Aina za Ndoa .... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aina za Ndoa ....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by FirstLady1, Mar 28, 2012.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ndoa yako ni ya aina gani katika haya magroup?

  1.Ndoa za mapenzi ..
  Hapa ni ile true love ambayo wote mnajikuta mmependana na hatimaye kuamua kuwa mke na mme

  2.Ndoa za Kulazimisha
  Hizi ni zile ndoa binti anaweza kuamua kubeba ujauzito na kutumia kama kigezo cha kuolewa
  Na mwanaume anaamua kuoa kwa sababu tu hana namna (Hapa mnaweza kuongeza maana sababu ni nyingi sana.

  3.Ndoa za kutamaniana.
  Mmeajikuta katika tamaa za kimwili mmeendelea na kutamaniana hatimae inafikia hatua mnawekana ndani..
  Matamanio yakiisha kasheshe zinaanza

  4. Ndoa za Madawa
  (msinipige mawe heheh)Hizi mambo zipo bwana vibinti vya siku hizi vinakamata watu kwa kuwatumia kalumanzira basi dawa zikishindikana kurenew kasheshe zinaanza ndani ya nyumba..mara ooh mara eeh.

  5. Ndoa za kuoneana huruma- By PakaJimmy

  Unakuta binti anakusimulia maisha aliyopitia...magumu sana, na hakika anatamani asingezaliwa!..
  Ukimsikiliza kwa umakini waweza kata shauri kumuoa!

  6.Ndoa ya kudimba dimba. By Ashadii
  Nje hawa watu ni perfect couple... Ila humo ndani kila mtu na maisha yake; wanakua tu na an understanding, kama mtu anafanya upuuzi iwe mbali na isijulikane na vice versa. Mara nyingi hii inakua as a result ya kuchokana kabisa na kutopendana na wote wakakubali hali halisi. Hivo badala ya kuondoka hapo na kuanza upya wanaona waendelee kushare hasa vile walivochuma pamoja ili mradi nje wasijue hilo.

  Bibi yangu alikuwa ananipa hili somo na kuniuliza mjukuu wangu wewe upo Kundi gani katika haya ?

  Kazi kwenu wana MMU


   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  FL1,
  Mi sijui niko group gani mpaka itakapofika saa mbili usiku leo...na wewe uko kundi gani au utasubiri muda uende ukitafakari kama mimi?
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,977
  Likes Received: 23,681
  Trophy Points: 280
  Ndoa za kubakana....

  Hizi zilikuwa zinafanyika sana kule kwetu Moshi hasa kipindi cha Christmass misa ya usiku.

  Unavizia kabinti kametoka church unakatupia mgongoni. Kakiingia room unakabaka, kesho hakaondoki ndo imetoka hivyo.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsaten sana FL1,

  Naona hizi ni aina za ndoa kwa mtazamo wa jinsia ya upande wa pili....Itabidi na sie tuangalie uwezekano wa kuweka aina za ndoa kwa upande wetu!!

  Hiyo No. 4 ni ngumu sana kwa wale tusioamini ndumba na urozi!!

  Naipenda sana No. 1 ila sijui ni asilimia ngapi ya ndoa zimebahatika kuipata!!!

  Babu DC!!!
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hizi ni common sana kwa makabila mengi....Bishanga anaweza kutupa ushahidi zaidi...!!

  Halafu inashangaza kwamba hizi ndoa zinadumu sana wakati zile za mission town, ambazo watu wanajidai kupendana sana zinadumu kwa muda mfupi...Nyingine hata honey moon haiishi!!

  Babu DC!!
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ha saa mbili utakuwa ok baada ya vimiminika kama vitatu hivi...
  Lakini unajua bwana ya kwako iko group gani ..?
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  AsprinHizi ndo zenu bado zipo mpaka leo??
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  Babu DC hebu weka mtizamo nyuma ya shilingi..
  Lakini Babu hivi bibi wakati ananisimulia alijua hizi namba nne zipo labda ya kwake ilikuwa namba 4
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Mie nadhani 2 na 3 ndiyo common sana,

  Hiyo nambari one ni ngumu sana kwa wanaume.....!!

  Babu DC!!
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,977
  Likes Received: 23,681
  Trophy Points: 280
  Zipo, sema tu siku hizi zimekuwa advanced... Yaani mnapanga kabisa na binti kwamba leo usiku uje unikamate unipeleke kwako unibake afu unioe....
  Source: Ukosefu wa mahari.
   
 11. condorezaraisi

  condorezaraisi JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ya kwangu ni namba Mbili umenigusa ...Maswali hayaruhusiwi:wink2:
   
 12. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  that is mine......
   
 13. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  teh umenikumbusha mbali babu?
   
 14. condorezaraisi

  condorezaraisi JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Preta una vituko sana nimecheka sana ....kwi kwi kwi
  Niambie ikawaje shost?
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  FL1,
  Kuna aina hii ya ndoa ambayo katika makundi hayo yako inaangukia wapi!
  Mwanamke anapompenda mwanaume, au vice versa, kwaajili ya fedha na uwezo!..then umasikini ukipiga hodi mlangoni penzi linasepa kupitia dirishani!
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Pia kuna ndoa za kuoana kwa kumwonea huruma mtu!
  Unakuta binti anakusimulia maisha aliyopitia...magumu sana, na hakika anatamani asingezaliwa!..
  Ukimsikiliza kwa umakini waweza kata shauri kumuoa!
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ndoa za FAMILIA KUPENDANA!...
  Unakuta familia mbili zimekuwa na urafiki wa aina yake....wanakuwa wametengeneza undugu kabisa...Sasa kama kuna vijana rijali wanaamua kufanya kweli kutokana na loophole ya urafiki wa hizi familia, na wazazi automatically wanalipokea wazo hilo!
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Halafu sehemu nyingine wasichana wamekuwa laini laini sana kiasi kwamba hata wale vijana wasio na uwezo wa kupiga sound nao wanapata. Vijana wengi ambao ujanja ni karibu na zero ndio walikuwa wanaponea kwenye kapu la kukamata mzigo na kuwahishwa home kwa msaada wa washikaji!!

  Ila nazo zilikuwa na kasheshe zake...Kwa kina Bishanga, nasikia kama binti alileta ubishi, ile timu ilitakiwa kumsaidia kumshikia mshikaji hadi apate sunnah!!

  Babu DC!!!
   
 19. condorezaraisi

  condorezaraisi JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngoja nijaribu ..hii inaangukia kwenye 2 maana nimeona ameweka kwamba kwenye mbili kuna sababu nyingi ambazo hajaorodhesha ,,analazimisha kuolewa mambo yakiwa mazito ndoa inakimbiwa .
  Kuna shost wangu alikimbia ndo kasema ya nn umasikini maisha yenyewe mafupi:thinking:
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  PJ,

  Ni kweli kabisa...ndoa za huruma na maslahi ni common sana....

  Ila nadhani hakuna ndoa isiyo na element ya maslahi ......

  Kuna binti aliambiwa na mama yake kwamba akimwacha huyo mchumba wake ambaye hakuwa na pesa wakati huo ila alikuwa mtu wa michongo, basi angekoma...Ndoa ilifungwa na utabiri wa mama ulionekana baadaye kuwa wa kweli!!

  Babu DC!!
   
Loading...