Naibu Waziri Kihenzile: Airport ya Tanga Kuboreshwa na Kuwa ya Kisasa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imewahakikishia wananchi wa Tanga kusudio lake la kuuboresha uwanja wa ndege wa mji huo hususani katika jengo la abiria, maegesho ya ndege, na eneo la kuruka na kutua ndege ili kuendana na mahitaji.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David kihenzile amesema hayo mara baada ya kutembelea uwanja wa ndege wa Tanga na kuona uhitaji wa maboresho hayo.

“Ukiangalia tumekaa kwa kipindi kirefu hakujawahi kufanyika mabadiliko yoyote katika Airport hii hivyo Rais ameona ni muhimu kufungua mkoa wa Tanga kwenye upande wa usafiri wa anga kwa kuhakikisha ndege kubwa zinatua hapa na uwepo wa Airport ya kisasa ndani ya jiji la Tanga” Alisema Kihenzile.

Aidha Naibu Waziri amesema uboreshaji wa uwanja huo wa ndege, utaenda sawa na mahitaji ya sasa na fursa zilizopo ndani ya mkoa wa Tanga ikiwa ni pamoja na fursa ya uwekezaji wa bomba la mafuta ambalo litaongeza idadi ya wageni watakaohitaji kutumia usafiri wa aina mbalimbali ukiwemo usafiri wa anga.

WhatsApp Image 2023-10-20 at 17.05.19.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-20 at 17.05.18.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-20 at 17.05.19(3).jpeg
WhatsApp Image 2023-10-20 at 17.05.20.jpeg
 
Porojo kabisa kwani TAA mbona huu uwanja haupo kweny plan zao za maboresho.
 
Back
Top Bottom