44#
 
Wenzao wanaweka unlimited za siku tatu kwa buku tano wao ndo wanashusha viwango na bei zilezile!! Mda wa kuwakacha sasa!!
 
Ni mtandao gani huu kuna mb400 kwa sh 2500? Maana airtel walishaiondoa siku nyingi sana. Kuna mb25 kwa sh 1500/ piga *154*44#
@kinyoba, hii bado ipo, naitumia sana kwenye simu.
 
Ni jana tu time za saa sita kasoro nilikuwa ninatumia modema iliyokuwa imeungwa na kifurushi cha 400 Mb, the speed wasn't bad kama inavyozungumza, au nimezoea ukonokono nikiona kinyonga naona kama formular one!!!
 
Back
Top Bottom