Noo!! wanaume wanaweza sana ku-pretend inategemeana na anataka nini kutoka kwako, binafsi Kitu kilichotufanya tudumu kwa mda mrefu katika mahusiano ni kwamba yeye alikuwa yupo busy sana na mimi hali kadhalika hivyo tulikuwa tunakutana katika aidha business au starehe na advantage iliyokuwepo yeye alikuwa ana nyumba yake na mimi nilikuwa ninaishi kwangu, kwasababu alikuwa anaishi na wadogo wake hivyo alikuwa analala kwangu mara chache sana, mara nyingi alikuwa ananibana sana katika suala la kufunga ndoa, nasita kabisa kutoa mbinu nilizokuwa nazitumia kufanya Delaying ya kumuoa kwasababu hata mimi binafsi sizipendi siyo nzuri wakizitumia na watu wengine kwakweli, ofcourse hata yeye anaweza akawa member humu JF nikizitaja zitamfanya ajijue specifically kwamba ni yeye ninayemzungumzia, kiukweli kitu nilichomfanyia hata mimi huwa kinanikosesha amani kwakweli nashukuru Mungu nasikia ameolewa.