Acheni Hofu!
Hayo matangazo ya kwenye SMS ni uda mrefu sana sasasa wamekua wakiyatuma kwa wateja. Naamini ni njia mojawapo ya kuwapunguza wateja kutumia mtandao kwa muda mrefu(scare tactics) ili kuwafanya wengi wabaki within fair usage limit ambayo kwa ile 2500/400Mb ni ngumu kuifuata.
Wewe tuma Internet kwenda 15444 hata kesho itakupa 400Mb kama kadawia na inakaa mwezi mzima. Naitumi hiyo bundle kwenye modem na kwenye iPad na kote inapiga kazi hata sasa ninapoongea hapa.
Kufanya modem iwe fast:
Hii najua ni ngumu kwa wengi kuamini lakini kuna viujanja vidogo vidogo vya kufanya modem yako ya airtel iwe faster. Kwanza kabisa naanza kwa kusema kwamba kitu rahisi kabisa kutumia ni modem ya Vodafone kisha ndani weka laini ya Airtel. Kuitumia, wewe install ile software inayokuja na hiyo modem ya Vodacom kama kawaida kisha ikishamaliza weka laini yako ya Airtel, ukienda kwenye upande wa kulia chini ya display yako utaona kale kasehemu ambako huwa tunatumia kutafuta wireless networks, kuna moja itakua inaitwa Vodafone web sessions, ifungue hiyo itakuuliza Username, Password na Access Point Name, hizo username na password acha tupu, kwenye access point weka neno Internet. Ukifanya hivyo mara nyingi nimeona modem za vodafone(ZTE) zinakamata 3G kirahisi kuliko za Airtel(wamezibana wenyewe = FUP again).
Kama huna modem ya Voda, namna nyingine rahisi ni kuingia kwenye settings za hiyo hiyo modem ya Airtel na kutafuta settings za connection options, humo wewe uchague 3G tu itakua kwa maneno kama UMTS Only au HSPDA only ama HSUPA only ama hata 3G only. Uliishaiweka hiyo save settings kisha ichomoe na kuirudisha modem. Ukiona imewasha taa ya bluu inablink, jua unakula 3G na ni kwa spidi ya hatari, ukiona inawaka taa nyekundu tu, jua hilo eneo halina 3G rudi kwenye settings na urudishe Dual Mode.
Sina lugha rahisi ya kuelezea hili jambo ila in summary, limit your Airtel modem to 3G Only ama timua modem ya Voda/Tigo na laini ya Airtel.