Airtel - Get The Modem That Gives You Free Internet - Huu ni Uongo

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Wakuu nimehamasika na matangazo ya Airtel kwenye redio hata hapa Jamii Forum tangazo lao liko hapa juu lisemalo nanukuu:

Get the modem that gives you free internet:
Buy for only 30'000 Tsh and get free internet for 6 months visit airtel shop now!
Mwisho wa kunukuu. Basi nimetoka muda huu hapa Airtel shop kama walivyosema na hapa kwenye ofisi zao Arusha nimepata bahati ya kumkuta shemeji yangu anayefanya kazi hapa nilipomuuliza shemeji vipi naweza kupata hii huduma amnayotangaza mpaka kwenye redio jibu alilonipa ni kua hilo tangazo ni uongo na ni biashara tu! Sikutaka kupoteza muda wangu nikaishia zangu mpaka naleta uzi huu je huu uongo wa biashara ndio mtindo wa kisasa? Nawasilisha.
 
Mkuu hizi ni lugha za kibiashara.., na kabla sijawaita waongo inabidi kusoma small prints..,
(Masharti na Vigezo Kuzingatiwa)

Hivyo basi kisheria kama labda wanakupa hata 400mb za kuanzia ambazo zitadumu miezi sita kama hutatumia (lakini kama ukizimaliza kwa dakika kumi, zitadumu dakika kumi) hapo wanakuwa hawajasema uongo sababu kama utatumia chini ya hicho kiwango kwa miezi sita utakuwa umetumia bure (au kwa lugha nyingine hautahitaji kuongeza salio)

Hivyo basi ni vema tukajizoesha kusoma small prints kwenye contract... (mimi sijazisoma hivyo siwezi kusema wamedanganya mpaka nione hizo small prints.., in other words huwezi kuwapeleka mahakamani kwa kudanganya mteja)
 
we una bahati umemwona shemeji yako kakwambia ukweli...sie wengine tukienda watakwambia zimeisha mpaka wiki ijayo
zilizopo ni za sh 80,000/=, ukienda wiki hiyo watakwambia hazijaja bado...ukiwa mzito kusoma alama za nyakati
kama gamba utapiga rapa sana ktk ofisi zao
 
Back
Top Bottom